Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 3,841
- 5,823
KWANINI AFRICA NI BARA MASIKINI?
Heshima yenu wakubwa na wadogo.
Bara la Afrika ni bara la pili kwa ukubwa baada ya Asia, ni bara lenye kila aina ya utajiri na rasilimali za kutosha.
La kushangaza ni bara masikini kuliko yote na la mwisho katika kila kitu, yaani ni masikini kiasi cha kustaajabisha.
Je, tatizo ni nini? ni kitu gani kinachosababisha bara hili kuwa masikini kiasi hiki?
Haya ni mambo matatu yanayoweza kuwa chanzo cha yote.
1: JE, NI ELIMU?
AFRICA imekuwa iikitumia elimu ile ya mkoloni. elimu ambayo ipo ili kuandaa watu waje kufanya kazi ya mtoa elimu huyo yani mkoloni. na sio elimu ambayo itakujenga kifikra au kiakili. Sio elimu itakayokujenga uwe mbunifu na kutumia ubunifu huo kutatua changamoto zako na za jamii yako. elimu itakayokufanya ujitambue ili ujitegemee utegemee akili yako binafsi. HAPANA bali ni inayokuandaa kuwa mtumwa uliye advance.
Hadi leo elimu hii inafanya kazi ya kukalilisha watu mambo ambayo hayana impact kwenye maisha yao zaidi ya kwenda kuomba kazi ambayo ataifanya maiha yake yote mpaka kufa kwake.
Hivyo nadhani elimu ni tatizo kubwa linalotufanya tuendelee kubaki hapa tulipo. Hivyo suluhisho ni kubadilisha mfumo mzima wa elimu yetu hii tunayoitumia.
2: JE, NI SIASA?
Africa bado tunafanya siasa ambayo haina tofauti na ukoloni. Viongozi wetu wote wanafanya mambo amabayo yana asili ya ukoloni ndani yake. UFISADI, RUSHWA, MASLAHI BINAFSI na WIZI bado vipo ndani ya siasa ya Africa.
Mwanasiasa anaiaba pesa anakwenda kuweka nje AFRICA. Uchumi wetu karibu asilimia 60% upo nje.
Siasa nalo ni tatizo pia. na tatizo hili linatokana na ELIMU ambayo nimeelezea hapo juu. Viongozi na wananchi ni zao la elimu ya mkoloni ambayo haimjengi mtu kujitambua{self awareness} Haimjengi mtu kutumia akili yake ipasavyo kama nilivyosema juu.
Hivyo siasa ni tatizo linalotoka na elimu yetu. solution ni kubadirisha mfumo wetu wa elimu. Alafu tutakuwa tumepiga ndege wawili kwa jiwe moja.
3: JE, NI DINI?
AFRICA tumekuwa tunatumia dini zilizoletwa na Mkoloni.{DINI ZOTE} dini ambazo zimeletwa ili kujenga hofu {fear} kumbuka ukitaka kumuendesha na kumteka mtu basi anza kumteka akili kwa kumjengea hofu.
Hivyo dini ni ya mkoloni ni jambo ambalo linachangia kwa kiasi chake kulibakiza BARA letu pendwa kuendelea kubaki nyuma na kubaki kuwa masikini miaka yote. dini imejenga mitazamo kwa watu ambayo ni migumu kung'oka. Solution ni ngumu kwa hapa sababu hii kitu ipo kwenye damu na imani amabayo ni ngumu kuibadirisha.
MFANO mdogo ni pale ambapo Mwafrika anakutwa na tatizo na kushindwa kuitatua sababu ana imani litatatuliwa na hicho anachoamini. Hii inapelekea kubweteka na kusubiria hivyo kubaki na tatizo hilo milele.
Hayo ni mambo matatu makuu yanayosababisha Afrika kuendelea kubaki nyuma kila siku. wewe Mwafrikaunadhani ni nini kinacho
sababisha afrika kubaki nyuma mpaka leo hii kwani miaka karibu 60 imepita tangu Mkoloni aondokea Tanzania na nchi baadhi za
Afrika.
Maoni yako nini?