El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 263
- 502
Sijui kama ni shida ninayoiona Mimi tu au na wenzangu mnaiona pia shida hii.
Mara kadhaa Sasa utawasikia watu na hasa viongozi, Kila wanapomtaja Rais lazima wamalizie na jina lake lote, Dr. Samia suluhu Hassan.
Utamsikia kwa mfano waziri anaeleza jambo " mheshimiwa Rais, Dkt. Samia suluhu Hassan alinituma hivi majuzi kwenda New York.
Kwangu Mimi ingependeza kama angesema" Mheshimiwa Rais alinituma kwenda New York.
Ukishasema Mheshiwa Rais, definitely inajulikana ni Dkt. Samia suluhu Hassan.
Kwingine inazidi kabisa" Namuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia suluhu Hassan anaingia hapa"
Hivi ukishasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaingia hapa, haitoshi mpaka utaje jina lake? Kwani Kuna Rais mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asiye Dkt. Samia Suluhu Hassan?
Kwangu Mimi dhana hii ya utajaji jina la Rais Kila mahali, hata ambapo cheo chake kimeshatajwa Ina dhana mbili kuu,
1) Hivi si kujipendekeza kwa watamkaji wa jina la Rais Kila mara kana kwamba huwa Kuna Rais mwingine tena wakati huohuo?
Maana nijuavyo, neno Rais linamhusu hasa aliyeko madarakani. Tukitaka kusema Rais mwingine aliye wahi kuwa, tutatumia maneno kama" Rais mstaafu" wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Dhana nyingine ninayoipata, ni taswira ya hofu "( inferiority complex")
Kutaja jina la Rais Kila wakati hata pale ambapo cheo chake kimeshatajwa, kwangu Mimi naona ni hofu( ya kupandiwa ?) yenye lengo la kuonyesha kwamba huyu ndiye.
Sasa jambo la kujiuliza ni, kwani Kuna mshindani Tena ndani ya urais? Kuna anayempinga Rais mpaka atambulishwe kwa jina Kila wakati kama kwamba asipotajwa jina atapoteza cheo chake?
Je kutajataja jina la Rais hata baada ya kumtambulisha kwa cheo chake, ni njia ya wakereketwa kuwaonyesha wale walioutaka urais wakati Fulani kwamba Sasa huyu ndiye?
Nakubali kweli kwamba Kuna wakati wa kumtambulisha Rais na jina lake lifuate katika nyakati kadhaa lakini haiwezi kuwa Kila wakati kama ninavyoona siku hizi.
Lakini ninaloliona hapa kwetu ni ajabu kiasi. Mtu hawezi tu kusema Rais, Tena Rais wetu tunayemfahamu wote kwa jina, ajabu lazima ataje jina lake kana kwamba anamtambukisha Rais wa Jamhuri nyingine.
Mantiki ya andiko langu ni kufanya mambo sahihi kwa njia sahihi.
Doing the right things, the right way!