Kwani Kiingereza ndio lugha ya mapenzi?

Mwisho wa yote ni Wakurya, wakiwa wanatongoza utawasikia wakisema " umeorewa au bado unapigapiga umaraya?"
mkuu bujibuji ukinitaka radhi nitakukubalia,sie hatuko hivyo,tunajua mistari
 
Mwandani,wa ubani,mpenzi ,mahabuba,wa ubavu,la azizi
Mume wangu,bwanangu,asali wa moyo
 
Tatizo kuna maombi mengine ukitumia lugha ya kiswahili mbele ya watu ni matusi, mfano unaweza kuomba "K" hata mbele za watu kwa kusema "Let us make love tonight".

Je unaweza kuomba "K" mbele za watu kwa kiswahili?
 
Sabalkheri mpenzi, pambo lenye uwidadi
Ewe tunu mwenye enzi, tawasufi 'so idadi
Shaufu si mwanagenzi, wa kunitia midadi
Stahabu zako malezi, mwingi wa heshima jadi

Zumaridi lako jaha, hata uvikwe hijabu
Moyoni naona raha, kupita mali dhahabu
Sitoweza kukataa, kuwa na wewe thawabu
Chakula n'onapo njaa, la jibu langu jawabu

Mkirimu hakuhini, aliumba kwa sahala
Hakufanya uhaini, kakupa kila pahala
Mpaka naja kubaini, janati iso jalala
Naweka yangu saini, kama katika hawala

Watembea kwa maringo, ya kweli si singiziwa
Jumbo kiasi viringo, tambo lako kuridhiwa
Bashasha lisilo wigo, haiba wakabidhiwa
Hata pande za udigo, sijapata nadhamiwa

Uzuzu ninaupata, kukuona mdiria
Ulimi ninajing'ata, akili kifikiria
Roho inatapatapa, majadi yamenijia
Huba lililotakata, nisoweza malizia

Penzi fumbo la mjinga, na mwerevu kaingimo
Gonjwa lisilo na kinga, wote latuzidi kimo
Kurugenzi na machinga, sote letu hilo shimo
Hakuna ataepinga, kwa kusema "mimi simo"

Tamati na kaditama, ladha nisije chujua
Nimejipinda inama, kukujuza uje jua
Sina hali wala fana, jinsi unavyozuzua
Kujikimu sintofanya, bila yangu kwako dua
 
yatajeni hayo maneno hapa km ambavyo mnatoa hiyo mifano ya lugha ya kiingereza
hii inaonesha wazi kuwa hata wanaoshadadia lugha ya kiswahili kwa matumizi yake katika mapenzi nao wamemezwa na hiyo inazoitwa 'lugha ya malkia'

Haya hapa ushapewa

Mwandani,wa ubani,mpenzi ,mahabuba,wa ubavu,la azizi
Mume wangu,bwanangu,asali wa moyo

na mengine ni

Bibie, mboni, habibi, huba,
 
Tatizo kuna maombi mengine ukitumia lugha ya kiswahili mbele ya watu ni matusi, mfano unaweza kuomba "K" hata mbele za watu kwa kusema "Let us make love tonight".

Je unaweza kuomba "K" mbele za watu kwa kiswahili?

Mbele ya watu gani?

Sioni kama kuna tofauti ya hiyo sentensi ya Kiingereza na kusema "ningependa kuwa nawe pekee usiku wa leo"
 
Sabalkheri mpenzi, pambo lenye uwidadi
Ewe tunu mwenye enzi, tawasufi 'so idadi
Shaufu si mwanagenzi, wa kunitia midadi
Stahabu zako malezi, mwingi wa heshima jadi

Zumaridi lako jaha, hata uvikwe hijabu
Moyoni naona raha, kupita mali dhahabu
Sitoweza kukataa, kuwa na wewe thawabu
Chakula n'onapo njaa, la jibu langu jawabu

Mkirimu hakuhini, aliumba kwa sahala
Hakufanya uhaini, kakupa kila pahala
Mpaka naja kubaini, janati iso jalala
Naweka yangu saini, kama katika hawala

Watembea kwa maringo, ya kweli si singiziwa
Jumbo kiasi viringo, tambo lako kuridhiwa
Bashasha lisilo wigo, haiba wakabidhiwa
Hata pande za udigo, sijapata nadhamiwa

Uzuzu ninaupata, kukuona mdiria
Ulimi ninajing'ata, akili kifikiria
Roho inatapatapa, majadi yamenijia
Huba lililotakata, nisoweza malizia

Penzi fumbo la mjinga, na mwerevu kaingimo
Gonjwa lisilo na kinga, wote latuzidi kimo
Kurugenzi na machinga, sote letu hilo shimo
Hakuna ataepinga, kwa kusema "mimi simo"

Tamati na kaditama, ladha nisije chujua
Nimejipinda inama, kukujuza uje jua
Sina hali wala fana, jinsi unavyozuzua
Kujikimu sintofanya, bila yangu kwako dua

Nshagundua sijui kiswahili aisee
Huko red kote nimeona nyota...
 
Mbele ya watu gani?

Sioni kama kuna tofauti ya hiyo sentensi ya Kiingereza na kusema "ningependa kuwa nawe pekee usiku wa leo"

Ukimkuta aliyelelewa kiseminari kama mimi anakuuliza "ili iweje eti?"...
 
Tufanye maombi hadi liamba

:A S angel:

Sawa mpendwa... ngoja nimwambie na kaka eliakimu aisiende mkesha kule mbali leo aje tuombe naye maana najua ana upako kweli yule mpendwa
 
Kiingereza ni moja ya lugha kuu ambayo iko so (sexy) ndio maana inatumiwa sana kwenye mapenzi. Hapo kwenye mabano cjui kiswahili chake kitakachoweza kuweka mkazo
 
Mbele ya watu gani?

Sioni kama kuna tofauti ya hiyo sentensi ya Kiingereza na kusema "ningependa kuwa nawe pekee usiku wa leo"
Haina uzito anaweza asielewe bhana.

Anaweza akafikiri unataka kuwa naye Pub or Night Club.
 
Back
Top Bottom