Elections 2015 Kwanini 2015, CCM mlituletea kiongozi asiyekuwa na maono hata ya miaka kumi ijayo?

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,282
3,077
Tangu, nchi hii ya Tanzania ipate Uhuru imepita katika vipindi mbali mbali vya uongozi. Katika vipindi hivyo tumeshuhudia viongozi wenye sifa tofauti. Lakini walikua na moja ya sifa ambayo ilikua inafanana ya kua na maono ya mbele juu ya Taifa la Tanzania. Japokua hayo maono yao hayakuweza kufikiwa kwa asilimia kumbwa lakini walionesha hata kwa dhamira zao kua kuna sehemu wanataka Tanzania ifike.

Lakini kwa kiongozi ambaye CCM walituletea 2015 ni tofauti kabisa na maraisi wa awamu zilizopita. Ni kiongozi ambaye anataka kufanya jambo ili aonekane kafanya bila kuangalia kua ilo jambo litatupeleka sehemu gani kwa miaka mingine mbele. Ili limejidhihirisha kwenye kampeni zinazoendelea sasa.

Ukimsikia huyu mgombea wa CCM, ameshindwa kabsa kuonenesha kua nchi yetu ameitoa wapi na inaelekea wapi.Cha ajambo na ambacho kimenifanya kuhoji juu ya maono ya huyu mgombea juu ya nchi yetu ni yapi ni ile kauli yake kua ni wasipomchagua yeye wanaokuja wataharibu alivyovifanya, ina maana watu wataenda kuvunja flyover ya Ubungo, wataziharibu Ndege alizonunua nk. Napata ukakasi na kusudi la dhati alilonalo Magufuli juu ya nchi yetu ya Tanzania.

Je, ni kwamba Tanzania haitakua na kiongozi mwingine zaidi yake?. Je, yeye ana mkataba na Mungu kwamba hatakufa kamwe? Maana sisi sote ni binadamu tunaozaliwa na kufa. Na kama akifa nchi itaendelea kuongozwa na yeye maana wengine wataharibu vitu alivyoviasisi?

Je, akimaliza miaka kumi ka katiba inavyosema hataondoka kwa kuhofia wengine wataharibu alivyovifanya?. Je, ana maono gani ikitokea amekufa na kabla ya hata muda wake kutimia?

Kiongozi mwenye maono ni Yule anayejenga msingi wa nchi yake utakaodumu hata miaka mia moja. Hii inamaana hata akiondoka kuna watu watakuja wataendeleza alipoishia kama yeye alivyoendeleza, Yeye kajenga flyover ya ubungo kuna watu walijenga barabara za nchi wakaweka hadi mataa, hiyo ilikua hatua ya msingi kabisa.

Tanzania inahitaji kua na kiongozi mwenye maono ya mbali kuliko kua na kiongozi anayetaka sifa yake ivume sana kuliko nchi kuvuma. Maana hakuna mtu ambaye ni mkubwa kuliko Tanzania.
 
Aiseeeeee. Wanakuja kutukana matusi tena ya nguoni! Hawana hoja wamebaki kutukana
 
Apumzike tu kwa kweli sisi binadamu wa Tanzania tumemchoka asubiri muda wake ukifika akaombe kuongoza malaika.
 
Tutamchagua Magufuli!

Hatutachagua mtu atakaeongoza nchi yetu kwa matakwa ya beberu wake Amsterdamu sisi
 
Ila dunia hii ina watu wa ajabu sana,hata kudanganyishia tu utapandisha mshahara hutaki,kwenye biblia ilitabiriwaga misri kutakuwa na miaka 7 ya shibe na miaka 7 ya njaa lakini huku kwetu tumetoka miaka 5 ya njaa na jiwe anataka kuturudishia tena kwenye miaka mingine mitano ya njaa badala ya kutupeleka kwenye miaka 5 ya shibe
 
Hawa ndo mtaji wao
FB_IMG_1599150682564.jpeg
 
Ulitaka awe na maono hata kwenye nchi yenu huko?

Sisi huku Tanzania, Amekuwa na maono ya vizazi vinne vinavyo, Kuna Reli ya Kisiasa itayodumu hata miaka 200 ijayo, kuna bwawa la kuzalisha umeme vizazi vingi vijavyo

Kuna bomba la mafuta litalobebe historia miaka mingi ijayo

Sasa unataka na kwenu huko Gambia awe na maono ya nchi yenu Ili Iweje?
 
Back
Top Bottom