KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 35,768
- 86,453
Naona kama watu wanakuwa na mikanganyiko haswa katika siasa zetu hapa Tanzania, imekuwa sio vuta nikuvute bali ni vurumai yakufuata mtu yoyote kwasababu mbalimbali aidha, nyadhifa fedha ama kujuana!.
Hivyo binafsi nikawaza kipi ni kipimo cha kiongozi bora..?
Binafsi naweza kusema kiongozi bora ni yule anaeongoza watu kufikia malengo yao, huku akilinda nakuendeleza mazuri yaliyopo na yajayo, awe muwajibikaji,mstahimilivu na weledi wakuona mbele, maana kuwa kiongozi ni kuwa dira yakuona mbele!.
Sasa sijui kama hapa kwetu tunaangalia haya au tunachagua tu kama tunavyochambua maharage!. nafikiri kila mtu aelewe dhana ya uongozi na umuhimu wa kura yake kabla hajaamua tu kutia tiki baadae ikawa kizaizai!.
Naona kama vile watu wamepotoka hivi sasa!, wanapenda kusikiliza viongozi wakitoa umbea na vijembe wala si hoja za wapi tulipo, tunaenda wapi kivipi na kwanini...?
Nyakati za uchaguzi zimekuwa za watu kusema "twende tukapige hela!" huku ni sawa na kujichimbia shimo ukiamini ni kisima kumbe ni kaburi!.