G Jonathan Kamenge
Member
- Apr 8, 2023
- 43
- 29
Mnisamehe lakini sasa budi niulize maswali yangu kadhaa, nipate mantiki na uelewa na nipate majibu ya kimantiki ya Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam.
Kwanza braza Chalamila anisaidie kuelewa ni Watanzania wangapi wanaishi "Ikulu" , Boma, Ushuani na ni wangapi wanaishi "Kitaa" na ikiwa anajua kwamba "mitaa" hasa ndiyo nchi!!? Kwa umuhimu wa "mitaa" tuna kitu nchi hii kinaitwa "Serikali za mitaa" na kina Wizara nzima inaitwa "Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa" ambayo Chalamila ni mtumishi wake. Kuna kosa gani kwa "Kitaa" kusema tunataka taifa letu kwenda hivi!!?
Kitaa ndiyo kinalipa kodi na hivyo kugharimia Serikali za Mitaa na hata Serikali kuu. Kitaa ndicho kinatoa rasilimali watu wanaolitumikia taifa letu katika ofisi za umma na binafsi, Kitaa ndiyo kinatoa vipaji na kufanya Wasanii, Viongozi wa Dini, Wanasiasa, Mafundi Sanifu na Wabunifu wengine, Chalamila anaelewa kosa analofanya kudharau Kitaa!!?
Kitaa ndicho kinapaswa kupiga kura kuchagua viongozi wetu na Kitaa kinaposema kwa hali ilivyo kwa Sasa hatuwezi kuwa na uchaguzi wa kweli, halisi na wa haki, kuna kosa gani!!? Chalamila hataki kusikia sauti ya Kitaa, hataki kusikia sauti ya wengi!!? Kwani tafsiri ya Chalamila ya neno Demokrasia ni ipi!!?
Mchakato wa Uchaguzi utafanya Rais Samia aendelee kuongoza hadi mchakato utakapokamilika!!? Ebu tuwaze pamoja. Kwani Watanzania walimpigia kura Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!? Pamoja na kwamba hakupigiwa kura kuwa Rais, si bado amekuwa Rais mzuri na amelivusha taifa letu kwenye kipindi kigumu cha kufiwa na Rais aliye madarakani kwa amani na utulivu!!? Ametuvusha kwenye changamoto ngumu za mabadiliko ya kiuchumi baada ya COVID-19!? Kuna ubaya gani kuamua kama nchi kwamba Samia Suluhu Hassan aendelee kuwa Rais wetu kwa mwaka hata miaka miwili mbele wakati tukifanya mchakato wa Katiba mpya!!? Chalamila anaogopa kuona Watanzania tukiandika ukurasa mpya kwenye historia yetu wenyewe tena kwa amani kabisa bila kuuana, kupotezana, kukatana vichwa kwa kisingizio cha "amani na utulivu"!!? Anaogopa nini!!? Kwamba historia hiyo itaondoa nafasi za vijana machawa na kuweka vijana "waasi" kwenye mamlaka, vijana waliotabiriwa na kutakiwa na Muasisi wa CCM, Julius Kambarage Nyerere!!?
Tuendelee kuwaza pamoja. Kwani kuna shida gani kwa Rais Samia kuendelea kuongoza taifa letu kwenye mabadiliko ya Katiba, ikiwa "wazee" kwenye chama waliongoza kile walichokiita "uteuzi" na kumpa nafasi ya kuwa mgombea pekee wakiweka kando Katiba ya CCM na Katiba ya Tanzania inayotaka kuruhusu mgombea wa uchaguzi kushindanishwa na wenzie ndani ya chama!!? Kwani tuna imani na Samia pale tu inapokuwa ni kwa maslahi ya wachache, lakini tuna mashaka na Samia inapokuwa ni kwa maslahi ya Nchi!!? Kwani Chalamila anamtumikia nani anayemtuma kujaribu to undermine uwezo wa Rais Samia kuongoza mabadiliko na changamoto kubwa za kijamii kama nilivyotaja hapo juu!!? Chalamila kaambiwa na nani kwamba Watanzania hawamuamini Rais Samia kuongoza taifa kupitia mabadiliko ya Katiba hadi uchaguzi huru na wa haki!!?
Chalamila anafahamu kwamba Tanzania Ina zaidi ya nusu ya watu wake kuwa vijana na kwamba hata waliofanya maamuzi ya kumpitisha Samia kuwa mgombea ni "wazee wa chama" na hivyo ni wachache kati ya wengi, na wanaopaswa kupiga kura ni vijana ambao ndiyo wengi!!? Chalamila anaelewa nini anaposikia "Chama kina wenyewe na wenyewe ndiyo sisi!?" Au anadhani "sisi" hiyo inahusisha kikundi kidogo cha watu ndani ya chama na hivyo chama siyo cha wanachama!!? Kama takwimu ni sahihi, basi zaidi ya 6milioni ya wanachama wa CCM (zaidi ya 50%) ni vijana na hiyo ingemaanisha CCM ni ya kwetu vijana, Chalamila anamsemea nani anapomtilia shaka Rais Samia kuongoza taifa hili kupitia mchakato wa Katiba!!? Maoni hayo ni ya nani na ni ya wangapi katika taifa la watu zaidi ya 60milioni!!? Au ni egocentrism ya kudhani kwa vile kwa Sasa yeye anakalia kiti, basi ana akili na utashi kuliko sisi wengine wote!!?
Hivi kwanini tumekuwa na viongozi wanaotoa maapizo (Kuna tofauti ya apizo na kiapo nadhani turudi tukajifunze) kwenye majukwaa!!? Mmoja juzi amedai kukata vichwa vya watu akiwa madhabahuni, na leo huyu anadai "never happen on Earth" kwa vile yeye haoni uwezekano wa hilo kutokea kama ambavyo mwenzake hakuona uwezekano wa kulinda amani, haki na Usalama wa Taifa letu bila kukatana vichwa. Nini kinafanya mnaamini kwamba muono wenu ndiyo sahihi kuliko sisi wengine wote!!? Hii dharau kwa watu mnaipata wapi!!? Kwanini mnamtusi Rais bila kumtusi mnapoonekana kumaanisha kwamba Watanzania kudai zaidi kwa Rais wao ni dhambi, mnadhani she can't deliver!!?
Nawaza tu kibanangabananga wala msinijali!!!