Kwamba zoezi la kuitafuta ndege iliyopotea pori la akiba Selous limesitishwa

Nimesoma mahali kuwa lile zoezi la kuitafuta ndege ndogo iliyopotea ikiwa na rubani mmoja limesitishwa baada ya wiki kadhaa za kuitafuta.

Njia zilizo tumika kuitafuta na kushindwa kubaini hata mabaki ya ndege hiyo kama haikuvuka mpaka wa JMT pia hazijawekwa wazi.

Inashangaza kuona wakati huu ambapo usafiri wa anga hapa Tanzania unaongezeka kutokana na kuwepo vyombo vingi vya usafiri, tunashuhudia ndege ikipotea kwenye rada za anga hii na isiache hata alama. Kama ndege hiyo ilipaa kwenda juu, Kuna mahali ilitua au kuanguka.

Nadiriki kusema na kuinyoshea mamlaka yetu ya anga kwa kushindwa kufuatilia kwa umakini vyombo virukavyo angani maana wanalipwa kwa ajili hiyo. Kama ni ndege ndogo iliyopotea na sio kishada kilichopotea TCAA waje na majibu kwenye hili mapema kabla hatujasikia kupotea kwa Airbus ikiwa na abiria 150.

====

NDEGE NDOGO YAPOTEA KATIKA PORI LA SELOUS TUNDURU RUVUMA IKIWA NA RUBANI .

October 30, 2021

Na Amon Mtega Tunduru.

NDEGE ndogo aina ya BatHawak yenye no za usajiri 5H-WXO inayomilikiwa na shirika lisilo la kiserikali la uhifadhi linalojulikana kwa jina la Protected Areas Management Solution Foundation (PAMS) imepotea wakati ikielekea kwenye pori la akiba Selous kanda ya Kingupila.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julias Mtatilo alisema kuwa ndege hiyo aina ya BatHawak inayorushwa na rubani Samweli Balina Gibuy imepotea Oktoba 18 mwaka huu majira ya saa 9.:09 jioni ikiwa inaelekea Pori la akiba la Selous.

Amesema kuwa ndege hiyo ambayo iliombwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyama Pori Tanzania -TAWA kupitia shirika la uhifadhi la Frankfurt Zoologocal Society (FZS)kwa lengo la kwenda kusaidia katika zoezi linaloendelea la utafutaji wa Faru weusi katika pori la akiba la Selous.

"Muda mfupi baada ya kuruka ndege inadaiwa ilionekana na wachimbaji wa madini eneo la matuli na baadae wananchi wa Kijiji cha Kajima kilichopo katika Kata ya Jakika Tarafa ya Matemanga wilayani Tunduru ikielekea uelekeo wa Mashariki mwa Kijiji cha Kajima ambacho kinakadiliwa kuwa na umbali wa kilomita 26 kutoka uwanja wa ndege wa Matemanga ambapo ndege hiyo iliruka wakati wa kuondoka" amesema Mkuu huyo wa Wilaya Mtatilo.

Ameeleza kuwa ndege hiyo ilitarajiwa kutuwa kingupira majira ya saa 11:30 alasili hadi 12:09 jioni ambapo kwa bahati mbaya haikufika kingupira kama ilivyotarajiwa na ndipo mawasiliano ya kuulizia kwa pande zote mbili ilikotoka na inako kwenda yalianza.

Mtatilo amesema kuwa baada ya kujiridhisha kuwa ndege hiyo haikufika Kingupira na wala haijaonekana kwenye uwanja wa ndege wa Matemanga ambapo ndiko kuna ofisi za PAMS Foundation wafanyakazi wenzake Rubani Samwel walimjulisha Mkurugenzi wa shirika hilo ambaye mara baada ya kufahamishwa aliangalia kwenye "Spider track" ya ndege hiyo yenye uwezo wa kuonesha alikopita na ilipo ndege hiyo na kwamba Spider track ilionesha kuwa ndege hiyo ilikuwa uwanjani majira ya saa 7 mchana ambapo muda huo alikuwa anafanya majaribio kabla ya safari kuanza na baada ya kuruka akielekea Kingupira Pori la Akiba la Selous spider track haikuoneaha chochote.

Aidha amesema kuwa taarifa zilitolewa katika ngazi za mamlaka mbalimbali huku maandalizi ya utafutaji na uokozi yikiendelea ambapo kazi hiyo imefanyika kwa siku tano kwa kutumia jumla ya ndege tano Kati ya hizo nne za mabawa na moja ni helicopter wameamua kusimamia zoezi hilo na kuwaomba wananchi na vyanzo vingine kuendelea kutafuta ndege hiyo na kwamba zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye fanikiwa kutoa taarifa ya ndege hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Familia ya Rubani Samweli Balina Gibuyi, kaka wa Rubani huyo Jani Killa amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa sana kupotea kwa ndugu yao lakini kwa kushirikiana na shirika la PAMS na Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama wanahakikisha wanampata ndugu yao lakini pia kupatikana na ndege aliyokuwa anaitumia.

Kwa upande wake mratibu wa mradi wa uhifadhi wa Tembo Ruvuma kwenye shirika la PAMS Foundation Osca Bakumbezi amesema kuwa tukio hilo la simanzi kwa sababu kwanza Rubani wao walikuwa wanafanyanae kazi muda wote na wameshirikiana nae kwenye kazi nyingi na kwamba hata kazi aliyokuwa anaenda kuifanya ni kazi ambayo ilikuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na si vinginevyo.

Mwisho.
Mtaalamu mbobezi wa aviation brazaj atasema this kind of shit only happens in Tanzania, na rubani kaangamia sababu ya ujinga wake kama Waafrika ote walivyo.
 
Lissu alikuwa anaambiwa hali hewa siyo nzuri.Anga limechafuka kupiga kampeni.
Huyu hawakuona haja kumjulisha anga limechafuka?
 
Kwani wenyewe wakina faru John wanaswmaje?
 
Nimekuja mbio nikidhani Malaysia airlines kumbe ni single engine propeller zile za kumagilizia pembejeo kwenye mashamba makubwa ya ngano! Waende tu karatu wataikuta.

barafu
Hawa jamaa hawajui kuwa zinapotea Boeing za watu 200+ na dunia inatafuta mpaka inaacha sembuse kandege kamoja ka propeller.
Ndege haitafutwi kama uyoga. Wanaangalia trajectory yake na mara ya mwisho ilionekana wapi kisha ndio wanakadiria itakuwa imepotelea eneo gani. Wakiikosa kwenye hilo eneo wanaongeza upana wa search area, wakikosa wanaachana na utafutaji ambao ni gharama kubwa
 
Wewe tangu nimesoma uzi na nikakutana na hii reply ndio nikajua kabisa hujui kitu kuhusu usafiri wa anga. Yaani unataka satellite itafute ndege?
Soma jomba!, Soma sana uelimike!! ... Elimu huwa haina mwisho. Ndege zenye rangi ya bluu, zote ziko tracked kupitia satellite.

Screenshot 2021-11-20 at 10-22-00 Live Flight Tracker - Real-Time Flight Tracker Map Flightrad...png
 
Soma jomba!, Soma sana uelimike!! ... Elimu huwa haina mwisho. Ndege zenye rangi ya bluu, zote ziko tracked kupitia satellite.

View attachment 2017955
Satellite haitumiwi kwenye kutrack ndege iliyopotea kijana. Satellite hata hiyo simu yako inaweza track ila usitake kusema wiki hii F-35B iliyodondoka Mediterranean sea hao Royal Navy na US Navy hawana satellite mpaka wakatumia submarines kuitafuta. Usitake kusema wazungu ni wapumbavu walipotumia meli, helicopters na subs kutafuta ndege ya Malaysian Airlines iliyododoka baharini ikapotea na watu hadi leo. Kwani hawakuwa na maelfu ya satellites uko angani mpaka watumie gharama nyingi kuitafuta?

Kwa hiyo wewe unaona flight radar inatafuta ndege zilizopotea. Hiyo inasoma transponders, ndege zenyewe zikiwa hewani zinalazimisha kujionesha na ndipo flight radar inazisoma. Zikipotea hapo ni kazi ya black box kutoa signal mpaka pale battery itakapoisha charge. Na hii black box haitafutwi kwa satellites, na huyo Rwanda mnayemkuza hana hata satellite ya kuchorea ramani, achana na kutafuta ndege.

Black box ikiisha charge chance za kutafuta ndege na kuiona zinapungua mno. Ndege umeitafuta black box ikiwa on hujaipata, sembuse ikiwa imezima
 
Satellite haitukiwi kwenye kutrack ndege iliyopotea kijana. Satellite hata hiyo simu yako inaweza track ila usitake kusema wiki hii F-35B iliyodondoka Mediterranean sea hao Royal Navy na US Navy hawana satellite mpaka wakatumia submarines kuitafuta. Usitake kusema wazungu ni wapumbavu walipotumia meli, helicopters na subs kutafuta ndege ya Malaysian Airlines iliyododoka baharini ikapotea na watu hadi leo. Kwani hawakuwa na maelfu ya satellites uko angani mpaka watumie gharama nyingi kuitafuta?

Kwa hiyo wewe unaona flight radar inatafuta ndege zilizopotea. Hiyo inasoma transponders, ndege zenyewe zikiwa hewani zinalazimisha kujionesha na ndipo flight radar inazisoma. Zikipotea hapo ni kazi ya black box kutoa signal mpaka pale battery itakapoisha charge. Na hii black box haitafutwi kwa satellites, na huyo Rwanda mnayemkuza hana hata satellite ya kucholea ramani, achana na kutafuta ndege.

Black box ikiisha charge chance za kutafuta ndege na kuiona zinapungua mno. Ndege umeitafuta black box ikiwa on hujaipata, sembuse ikiwa imezima
Naona umekariri simulizi za matukio hadi nukta. Rudi kwenye hoja yangu inayohusu ndege ndogo iliyopotea yapata mwezi sasa na haijaonekana!. Nini kifanyike ?.
 
Mimi nimereply comment yako ya kwamba Rwanda wana satellite watusaidie kuitafuta ndege. Ndio nikajua kwenye habari za anga umeanza kuzijulia TBC Magufuli aliponunua zile Bombardier. Unaniita nimekariri, hata ingekuwa hivyo sio vibaya mradi niwe sahihi. Kwa hiyo unaamini satellite ya Rwanda inatafuta ndege?
 
Sijui hamuelewi kuna rubani ni mtanzania mwezetu inabidi tujue yupo wapi na anaendeleaje.?ndio maana ni muhimu kupatikana.
 
Sioni mantiki ya TBC na Magufuli kuingizwa kwenye mjadala huu kwani sio lengo la hoja. Hebu pitia hii habari, inawezekana hukuwahi kuisikia.https://Africanews.space/Rwandas-first-satellite-in-space-set-for-release-from-ISS/
 
Sijui hamuelewi kuna rubani ni mtanzania mwezetu inabidi tujue yupo wapi na anaendeleaje.?ndio maana ni muhimu kupatikana.
Hili ni suala nyeti hasa ukizingatia ugaidi unaoendelea kaskazini mwa Msumbiji kwa sasa.
 
Back
Top Bottom