Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,742
- 25,676
Ulimkuta kwao/kwake akiwa mzima na mwenye afya tele, akiwa na mavazi na uwezo wa kujikimu shida zake kadhaa.
.
Kwa unyenyekevu na maneno matamu ukaomba kuwa nae, ukaomba mfunge ndoa/muishi pamoja, na kuijenga familia moja.
.
Sasa umeshamzoea, umeanza kuleta dharau, umeanza kumsahau, umeanza kumchukulia poa, mambo muhimu humshirikishi, akikuuliza kwanini unamwambia "KWANI HAPA HULI??? " "HUVAI "???
.
Ndugu yangu, mwanzo hukumkuta katupwa mpaka useme kauli hizo kwake, hukumkuta anasota na njaa, hukumkuta anatembea bila nguo.
.
Jeuri hiyo ya kuropoka kauli hizo unaitoa wapi??? Kwako hakufata kula, kafata upendo wa dhati, kama kula hata kwao anaweza kwenda kula.
Kwako hakufata kuvaa, kafata mtu aliyedhani atampa furaha na amani ya moyo, atakayemtibu homa yake ya mapenzi.
.
Kauli zako, jeuri yako, kejeli zako, matusi yako, nguvu yako ya kumpiga, unavitoa wapi??? Au ni hao wanawake wapembeni ndo wanakupa jeuri??? Au ni hao marafiki na ndugu zako wanakupandikiza jeuri??? Watoto wako wanajifunza nini kupitia wewe?? Unataka watoto wako wakike wajenge chuki na hofu ya kuwa na wanaume au ndoa ukubwani???
.
Bomu unalolipanda leo katika shamba la mioyo ya familia yako, utakuja kulikanyaga wewe mwenyewe.
Lakini watakuja kulikanyaga na wanaume wenzio sababu ya chuki ya kijinsia uliyoijenga ndani ya mkeo, na wanao wakike.
.
Laana zako, zikurudie mwenyewe, sisi wengine tunazikataa kwa uweza wake Mwenyezi Mungu.
AMEN.