Kwako Waziri wa Maji: Tatizo la maji eneo la Mwananchi jijini Mwanza

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kwanza nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo ni tunasherehekea miaka 60 ya kumbu kumbu ya uhuru wetu. Kwa masikitiko Mhe. Waziri hapa Mwanza maeneo ya Mwananchi tuna siku ya tatu hakuna tone la maji bila hata MWAUWASA kutoa taarifa.

Nimesikia likisemwa kuwa wewe ni kati ya Mawaziri wachapa kazi lakini binafsi hili sioni kama ni kweli. Umewahi kusema kuwa katika maeneo ya mijini hasa Mwanza upatikanaji wa maji ni 80% na Ziwa Victoria ni robo kilomita toka eneo la Mwananchi. Mhe. Waziri tunaomba maji ili tusherehekee miaka 60 ya uhuru kwa furaha na bashasha.
 
Jiji kama Mwanza kunakuwa na mgao wa maji, yaani kitu cha aibu sana.

Ziwa lisingekuwepo si maji yasingekuwepo kabisa.
 
Back
Top Bottom