Kwangu mimi ilikuwa ni kama ndoto……………………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwangu mimi ilikuwa ni kama ndoto……………………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 13, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hadi leo naona kama ndoto.............!
  (Picha haihusiani na habari hii.)


  Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1991 wakati huo nikiwa nafanya kazi kwa mtu binafsi, Muasia mmoja. Nakumbuka katika mojawapo ya majukumu yangu, nililazimika kwenda Nairobi nchini Kenya.
  Nilikwenda huko kikazi na nililazimika kukaa kwa mwezi mmoja. Nilipomaliza kazi ile, niliamua kukaa kama siku tatu zaidi ili kujionea hali ya Kenya ilivyo. Nilizunguka jijini Nairobi na kwenda maeneo ya karibu kama vile Thika, Kinangop na miji mingine iliyo karibu na jiji hilo maarufu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

  Siku moja wakati natoka kwenye matembezi yangu nje ya jiji hilo la Nairobi, nilikutana na mtu mmoja. Huyu bwana alikuwa anaonekana kuchoka sana, ama kwa kuumwa au kwa njaa. Nilikaa naye kiti kimoja kwenye Matatu, yaani daladala za Kenya. Huyu bwana alikuwa ananitazama mara kwa mara na kujitahidi kutaka kama kutabasamu, ingawa hakumudu sana.

  Niliingiwa na huruma na kulazimika kumuuliza kama alikuwa yu mzima wa afya. Alisema anaumwa na hana hata senti tano ya kulipia matibabu yake. Nilimuuliza kama anao ndugu. Alisema hana na familia yake iko mashambani, ambapo haina kitu kabisa. "Nina watoto watatu mmoja amemaliza shule hana kazi na wawili wanasoma, lakini ni kwa mashaka sana, kwani mara nyingi hurudishwa nyumbani kutokana na kukosekana ada." Aliniambia.

  Ilibidi nimchukue yule bwana hadi hospitalini ambapo alichukuliwa vipimo. Aliambiwa arudi kesho yake kuchukua majibu yake. Tuliagana tukutane pale hospitalini kesho yake. Kwa kweli hakuamini kwamba, nilimfikisha hospitalini na kumlipia matibabu. Hakuweza hata kushukuru na nilielewa ni kwa sababu gani. Mshangao ulikuwa ni mkubwa sana kwa upande wake.

  Kesho yake alipata majibu yake ambayo yalionyesha kwamba alikuwa na maji kwenye pafu moja pamoja na kifua kikuu. Ilibidi aandikiwe dawa. Hakuwa na fedha kabisa. Ilibidi nitoe fedha zote za matibabu yake. Ilikuwa kama silimia 20 ya pesa zote nilizozipata pale Nairobi kama posho. Lakini hiyo haikunisumbua. Nilikuwa najisikia vizuri kuona angeweza kupona.

  Ilibidi niombe ruhusa ya siku saba zaidi ili nikae Nairobi kukagua hali ya yule jamaa. Wakati huo huo nilimwambia kwamba, kama anaweza kumwita mkewe akae naye pale mjini wakati anatibiwa ingekuwa vizuri. Nilimwambia ningemsaidia pesa kidogo za kumwezesha mkewe kukaa naye angalau kwa siku kadhaa. Alikubali na kumwita mkewe. Mkewe alipofika hakuamini kwamba niliweza kumsaidia mumewe vile. Yule mama alilia sana na aliniombea sana kwa kikwao, yaani Kikikuyu kwa majina ya mizimu yote. Nilijisikia furaha kwa namna mke wa jamaa alivyojisikia vizuri kuona mumewe amepata matibabu.

  Niliondoka Nairobi siku ya tatu tangu mkewe kuja. Niliwaachia hela kiasi cha shilingi 14,000 za Kenya, ambazo nilimwambia yule mama zingemsaidia kufanyia shughuli yoyote ambayo ageona inafaa. Niliondoka bila hata kuwaachia anuani yangu wala simu yangu. Labda wao walitegemea ningewapa anuani yangu, lakini sikufanya hivyo. Mimi sikuona sababu ya kuwapa kwani, niliwasaidia kama binadamu ambao wanahitaji msaada wangu, siyo ili wanijue au tuwe marafiki.

  Hivyo ndivyo nilivyo hata leo. Sijisifu kwa sababu sioni kuwa ni sifa, bali naona kila binadamu angetakiwa kuwa hivyo, ila basi tunazuiwa na choyo ya kufundishwa. Sikuwahi kusoma kuhusu masuala ya kusaidia na kupata furaha wala kumsikia mtu. Tabia hii nilitoka nayo kwetu, niliitoa kwa baba yangu ambaye, alikuwa mtu wa kusaidia sana bila kujali malipo. Hilo nalijua.

