kwako marehemu baba wa taifa,natumaini umepunzika kwa amani hakika nataka kukujuza maajabu mengi yaliyotokea tz toka uaage dunia;
- Kepten john komba amekuwa mbunge lakini kazi yake ni kusinzia tu bungeni
- Lowasa alipata uwaziri mkuu
- CCM imekuwa kichaka cha mafisadi
- Chama Chako kimejaa magamba tu
- Raisi wa nchi hajui kwa nini watu wake ni maskini
- Madini ambayo uligoma yasichimbwe mpaka watu wako watakapokuwa na uwezo,leo yanachimbwa na wananchi wanauwawa kwa risasi wakipinga unyonyaji lakini serikali inawaita wavamizi.
- Magari ya ikulu yanachakachuliwa mafuta
- Mafisadi wanaitwa mashujaa
- Uongozi unapatikana kwa kuwa na pesa badala ya uwezo wa mtu
- Kilimo kimekuwa ni siasa tu watu wanakufa na njaa
- Kiongozi mkuu wa nchi (mkuu wa kaya) anahubiri udini
- Semina elekezi kwa mawaziri zakutosha pamoja ya kuwa wanakutana kwenye vikao vya baraza la mawaziri
- Yusuph makamba alishika nafasi ya katibu mkuu CCM
- UVCCM sio kisima cha fikra tena imegeuka kijiwe cha kahawa
Hakika baba wa taifa maajabu mengi yametokea,haya ni baadhi tu utayapata mengi leo hii, kwa sababu toka uondoke tz ya leo sio ile ambayo uliiacha au ile ulipenda iwe,tz ya leo pengo kati ya maskini na tajiri limekuwa kubwa mnno,mpaka sasa hakuna hatua zzte madhubuti za kupunguza umaskini wa watz zaidi ya usanii,upatapo walaka huu naomba utunusuru na hili ombwe la uongozi katika tz yetu yenye neema.Mungu ibariki tz na watu wake.