Kwani Kiingereza ndio lugha ya mapenzi?

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,166
1,247
Hivi wana JF kuna uhusiano gani kati ya hii lugha ya malkia na mapenzi?.Nimejaribu kufanya uchungunzi mdogo nimegundua kwamba CARD au SMS nyingi za mapenzi zimeandikwa/zinaandikwa kwa luga ya kiingereza.Utakuta mtu na mpenzi wake labda wote ni wasukuwa,w anyamwezi,wapale nk lakini bado ktk maongezi yao utasikia ...i miss you...i lov you...honey...HIVI KWELI KISWAHILI HAKINA MANENO MATAM NA YENYE-MVUTO KTK MAMBO YA MAHABA?...nawataadhalisha wapendanao...ukiona mtu anapenda sana kutumia luga ya mkopo,angalia isijeikawa ata hizo hisia anazotoa kwako amekopeshwa...
 
...HIVI KWELI KISWAHILI HAKINA MANENO MATAM NA YENYE-MVUTO KTK MAMBO YA MAHABA?..

Hapana, si kweli. Kiswahili kina misamiati mingi tu ya kimahaba iliyo mitamu na yenye mvuto. Tatizo kubwa nilionalo mimi ni sisi waongeaji wake ndiyo hatukithamini na kukitumia ipasavyo. Na bila kufanya hayo mawili hakitaweza kukua na kupanuka kama ambavyo baadhi yetu tungependa.

Kasumba tuliyotiwa na wakoloni imetuathiri vibaya sana. Imetufanya tusithamini vya kwetu. Kuna watu wanakihusisha Kiswahili na hali ya uduni au ukosefu wa ustaarabu. Na badala yake wanahusisha Kiingereza na ustaarabu na hali fulani ya kiwango cha maisha.

Kwenye jamii yetu mtu akiwa anajua Kiingereza anaonekana kama kastaarabika. Anaonekana kama msomi. Anaonekana kama ana akili sana. Kinyume chake, mtu akiwa hajui Kiingereza au akiwa hakijui vizuri anaonekana kama hana akili. Tunamcheka na kumkejeli. Mfano Kanumba yule mcheza filamu.

Sheria zetu nazo zimeandikwa kwa Kiingereza. Sijui tumemwandikia nani kwa lugha hiyo. Labda zinawafanya wale wadada na wakaka wasomi (wanasheria) wajione na kujisikia "wamesoma". Manake ndiyo wanavyojiita hivyo. Lakini hilo kwangu ndiyo kilele cha upumbavu na ujinga.

Kama watu wengi wangekuwa wanakipenda Kiswahili kama ninavyokipenda mimi basi sina shaka kingekuwa kimekua na kupanuka kuliko kilivyo sasa. Huko tunakoelekea sasa hivi kina hatari ya kupotea ama kumezwa na hiki kinachoitwa 'Kiswanglish'. Inasikitisha sana hasa kwa sisi tulio wapenzi wake.
 
Hiyo labda kwa watoto wa siku hizi, sie wa zamani Kiswahili mwanzo mwisho, popote saa yoyote :]
 
Tatizo la kiswahili ni kuwa kinachotumika mitaani ni tofauti na kinachotumika vitabuni (mtazamo wa kiujumla). Lakini kwenye mapenzi,maneno mengine yanakua kama yamepungua ladha ama yameongezeka ukali zaidi. Kuna maneno ya kiswahili kuyatamka mapenzini inakua ngumu kidogo hadi ukishikilie mahali,lol
(Hivi 'LOL' kiswahili utasemaje?)
 
Tatizo la kiswahili ni kuwa kinachotumika mitaani ni tofauti na kinachotumika vitabuni (mtazamo wa kiujumla).

Hata Kiingereza nacho kiko hivyo hivyo. Njoo nikupeleke Bankhead au Mechanicsville tuone kama utaambulia chochote!

Lakini kwenye mapenzi,maneno mengine yanakua kama yamepungua ladha ama yameongezeka ukali zaidi. Kuna maneno ya kiswahili kuyatamka mapenzini inakua ngumu kidogo hadi ukishikilie mahali,lol

Unaona sasa...tatizo letu ni kudhani hayo maneno ya Kiingereza yalijileta tu yenyewe!

