Kwani ni lazima wanawake wadeke?

kudeka raha jamanh hasa ukimpata anayejua kudekeza mana kuna wanaume wengine lol
 
Jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia kwamba wanawake kuumwaumwa ni aina yao ya kudeka ili wajue kama mwanaume unampenda kweli au magumashi. Pia siyo kila kilio cha mwanamke ni kilio cha kweli.

Hata mimi naamini kwamba wakati mwingine wanawake "wanaumwa" ili wawe karibu na wapenzi wao.Au wanalia ili wabembelezwe.

Sasa kwani ni lazima wanawake wadeke ndiyo wajue wanapendwa kwa kubembelezwa?
wangu amezidi kupretend khaaaaaa!s ome times *nikimgombeza kdogo *kesho yake lazima 'aumwe"hata *akitaka nirudi mapema "anaumwa"NK, some times nashindwaga kujua wakati gani anakua anaumwa kweli au la,so naamua kumchunia hadi nione amezidiwa
 
Mtu kila weekend anaumwa Mara anataka umshikilie anapokwenda chooni, umpikie chakula kwa sababu anadai anasikia kizunguzungu, umwogeshe, umfulie Ch&@i yake, ukitoka kidogo mesegi kibao kwamba umemtelekeza. sasa Ashadii anasema ni kutaka attention mimi kwa uelewa wangu lengo la kudeka ndiyo hilo la kuvuta attention.

Sasa na kulia ndiyo huko tena. Jambo dogo chozi hilo.... Nakubaliana na Tz1 kwamba kama kudeka basi wanawake dekeni wiki mbili baada ya hapo mnakera jamani. Maana wakati mwingine mnaongea au unamwelekeza jambo la maana yeye ghafla anabadili sauti na kuanza kuongea kama mtoto mdogo. Aaargh! Inakera bana.

we naweee! Kama anaumwa unashindwa kumuhudumia?
Sasa wiki mbili zikiisha hajapona afanyaje?
 
we naweee! Kama anaumwa unashindwa kumuhudumia?
Sasa wiki mbili zikiisha hajapona afanyaje?
wiki mbili hajapona tu!!? Tatizo tumeshawastukia kwamba nyinyi wakati mwingi mnakuwa mna- act mnaumwa kumbe hakuna kitu.
 
Jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia kwamba wanawake kuumwaumwa ni aina yao ya kudeka ili wajue kama mwanaume unampenda kweli au magumashi. Pia siyo kila kilio cha mwanamke ni kilio cha kweli.

Hata mimi naamini kwamba wakati mwingine wanawake "wanaumwa" ili wawe karibu na wapenzi wao.Au wanalia ili wabembelezwe.

Sasa kwani ni lazima wanawake wadeke ndiyo wajue wanapendwa kwa kubembelezwa?

Nafikiri umekariri, kama siyo fikra potofu uliyonayo kwa wanawake. Kama mtu anaumwa anahudimiwa kwa ugonjwa wake. Kudeka ndiyo nini? mifano yako haihusiani na neno KUDEKA.
 
kudeka kwa mwanamke kuna mfanya awe na mvuto hata wa kimapenzi labda huyo wa kwako hawiani na madeko anayofanya na yeye alivyo ndo maana inakuboa.Mfano kuna wasichana wana misauti ya kiume hao hawafai madeko yahusuyo sauti.
 
hahahaha! Hili nalo neno.
 
Wee endekeza mawazo yako hayo yakujidanganya mwanamke kuumwa umwa ni kawaida, kumbe mwenzio, anaumwa
Kweli unadhani anadanganya.

Mwanamke kuumwa muhimu, mtu atoke job kachoka afike home kazi zina msubiri, duuh

Kati kati ya usiku aamshwe kugawa doze kwa mwenyewe, hee ye kawa nani asiume mikazi yote hiyo na kulihudumia lijitu lizima mchezo.
 
kulihudumia lijitu lizima mchezo.
Jamani msituite mijitu wenzenu!! labda kwa vile mnatuona ni mijitu ndiyo maana mnadhani kwamba bila kudeka hatuwezi kuwajali!!

Na hii ndiyo maana ya kudeka kwa mujibu wa Kamusi ya Taasisi ya Ukuzaji Kiswahili (TUKI).

Dek.a kt [sie] 1 demand attention. 2 show conceit, be arrogant. 3 hope to get something from somebody you are sure could help. (tde) dekea; (tdk) dekeka; (tds) dekeza.

Haya waswahili wenyewe tafsiri yao ya kudeka ndiyo hiyo tena!!
 
Back
Top Bottom