Kwani kutokuwa na fedha ndio utakufa......!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwani kutokuwa na fedha ndio utakufa......!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vukani, Oct 18, 2011.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwaka 1936, wakati ulipotokea uhaba wa fedha taslimu kule Tenino, Washington, Marekani, noti zilitengenezwa kutokana na mbao kwa kipindi kifupi. Kulikuwa na noti za mbao za thamani ya dola 1, 5, na 10.

  Kwa hiyo, leo hii mtu anapoona bila fedha maisha hayawezekani, inabidi umshangae sana. Kama hivi majuzi tu, sarafu ziliisha kwa nchi kama Marekani na watu wakaamua kuchukua mbao na kuunda noti za mbao, ina maana gani? Ina maana kwamba, siyo fedha kwa maana ya kitu fulani, bali kwa njia ya kubadilishana.

  Kwa ujumla, fedha zilianza kuisumbua dunia miaka 300 tu iliyopita, kabla ya hapo mabadilishano yalikuwa kwa njia tofauti. Lakini hata hivyo, bado binadamu alikuwa akihangaika na kuteseka kutafuta kwa kujilinganisha. Kwa hiyo ulafi, choyo, na husuda, havikutoka kwenye fedha, bali fedha imerahisisha tu tabia hizo kupokelewa kirahisi na jamii na kuwa sugu.

  Hivyo tunaweza kabisa kuishi bila fedha na maisha yakawa bora zaidi. Kinachotakiwa ni mabadilishano ambayo wala hayana kutumia nguvu wala hayana kuumizana.

  Najua Wahafidhina mtabisha, hebu soma hii maneno hapa: http://www.ci.tenino.wa.us/wooden_money.htm
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hebu watengeneza sasa hivi waone...............
  Mafundi randa wangekuwa mamilionea
   
Loading...