  Mambo yangu yalienda vizuri hadi mwaka 1994. Mwaka huo nilipoteza kibarua change na hata shughuli zangu zikawa zimepoteza umaarufu kutokana na mabadiliko ya teknolojia. Ilibidi nianze kuhangaika. Kufikia mwaka 1996, nilikuwa hoi bin taabani kiuchumi. Watoto wangu watatu wakawa hawaendi tena shule, hakuna ada. Tulishindwa kulipa kodi ya nyumba, ambapo ilibidi tufukuzwe na kwenda kuishi kwa ndugu wa mke wangu. Huyu naye hatukukaa hata mwezi masimango yakaanza. Siwezi kumlaumu, kwani kusaidia siyo jambo rahisi, ingawa naamini ndipo mahali furaha ya binadamu ilipo.

  Tulilazimika kuhama na kwenda kuishi Mtoni Kijichi. Huko hatukuwa tumepanga. Jamaa yangu mmoja alikuwa anajenga kule na alikuwa anataka mlinzi, ambapo nilimwambia ningefanya kazi hiyo. Hivyo tukawa tunaishi kwenye kibanda cha mtumishi. Lakini tulihisi nafuu. Hata hivyo watoto wote walisimama shule, kwani hata nauli ya kuwapa ili waende shule ilikuwa ni vigumu.

  Mwaka huo huo wa 1996 mwezi Novemba likazuka tatizo lingine. Mke wangu alianza kuumwa. Ilikuwa kama ghafla tu, alianza kulalamika tumbo na akaanza kuwa anatoka majimaji sehemu za siri. Nilijitahidi kumtafutia dawa za miti shamba kwa wenyeji bila mafanikiao. Jirani yangu mmoja aliona hali inazidi kuwa ngumu na alijua tatizo langu ni ukata. Huyu alijitolea kunipa 3,000 nilimpeleka mke wangu hospitalini. Nilimpeleka pale Temeke ambapo nao walisema labda nimpeleke Ocean Road, kwani wana wasiwasi kwamba, huenda alikuwa na kansa.

  Nilimpeleka Ocean Road na matokeo yakawa ya kuumiza kuliko maradhi yenyewe. Ni kweli alikuwa na kansa, tena ilikuwa imefikia hatua ya nne. Kwenye hatua kama hii, kupona ni miujiza. Ilibidi aanze huduma ya matibabu palepale. Alipomaliza huduma ya matibabu hakuchukua miezi mitatu akafariki. Lazima niseme kweli kwamba, nilipoteza sehemu yangu kwa kumpoteza mke wangu.

  Tunaambiwa kila mtu ni kamili kama alivyo, lakini kuna wakati tunaweza kumpoteza mtu, tukahisi kama nasi wenyewe tumepotea nusu. Msiba huu ulikuwa mkubwa kwa namna mbalimbali, kwani hata mazishi yenyewe yalikuwa na kero zake. Kutokana na ugeni pale Kijichi, ilionekana hakuna aliyekuwa akitujua na ilionekana kwa maana hiyo kwamba, hatuhudhurii mazishi. Kwa hiyo waliohudhuria mazishi ya mke wangu walikuwa ni watu wachache sana.

  Lakini tulizika na mambo yakaisha. Nilibaki na wanangu watatu ambao nao hawakuwa na mwelekeo. Mmoja alikuwa amekomea darasa la sita, mwingine la nne na wa mwisho wa kike darasa la pili. Huyu ndiye aliniumiza sana, kwani alikuwa karibu sana na mama yake. Mambo hayakubadilika na katika kujihami na shinikizola ukata nililazimika kuanza kunywa pombe. Nilitaka kupoteza mawazo, kwani sikuwa namudu tena kuishi nikiwa mzima wa akili. Nadhani ndilo kosa ambalo wengi huwa tunalifanya tunapokabiliwa na matatizo.

  Mwaka 1998 nilikuwa na watoto wawili pale nyumbani. Yule mkubwa wa kiume alihama nyumbani na nikasikia kwamba anafanya kibarua cha kupiga debe. Sikujali kuhusu taarifa hiyo. Yule wa pili alikuwa tu nyumbani akiishi kwa kufanya vibarua vya kubeba mchanga au vya aina nyingine. Yule mdogo wa kike, alikuwa anasoma kwa msaada wa jirani ambaye alitokea tu kumpenda, kwani alikuwa ameelewana sana na marehemu mke wangu, wakati tuliphamia pale. Hiyo pia haikunisumbua na wala sikwenda hata kumshukuru.

  Septemba mwaka 1998, nikiwa ninatoka kwenye ‘kubangaiza' mjini nilipita eneo la karibu na Hoteli ya Peacock. Wakati napita jamaa mmoja alinismamisha na kunisalimia.
  Huyu jamaa tulikuwa naye zamani kwenye ile kampuni ya Waasia. Tulisalimiana na alinipa pole ya msiba wa mke wangu. Halafu tulianza kujadili kuhusu maisha kwa ujumla.

  Wakati tukiwa tunaongea, alitokea jamaa mmoja na kusimama akitutazama. Huyu jamaa alikuwa mnene, mrefu na mwenye rangi ya maji ya kunde. Sikuwa namjua na nilihisi alikuwa anajuana na mwenzangu, hivyo alikuwa anasubiri tumalize kuzungumza ili wazungumze. Hivyo ilibidi nimuage yule jamaa ili niwape nafasi.
  Wakati najiandaa kuondoka, yule mtu aliniita kwa jina langu. "Nadhani ni wewe bila shaka, kama siyo wewe utanisamehe." Alisema.

  Nikiwa nimeshikwa na butwaa nilimjibu. "Ni mimi, samahani, nimekusahau kidogo, labda unikumbushe." Halafu lilikuja jambo ambalo hata kama ingekuwa ni wewe usingelitarajia. "Tulikutana Nairobi, ulinisaidia, uliokoa maisha yangu……." Kuna wakati mtu unapata mshangao ambao unakuwa kama vile ni maumivu yasiyovumilika. Ndivyo ilivyokuwa kwangu. Nilitulia kwa muda mrefu sana, kabla sijasema, "nakukumbuka, nakukumbuka sasa vizuri."

  Unaweza ukadhani najua kujifaragua, lakini hapana. Ninapomsaidia mtu huwa nimemsaidia na tumemalizana, sihitaji kumjua tena kama siyo lazima. Kwa hiyo hata huyu bwana sikuweza kumkumbuka kirahisi. Mabadiliko ya mwili aliyokuwa nayo, pia yasingeniwezesha kumkumbuka hata kama ingekuwaje. Aliniambia kuwa anakuja hapa nchini kibiashara na amekuwa akitamani kuniona. "Nikija Dar huwa natembea sana kujaribu kukutafuta. Niliuliza ile kampuni uliyosema unafanya nikaambiwa uliondoka." Aliniambia na kuniomba twende chumbani kwake pale Hotelini.

  Alikuwa amefurahi zaidi kuniona mimi bila shaka, na alianza kunisimulia kuhusu namna mkewe alivyoweza kufanya biashara kwa zile fedha nilizompa na yeye kuungana naye baada ya kupona. "Tuliweza kufanya kitu kikubwa sana. Fedha zako zilikuwa na baraka na kuna wakati tulikuwa tunaambiana na mke wangu kwamba, hatuwezi kukuona kwani tuliamini wewe ni malaika kiongozi (Guardian Angel)." Alisema. Ulipokuja upande wangu kusimilia maswahibu yangu, yule bwana furaha yote ilimwishia na alilia kwa muda mefu sana. Baadaye aliingia bafuni na alimpigia mkewe simu kumweleza hali yangu.

  Alikuwa anazungumza kwa Kikikuyu, lakini kwa sababu ni kibantu niliweza kuokota maneno mawili-matatu. Halafu aliniomba kama ningeweza kufuatana naye kwenda Nairobi kesho yake. Nilimkubali. Tulikula chakula cha mchana pamoja huku akinisifu kwa namna nilivyo na ukarimu. Tumbo langu bila shaka lilipata mshangao, kwani kwa miaka mingi nilikuwa sijala chakula cha utulivu.

  Niliagana naye huku akiniachia shilingi 50,000. Ilikuwa kama vile nimepata shilingi milioni tano. Jioni ile nilikwenda kwa yule jirani yetu anayemsomesha mwanangu, ambapo nilimpa shilingi 20,000 na kumwomba radhi kwa kutoona anachofanya. Halafu nilimwita mwanangu mwingine na kumwambia asikate tamaa, kwani mambo yatakuja kubadilika. Huyu nilimpa shilingi 10,000 na kumwomba aache kwa muda kufanya vibarua.

