Kwani Rais anateua sana kutoka UDSM? Mzumbe na UDOM vipi?

Ethos

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
2,294
2,000
Wakuu..

Nimekuwa nikifuatilia teuzi zilizotukuka za mh Rais..

Kama kawaida hupenda sana kujaza Academicians katika nafasi mbalimbali hasa wahadhiri wa vyuo vikuu.. Hivi Leo katika teuzi Tatu ni wahadhiri wa vyuo..

Kipindi cha nyuma niliwahi msikia Prof Mkandala akilalamikia kuhusu upungufu wa wataalam hawa pale UDSM Lakini mkuu Amekuwa akiwapangua kila kukicha..

Swali langu ni Je, vyuo kama Mzumbe, UDOM au hata Ardhi huwa havina wabobezi wa maswala mbalimbali? Kwanini hapo UDSM?

Hebu nieleweshwe tafadhali... Nataka kuelewa tu... Sina lingine!!

Ethos.
 
Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
3,962
2,000
Huenda vyuo vingine vina Wahadhiri wachache sana kiasi kwamba ukimng'oa mmoja wanabakia wachache hivyo huleta Upungufu mkubwa sana wa Wakufunzi.

Pili,huenda anatoa Ahsante kwa chuo alichokisoma. Analipa fadhila kwao.

Tatu,huenda watu wanaohitajika kujazwa kwenye nafasi husika wengi wenye ueledi huo wapo Chuo kikuu cha Dar es Salaam hivyo kuwa na ulazima wa kuwateua tu.

Nne,huenda anayeteuliwa amewahi kufanya kazi mahala tajwa kabla ya kuwa Mhadhiri chuoni. Au labda wana uzoefu na eneo tajwa linalohitaji uteuzi.

Au labda vyuo vingine wanateuliwa lakini wanakataa teuzi.

Mawazo yangu tu.
 
Asante.. Naanza kupata picha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom