Miezi miwili iliyopita wakati ugonjwa wa Covid-19 uliposhika kasi nchini China na baadaye Ulaya na Marekani, wataalamu wa magonjwa walijaribu kutabiri mahali gani kwengine COVID-19 itaangamiza zaidi
Wengi walifikiri Afrika itakuwa eneo linalofuata kuwa na hatari kubwa, lakini baada ya kufika COVID-19 barani Afrika utabiri wote mbaya haukuwa kweli
Sababu kuu za kwanini Afrika imeepukana na utabiri huo
Watu wengi wamekuwa na nadharia tofauti. Baadhi wanasema uwepo wa vijana wengi. Wakati vifo vingi vya COVID-19 katika Ulaya vimewagusa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60, umri wa kati wa watu wa Afrika ni miaka 19, na asilimia 60 ya bara la Afrika ni watu wenye umri wa chini ya miaka 25.
Wengine wanasema kwasababu hakuna takwimu sahihi kwa vile wengi hawakupimwa.
Lakini kwa ujumla ni kwamba wakati nchi za Ulaya zikisita kuchukua hatua, nchi za Afrika zilichukua hatua mapema za zuio, kuweka karantini na kupima watu joto. Pia Afrika imepambana na magonjwa mengi ya mlipuko hivyo ina uzoefu wa kupamabana na magonjwa.