  Kwa mara ya kwanza tangu kufiwa nilitembelea kaburi la mke wangu. Nililia sana hapo kaburini kwa kushindwa wajibu wangu kama baba. Nilirejea nyumbani na kulala baada ya kuandaa nguo ambazo ningesafiri nazo.

  Naona nisiwachoshe kwa kuwasimulia kila kitu. Ni kwamba, nilifika Nairobi na kushangaa kukuta yule jamaa yangu akiwa na biashara kubwa ya jumla ya vifaa mbalimbali.

  Alikuwa akinunua vifaa mbalimbali ambavyo kwa Kenya ni adimu, na ambavyo vinapatikana Tanzania. Ilikuwa ni biashara kubwa. Nilipokewa vizuri kiasi kwamba, niliona kama sistahili. Nilitambulishwa kwa kila ndugu na jamaa wa familia ile kwamba, mimi ndiye niliyewapa mtaji wa biashara. Hawakuficha wala kuona aibu. Walikuwa ni watu wanaojiamini. Hao jamaa na ndugu zao walinitazama kwa woga mkubwa wakijua kwamba, mimi ni tajiri wa ajabu.

  Nilikaa Nairobi kwa wiki moja. Unajua walifanya nini watu wale? Walinipa shilingi 300,000 za Kenya ambazo zilikuwa kama shilingi milioni 3.5 za hapa kwetu kwaq wakati ule. Waliniambia hawana njia nyingine ya kuonyesha shukurani yao kwangu kwani hicho walichonipa ni kidogo sana. Kwangu ilikuwa kama ndoto.
  Nilirudi Dar nikiwa mtu tofauti kabisa. Yule bwana na mkewe walinipa uwakala wa kuwapelekea bidhaa kule Nairobi, badala ya yule jamaa kuja kila wakati. Shughuli hiyo nilimpa mwanangu mkubwa ambaye nilimsaka na kumpata baada ya kurejea.

  Hakuwa anataka kusoma hivyo niliona nimpe yeye biashara ile. Nashukuru hakuwa ameingia ulevini wala kwenye kuvuta bangi na alikuwa amefungua akaunti benki ya posta, jambo ambalo lilinionyesha kwamba, alikuwa na ufahamu mkubwa.

  Hadi leo anafanya biashara za Nairobi-Kampala-Dar es Salaam. Ile familia imekuwa ni ndugu zetu. Watoto wangu wale wawili waliendelelea na elimu hadi elimu ya juu na sasa wamemudu kusimama wenyewe. Miaka miwili baadae tangu niliporudi kutoka Nairobi nilioa na sasa nimepanuka kibiashara, nikiwa nimejikita katika maeneo ya Manzese, Magomeni na Kinondoni B.

  Usione mtu ana biashara fulani au mafanikio fulani ukadhani yalikuja tu, kuna habari pana nyuma yake wakati mwingine.

  Kuna jambo naomba sana nikusaidie kulifahamu. Hili ni jambo ambalo linaonekana halina maana, lakini ndio ubinadamu wenyewe. Jitahidi sana popote ulipo kuwasaidia watu, bila kujali kama watakukumbuka au kukulipa ama hapana.
   
 2. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kweli ni somo kubwa sana,hii imenifanya mpaka nikatoa chozi.
   
 3. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mh...Ha...!
  Nimesisimka Kiasi Hata Cha Kuongezea Sina Zaid Ya Kusema NIMESISIMKA!
   
 4. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  1. Posho ya safari, mshahara na marupurupu toka kwq mwajiri wako yaani yule muasia inaonekana kuwa ilikuwa kubwa kiasi cha wewe kuweza kuweka akiba au kuiwekeza katika maeneo mengine. Hii inathibitishwa na kiasi kikubwa cha fedha ulichokitumia katika matibabu ya mtu mgonjwa ulokutana naye Nairobi pamoja na kiasi kikubwa cha fedha - 14,000 za kikenya ulizomuachia na ambazo bila ya kuwa na ufahamu ndizo baadaye zilisababisha kubadilisha kabisa maisha yako.

  2. Kutotoa shukrani baada ya kupewa msaada ni tabia ya mtu ila asilimia kubwa ya ndugu zetu wakenya ndivyo walivyo. Akija mkenya katika duka lako badala ya kuulizia kwa lugha ya kawaida bidhaa anayoihitaji atakuambiaa nipe au lete hiyo ................ Utakapokwenda mahali popote ambapo wewe ni mgeni jaribu kusoma sana hulka na tabia za wenyeji wa maeneo hayo.

