kwako Mheshimiwa Rais na Wazir mkuu kuhusu biashara ya magogo ya transit.

Goldman

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
1,930
2,400
Mwaka jana TFS ( idara ya misitu), walikamata kontena zaidi ya 60, wakituhumu ni magogo ya tz! Mpaka sasa wameshikilia kontena zile na imethibitishwa kontena zilitoka Zambia siyo tz! Mpaka leo hawajui wafanye nini! Wawape wazambia wapige mnada? Au wapige wenyewe mnada wakati ishathibitika mzigo ni wa kutoka Zambia!
Acha hiyo kuanzia November mwaka Jana mpaka leo port charges ya yale makontena ishakuwa in tsh billions nani atalipa! Wamekaa kimya!
Wakakaa wakaja na tamko mzigo wa Zambia ukija uwe unakuja na docs za Zambia forest, wafanyabiashara wengi kutokana na bureaucratic ya docs za Zambia kuja tz wakahamia Congo DRC, wakaleta mizigo tena TFS wakasema mizigo ya DRC lazima iwe na barua ya kamishna wa DRC watu wakafanya hivyo zimekuja kontena kama mia 200!
TFS wakazuia mizigo ya DRC wanasema wafanye uchunguzi! Wakati mizigo imeidhinishwa na kamishna wa DRC.!
TFS mnakaa na kontena za watu baada ya miezi miwili mnaachia huku kuna container charges kwa mteja kila siku kama $30 pia kuna icd charges kama $40 kwa siku hiyo roughly ni kama $70 kwa siku kwa miezi miwili then mnaachia mizigo huyo mteja atakuja tena kuleta kontena bandari yetu!
Kama hamtaki wateja wa magogo kupitisha mizigo yao ya transit muwaambie kwamba tz hatupitishi mizigo ya transit ya magogo! Simple!
Halafu mnalalama kuwa bandarini mizigo imekauka kumbe ni utaratibu mbovu wa kutotoa maamuzi ya haraka. Hope somebody make a decision somewhere
 
Back
Top Bottom