Kwako marehemu baba wa taifa mwl. JK Nyerere

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
kwako marehemu baba wa taifa,natumaini umepunzika kwa amani hakika nataka kukujuza maajabu mengi yaliyotokea tz toka uaage dunia;

  1. Kepten john komba amekuwa mbunge lakini kazi yake ni kusinzia tu bungeni
  2. Lowasa alipata uwaziri mkuu
  3. CCM imekuwa kichaka cha mafisadi
  4. Chama Chako kimejaa magamba tu
  5. Raisi wa nchi hajui kwa nini watu wake ni maskini
  6. Madini ambayo uligoma yasichimbwe mpaka watu wako watakapokuwa na uwezo,leo yanachimbwa na wananchi wanauwawa kwa risasi wakipinga unyonyaji lakini serikali inawaita wavamizi.
  7. Magari ya ikulu yanachakachuliwa mafuta
  8. Mafisadi wanaitwa mashujaa
  9. Uongozi unapatikana kwa kuwa na pesa badala ya uwezo wa mtu
  10. Kilimo kimekuwa ni siasa tu watu wanakufa na njaa
  11. Kiongozi mkuu wa nchi (mkuu wa kaya) anahubiri udini
  12. Semina elekezi kwa mawaziri zakutosha pamoja ya kuwa wanakutana kwenye vikao vya baraza la mawaziri
  13. Yusuph makamba alishika nafasi ya katibu mkuu CCM
  14. UVCCM sio kisima cha fikra tena imegeuka kijiwe cha kahawa
Hakika baba wa taifa maajabu mengi yametokea,haya ni baadhi tu utayapata mengi leo hii, kwa sababu toka uondoke tz ya leo sio ile ambayo uliiacha au ile ulipenda iwe,tz ya leo pengo kati ya maskini na tajiri limekuwa kubwa mnno,mpaka sasa hakuna hatua zzte madhubuti za kupunguza umaskini wa watz zaidi ya usanii,upatapo walaka huu naomba utunusuru na hili ombwe la uongozi katika tz yetu yenye neema.Mungu ibariki tz na watu wake.
 
15. CDM ndio chama pekee kinacholeta matumaini kwa wananchi
 
Mkuu hapo namba moja umenchekesha sana!.. Hakika waraka ukimfikia baba wa Taifa, atakufa kwa mara ya pili. Tehe tehe!
 
17. Umeme unakatika katika ovyo
18. Ahadi hewa kwa mgombea wa CCM ni nyingi tu, hupaswi kuzisikia
19. Mbunge sasa anasema "jimbo lake"
20. Fedha zinachapwa kwa gharama kubwa bila sababu ya kuchapwa zingine na hatuambiwi gharama za uchapaji (ni siri?)
 
21.wabunge wanataka kufunga milango ili wapigane
22.Spika alilazimisha PINDA kupiga kura tofauti na anavotaka yeye
23.eeeeh halafu JK alisema wanaopata ukimwi na mimba ni kwa sababu ya viherehere vyao
24.Yaani JK kutwa kwenye nchi za watu hata aalikwe kwenye sherehe za jando za mtoto wa museveni anaenda..
 
Baba...TANESCO siku hizi hawafanyi kazi vizuri, wazembe!..yani kama jana huku Moshi hawakukata umeme kabisa!
 
Hii lazma wachukuliwe hatua kali!
You made my day!

hahaha..hope hawajaliona hili!
yani ts funny ati usipokatiwa umeme ndo unashangaa ati..tena wengine wanakasirika, "Mbona hawa jamaa hawajakata umeme leo?" au "Leo wamechelewa!", "Mh! mpaka saivi (6:30pm) hawajakata...lazima mtu afukuzwe kazi leo"...ndo mtaani kwetu baba!!!
 
24.Yaani JK kutwa kwenye nchi za watu hata aalikwe kwenye sherehe za jando za mtoto wa museveni anaenda..[/QUOTE]

HA HA HA HA HA
 
hahahaha....you made it man.....aliekuwa zamu alizidiwa na mninginio wa kilaji akalala siku nzima hakukumbuka hata kumwomba mwenzake akakate umeme...ikawa faidi kwa watumiaji...
Baba...TANESCO siku hizi hawafanyi kazi vizuri, wazembe!..yani kama jana huku Moshi hawakukata umeme kabisa!
 
Baba wamekueleza karibia yooote, ila wamesahau kukwambia kuwa, baadhi ya watuhumiwa wa EPA wamekula mvua tano. Wamesahau kabisa adhabu yako ya viboko 24, yaani 12 wakati anaingia ili wamsodome vizuri, na 12 wakati anatoka akamuonyeshe mkewe.
 
Back
Top Bottom