(Hivi 'LOL' kiswahili utasemaje?)

Napasuka mbavu (NM).
 
wengi siku hizi ni usanii tuu..

lakini ukikutana a yule ambaye anajua
hii lugha ya kigeni utafurahi kwa kweli...
 
Of coz kina cha kiingereza kinategemea na chimbulko na hata uzoefu. Hata kiswahili ulichoongea ukiwa mtoto sio sawa na uongeacho sasa. Na wajua neno la kijinga/chafu likiongelewa kidhungu unaona kama umejificha ama lina akili.
Hata Kiingereza nacho kiko hivyo hivyo. Njoo nikupeleke Bankhead au Mechanicsville tuone kama utaambulia chochote!

Unaona sasa...tatizo letu ni kudhani hayo maneno ya Kiingereza yalijileta tu yenyewe!

Napasuka mbavu (NM).
Unaona sasa,kupasuka mbavu, kuvunjika mbavu ama kuangua kicheko?
 
Maneno ya Kiswahili yanajitosheleza kwenye mahaba na mapenzi kwa ujumla.

Tunachokosea ni kutaka kutafsiri neno la Kiingereza kuwa la Kiswahili.

Mtu atasema nikitaka kuita "baby" jee?

Kwani lazima umuite "baby"? Maneno ya Kiswahili ya kimahaba na kiuchokozi wa mapenzi yapo mengi, hakuna haja ya kuita "baby" wala "I love you"
 
tatizo uzungu umetutawala ndo maana tunawapeleka watoto wetu kwenye hizi shule za international ili wajifunze kiingereza kiswahili watajifunza kwetu kule tunasemaga 'nikwenda bojo' yaani nakupenda sana
 
Binafsi nakubaliana na wewe, Maneno ya Mapenzi kwa kiswahili ni
mengi sana ila tu ndio hivyo, mara Ooohh Baby baby baby pumbafuuu,
sasa na mtoto mchanga utamwitaje???? mimi mwandani wangu simwiti
maneno ya kiingreza hata siku moja, nikitaka kuita utanisikia,
Mahabuba, Laaziz, Asali wa moyo na mengine mengi tu.
 
Wabongo utawaweza, kila anachofanya mwingereza wanakiona ni bora na cha kisasa kuliko vyao ndo maana siku zote nasema tumetawaliwa bado japo indirect bora ikiwa direct mtu unaweza kujinasua
 
Maneno ya Kiswahili yanajitosheleza kwenye mahaba na mapenzi kwa ujumla.

Tunachokosea ni kutaka kutafsiri neno la Kiingereza kuwa la Kiswahili.

Mtu atasema nikitaka kuita "baby" jee?

Kwani lazima umuite "baby"? Maneno ya Kiswahili ya kimahaba na kiuchokozi wa mapenzi yapo mengi, hakuna haja ya kuita "baby" wala "I love you"
yatajeni hayo maneno hapa km ambavyo mnatoa hiyo mifano ya lugha ya kiingereza
hii inaonesha wazi kuwa hata wanaoshadadia lugha ya kiswahili kwa matumizi yake katika mapenzi nao wamemezwa na hiyo inazoitwa 'lugha ya malkia'
 
Hivi wana JF kuna uhusiano gani kati ya hii lugha ya malkia na mapenzi?.Nimejaribu kufanya uchungunzi mdogo nimegundua kwamba CARD au SMS nyingi za mapenzi zimeandikwa/zinaandikwa kwa luga ya kiingereza.Utakuta mtu na mpenzi wake labda wote ni wasukuwa,w anyamwezi,wapale nk lakini bado ktk maongezi yao utasikia ...i miss you...i lov you...honey...HIVI KWELI KISWAHILI HAKINA MANENO MATAM NA YENYE-MVUTO KTK MAMBO YA MAHABA?...nawataadhalisha wapendanao...ukiona mtu anapenda sana kutumia luga ya mkopo,angalia isijeikawa ata hizo hisia anazotoa kwako amekopeshwa...

Body language ndo lugha ya mapenzi:)))
 
Back
Top Bottom