  3. Kutoa ni moyo na wala si utajiri. Hili lilikusaidia sana kwani pamoja na kuwa wewe ulikuwa ni mtu wa kutumwa na mabosi wako bado ulikuwa na moyo wa kuwasaidia wenye uhitaji. Yatupasa leo hii, na hasa nafasi yako inapokuruhusu kufanya hivyo kutoa msaada kwa wale wenye uhitaji. Msaada utakaoutoa usiwe wenye masharti kwani hata waswahili wanasema tenda wema nenda zako usingoje shukrani. Malipo ya wema wako anayajua Muumba. Nadhani msaada ulioutoa kwa mwenye uhitaji kule Nairobi ulikupa malipo yake kupitia kwa Mungu.

  4. Ukipata second chance in life itumike vizuri ipasavyo. Hii haijalishi nafasi hiyo imepatikana kwa sula gani; liwe la kisiasa, kijamii au kiutamaduni. Linapotokea sula la ugumu wa kimasiha na baadaye ukanyookewa, makosa yalofanyika hapo awali yawe ni funzo kwa ajili ya kumaintain mafanikio utakayoyapata kama ulivyofanya wewe.

  5. Shukrani kwa mafanikio ya kibinadamu. Ukumbuke sana kuwasaidia wenye uhitaji na bila ya kujali mafanikio yako umeyapata kupitia mazingira gani cha msingi yawe ni halali tu. Maduka uliyoyaanzisha ktaika maeneo uliyotaja waweza kutoa malipo ya mafanikio yake kwa walau kutoa ajira kwa wenye uhitaji na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.


  The listener - Ex Detective
   
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nice story
  Kweli bwana wema hauozi!
   
 6. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mtambuzi umeniliza jamani daaah.............maisha ni kujifunza,asante sana. Kweli unaweza kujiona wewe una matatizo lakini ukisikia ya mwenzako unabaki kujiuliza hivi kweli haya yangu ni matatizo au namkufuru Mungu tu kwa kulalamika.

  Ubarikiwe kaka yangu endelea kutuletea mafundisho.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Story nzuri....naomba tu ubadilishe ending, naona inajirudia rudia. Nakumbuka story ya mwizi na ile ya kaka mpiga picha.
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Asante Mtambuzi , Makala yako ina mafunzo muhimu na mazuri sana hasa sentensi ya mwisho. Hakika nitaendelea kuifanyia kazi.
  Swali la kizushi: Sasa hapa ukimsaidia mtu haupaswi kuchukua contacts zake? Maana hii stori inaonyesha kama jamaa angewaachia contact wale rafiki zake huenda wangemtafuta mapema na mambo mengi mabaya yasingeweza kumkuta!
   
 9. salito

  salito JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Duh,asante kiongozi kwa kunipa hii elimu.
   
 10. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Imenigusa sana
   
 11. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Da hadi machozi yamenitoka sicerely hata me nikimsadia mtu huwa sitaki hata ajue natokea wapi
   
 12. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  ama kweli wema haufilisiki.
   
 13. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  ..................................................................................................................................Toka siku hiyo wanavijiji wa pande mbili za vijiji hivyo wakaishi maisha mazuri na ya amani kiasi hata cha kuvunja ule mwiko wa kijana wa kijiji kimoja kumuoa binti wa kiji kingine. MadameX nadhani huu ni mwisho mzuri wa stori. Sasa kazi ni kuwa na story yenyewe. Imenikumbusha wakati niko kidato cha pili na ilikuwa ni mtihani wa Taifa.

  The Listener - Ex Detective
   
 14. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Thanx Mtambuzi, vipi Ununio utarudi tena?
  Kwa kweli mungu ni mwema na mwaminifu hamtupi mja wake.
  Tenda wema utalipwa na mungu,,
  Kinachonifurahisha sana wa TZ waliowengi ni wema sana na wanahuruma sana
  mungu azidi kutupa huu moyo !
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  veeeeri tachingi
   
 16. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Dah! Inspirational and touching story....
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. peri

  peri JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mtambuzi umetupa shule ya nguvu, kweli Mungu hamtupi mja wake.
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Wana kuambia Tenda wema uende zako, Mpende Jirani yako kama ujipendavyo wewe
   
 20. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  maisha ni safari yenye majaribu mengi,tunapanda milima na kushuka,hiyo lazima kila binadam apitie ili kuweza kuwa mkamilifu,kumbuka hata Yesu alisulubiwa msalabani na kufa ili aweze kutimiza process nzima ya maisha ya binadam,nafikiri maisha uliyopitia yamekufanya uwe smart na mwangalifu zaidi na umekomaa zaidi
   
Loading...