Chama cha siasa ili kiwe na nguvu ni lazima kiwe na NARRATIVE yenye mvuto. Wakati Dr Slaa akiwa Katibu Mkuu wake, Chadema kilipata nguvu kwa kasi kubwa chini ya NARRATIVE ya kupinga ufisadi. Wote tuliaminishwa kwamba Chadema kina PRINCIPLE. Binafsi nilikiamini hadi nikakichangia fedha. A nontrivial amount.
Kilipofika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita, Chadema wakakiuka PRINCIPLE inayosema "the end does not justify the means". Waliamua wawakanganye wananchi kwa kuchukua mtu waliyedhani "ana nguvu sana" apeperushe bendera yao, pamoja na ukweli kwamba walikuwa wanamtaja huyo mtu kuwa ni fisadi papa. That destroyed their NARRATIVE completely.
Ushauri wa bure kwa Chadema. Tafuteni NARRATIVE nyingine yenye mvuto mkubwa na muiimbe kila mahali na kila saa. Mpaka ikolee kabisa. Itawajenga tena. Ipo NARRATIVE ya aina hiyo. Ni KATIBA MPYA. Drop everything and concentrate on that. Mbona mtaungwa mkono na kila mtu! Hata CCM wengi watawaunga mkono.
Stop petty things like attacking Dr Slaa. That won't build you up. He commands far more respect that you do.