Kwani hii dhana bado ipo...??

Heart

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
2,673
1,704
Kila siku watu wanapendana na wengine kuachana kutokana na sababu mbalimbali...hili suala la "age mates" kupendana lina tatizo jamani?? Maana nimekuwa nikisikia watu wakili-discourage sana,kwamba mtakuwa wote na mawazo ya kitoto...kila mmoja atakuwa anajiona anajua zaidi ya mwingine. Na kwamba kuwa katika mahusiano,ambayo mwanamke kapitwa miaka kuanzia mitano ndo yenyewe....Kwa mtazamo wangu tabia ni hulka tu ya mtu kutokana na mazingira aliyokulia au yanayomzunguka...Suala la mapenzi ya "age mates" mwalionajee wana JF?
 
mapenzi na umri haviingilini kabisa!! mapenzi yanatoka moyoni na moyo haujui namba.
 
Ukitaka kataa, lakini ukweli ni kuwa mnapokuwa rika moja ni vigumu sana kuheshimiana. I won't rule out rare cases ambapo mahusiano ya agemates yamefanikiwa but the majority ni ngumu. Unajua kwenye mahusiano lazima awepo mmoja wa kujishusha na hii inakua tatizo kwa wanaolingana umri. I have personally experienced that..
 
Umri ni namba tu,km mmependana kwa thati wala haina tatizo,
Tatizo litakuja km mtaacha kufuata mioyo yenu na kusikiliza watu wa nje wanasemaje na kutaka kuwaridhisha!!
 
Tatizo ni kwamba inaaminika kwamba jinsia moja hua inamature kaikili/kimawazo/kifikra haraka zaidi ya nyingine. Hivyo ukitaka mahusiano ambayo wote mtakua kwenye level moja ya kufikiri inabidi uwe na mwanaume ambae amekuzidi kidogo (normally) japo bado unaweza ukakutana na mtoto kwenye mwili wa mtu mzima. Ila bado wapo wanaomature haraka bila kujali jinsia na umri hivyo we unachotakiwa kufanya (kama maturity ni muhimu kwako) mchunguze mtu yeye kama yeye bila kujali jinsia.
 
mmmhhh Canta,hebu linganisha kavulana ka 18years old na binti wa umri huo,mentally unawaonaje?
 
umri ni namba tu,km mmependana kwa thati wala haina tatizo,
tatizo litakuja km mtaacha kufuata mioyo yenu na kusikiliza watu wa nje wanasemaje na kutaka kuwaridhisha!!
kuna siku mtakuja kujua umri ni umri na namba ni namba hayo nimaneno ya kujipa moyo tuu!
 
arghhhh...wee mama olewa tuu na huyo serengeti boy wako ili kesho awe mariooo umlee kisha akutende akatembee na dogodogo kwa kutumia maslahi na juhudi zako za kumwezesha...true dat
 
Umri ni namba tu,km mmependana kwa thati wala haina tatizo,
Tatizo litakuja km mtaacha kufuata mioyo yenu na kusikiliza watu wa nje wanasemaje na kutaka kuwaridhisha!!

Tatizo ni kwamba inaaminika kwamba jinsia moja hua inamature kaikili/kimawazo/kifikra haraka zaidi ya nyingine. Hivyo ukitaka mahusiano ambayo wote mtakua kwenye level moja ya kufikiri inabidi uwe na mwanaume ambae amekuzidi kidogo (normally) japo bado unaweza ukakutana na mtoto kwenye mwili wa mtu mzima. Ila bado wapo wanaomature haraka bila kujali jinsia na umri hivyo we unachotakiwa kufanya (kama maturity ni muhimu kwako) mchunguze mtu yeye kama yeye bila kujali jinsia.
Mimi na mama Matesha wangu tumelingana umri. Na hatujawahi kujutia penzi letu.

Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele.
 
mmmhhh Canta,hebu linganisha kavulana ka 18years old na binti wa umri huo,mentally unawaonaje?
Kwenye mapenzi kila kitu kinawezekana Mzee bishanga,
Mbona wapo wanaume na umri mkubwa tu still wanaongozwa na wanawake wadogo kiumri,
Utashi wa mtu hauhusiani na miaka au umri!!!
Km upendo ni lzm heshima itakuwepo,masikilizano na ushirikiano ktk kila jambo.
 
Mimi na mama Matesha wangu tumelingana umri. Na hatujawahi kujutia penzi letu.

Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele.
Shikamoo Babu,
Nimefurahi kwa vile umekubali, km mapenzi yapo wala mambo ya umri hayana nafasi kbs!
 
kuna siku mtakuja kujua umri ni umri na namba ni namba hayo nimaneno ya kujipa moyo tuu!
Hapa cha msingi ni mapenzi hizo namba wala sio ishu,mambo yameshabadilika,
Ndio maana kuna wale wanaoitwa "WATU WAZIMA HOVYO"
Ndio ukweli huo hakuna cha kujipa moyo wala nn hapo!!
 
Shikamoo Babu,
Nimefurahi kwa vile umekubali, km mapenzi yapo wala mambo ya umri hayana nafasi kbs!
Tena FYI mkilingana ndio inanoga zaidi......
Siyo mmoja anataka kwenda bongo fleva mwingine anataka kwenda Kitambaa cheupe
Mwingine anazungumzia TANU mwingine anajua CCM
Huyu anajua ya Nyerere mwingine January Makamba
Huyu anataka kupumzika mwingine anataka kwenda disko
Basi tabu tupu!

Baada ya kusema hayo, naitikia shkamoo yako.
Afu unajua navyokupenda?
 
Ndio maana na mie nakupenda babu,
Japo sijui kiwango chako cha kunipenda kimeongezeka au nikile kile!
Kiukweli linapokuja swala la watu kupendana kwa dhati km Babu ODM na bibi yetu MATESHA,
Umri munabaki kuwa namba tu,ndio maana some time babu anaendaga sokoni na kumsaidia bibi kupika lol!
 
Tena FYI mkilingana ndio inanoga zaidi......
Siyo mmoja anataka kwenda bongo fleva mwingine anataka kwenda Kitambaa cheupe
Mwingine anazungumzia TANU mwingine anajua CCM
Huyu anajua ya Nyerere mwingine January Makamba
Huyu anataka kupumzika mwingine anataka kwenda disko
Basi tabu tupu!

Baada ya kusema hayo, naitikia shkamoo yako.
Afu unajua navyokupenda?

Mbona hata wenye umri sawa wanaweza wakawa na interest tofauti kabisa?Sema ubahatike kumpata yule mnaelingana hata kifikra na sio kiumri tu maana sio kigezo cha kutosha kuwaweka kwenye ukurasa mmoja.
 
Mjazeni kiburi aolewe na kiserengeti, sasa hivi atakuja hapa na Phd bila kiungia darasani.

Back
Top Bottom