Kwako kipenzi changu pennina.....1

Kwako kipenzi changu pennina.....1

yamoyoni mwangu

Senior Member
Joined
Oct 25, 2013
Posts
106
Reaction score
31
Ni zaidi ya miaka mitatu sasa tangu nifukuzwe kazi kwenye shirika la umeme Tanzania(TANESSCO) sina furaha kabisa maishan mwangu... mwanangu ZULFA ni mgonjwa na tiba yake inahitaji mamilion ya pesa..... mke wangu amenikimbia na kuniacha nikiwa masikini wa kutupwa....

ndugu yangu nasema heri mara mia kumwamini adui yako kuliko kumuamini mwana haramu mwanamke kama PENNINA...sisemi kuwa wanawake wote wako namna hii.. la hasha... wao wengine wana moyo wa huruma na ukarimu wa ajabu... kama alivyo mama yangu mzazi... aliyenilea kwa dhiki kubwa.. nikasoma kwa dhiki pia...nikala na kulala kwa dhiki.... nimevaa kwa dhiki.... hii ndiyo sababu ilinifanya nimwamini PENNINA na kumheshimu kama mama yangu na pia mlezi wa mwanangu ZULFA.....

PENNINA kwa nn ulimtumia mwanao uliye mzaa kwa shida tena kwa kuchanwa kisu kikali tumboni al manusura ufe kipenzi changu... ukamufanya biashara ya ngono tena ukimtafutia wateja wewe mwenyewe ukamfundisha kunywa pombe kali.. ukampeleka kumbi za starehe usiku wa manane.. ilihali unajua hajatimiza hata miaka 18.... kwa nini ulifanya haya kwa siri...? ulikuwa ukisuburi nisafiri kikazi ufanye haya...

sasa mbona umemtelekeza... umemuacha akiwa hoi bin taabani.... sasa ni teja wa madawa ya kulevya... umeshiriki kuchoropoa mimba zaidi ya moja... kwa siri kubwa hata hukuniambia ....nakuomba popote ulipo uwe hai ama umekufa unastahil adhabu ya kifo... dhambi hii itakufuaata popote uendapo... tafadhari nakuomba kama umeitubu.... jitokeze hadharani utoe ushuhuda ili liwe funzo kwa wengine..... najua siku si zangu nitakufa.... umeniua kwa gonjwa hatari a UKIMWI...ona ninavyo watesa ndugu zangu... wapoteza muda wao mwingi kunihudumia nikiwa hoi kitandani.....plzplz mdogo wangu YAMOYONI nakuomba chukua karatas hii ina ujumbe mzito usome kwa makini.... ikiwezekana wape wengine wajifuze kupitia mm... usichoke mdogo wangu... kaka yako nitakufa siku si zangu....mtunze mama yetu.... wadogo zako.... kumbuka mama ametulea kwa dhiki sana..jitahidi kuwa makini na binadamu wa leo sio wema... nakutakia kila rakheri......


Huu ndo ukawa mwisho wa kumuona kaka yangu mpendwa YOHANA JOSEPH MALOLE rest in peace brother.... wakati nachukua karatas ile sikujua kama kuna story ndefu yenye kusisimua ndani yake.... ninaomba niiweke jukwaani hapa japokuwa ni ndefu lakin ntajitahidi kwa wiki niitoe mara mbili yaani jumatano na ijumaa naomba ifahamike wazi mnamo mwaka jana 15/12/2012 familia yetu ilimupoteza kaka yetu mpendwa..... tulimpenda ila bwana alimpenda zaidi.... jitahidi kuifuatilia utajifunza mengi hasa wewe kijana.....USIKU MWEMA...tukutane jumatano...
 
Dah! mpaka hapa kuna somo, Ewe mungu ulie juu hi dunia kunasehemu imetoboka hii, na kama ni jahazii basi limeshazana kwenda mrama, liookoe..
 
Duuh pole kijana kwa mitihan ya dunia ili vijana wote tufaidi na kujifunza huu uzi, tengenezea muvi mtafute Musa Banzi akupeleke location.
 
naona kama muvi za kibongo mwanzo mzuri ila mwisho majanga ngoja nitenge macho nisubir j5 itakuwaje muvi yetu
 
naona unataka kumpiku shigongo nini kwenye utunzi kila la kheri mkuu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom