Kwahiyo haki yangu ndo nadhulumiwa?

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
782
1,056
Wakuu,

Mimi ni mwajiriwa katika taasisi binafsi,
na miezi kadhaa ijayo mkataba wangu unaelekea kwisha.

Sasa nasikia mfuko wa jamii wa PPF wamesitisha kuwapa mafao yao wale wanaojiondoa,
Nami niliunganishwa kwenye huo mfuko na mwajiri.

Ina maana
hakuna namna ingine ya kupata hiyo haki yangu zaidi ya kudhulumiwa jasho langu la kipindi chote nilichotumikia kazini?
 
Nadhani ishu yako ni tofauti, kwa sababu mkataba unakwisha sasa hapo lazima wakupe chako. Kujitoa ni tofauti na mkataba kwisha. Mkataba kwisha mana yake unastaafu. So stahiki zako lazima upewe
 
Haki yako ya msingi kamwe haitopotea hama Kazi Mara nyingi uwezavyo akiba yako itaendelea kuwepo hadi 55 miaka
 
Na inakuwaje kama nina lengo la Ku_terminate mkataba kabla ya muda wake kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa Kwenye mkataba?
 
Kwa mfano mtu ana lengo la kusitisha mkataba na kuanza kujiajiri Hata Kabla ya miaka 55 inakuwaje?
 
Na inakuwaje kama nina lengo la Ku_terminate mkataba kabla ya muda wake kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa Kwenye mkataba?
Hapo ndio unalipwa yale makato yako tu, kutoka kwa mwajiri wako hupewi
 
Nadhani ishu yako ni tofauti, kwa sababu mkataba unakwisha sasa hapo lazima wakupe chako. Kujitoa ni tofauti na mkataba kwisha. Mkataba kwisha mana yake unastaafu. So stahiki zako lazima upewe
Hadi miaka 55 ndio utapata,hii sheria ni mbovu kabisa mtu anaeza achishwa kazi usiwe na pa kuanzia.

Lengo la SSRA ni kuondoa umaskini je waaondoa au wanazidisha ?

Nina mdogo wangu kaajiriwa kwenye mradi pale Muhas baada ya miaka 3 mrad unaisha hapo watamwambia asubiri miaka 55 hii haiingii akilini hata kidogo

Kwakweli Tz tunakoelekea kubaya,

Basi wapeni watu kazi za kudumu hapa mnawanyima haki zao wale wanaofanya kwa muda mfup
 
Nadhani ishu yako ni tofauti, kwa sababu mkataba unakwisha sasa hapo lazima wakupe chako. Kujitoa ni tofauti na mkataba kwisha. Mkataba kwisha mana yake unastaafu. So stahiki zako lazima upewe
Huko sio kustaafu ndugu, hapo Unachukua fao la kujitoa na wala sio pension ya kustaafu, kustaafu ni mpaka utimize 55yrs au 60yrs
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom