Kwaheri ya kuonana Faru John

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,863
5,694
Hakika tutakumbuka daima Faru John, kwani umetutoka kimazingara na wakati bado tunakuhitaji hapa Duniani. Ni vigumu kuamini kama umetutoka basi salamu zetu zikufikie popote pale ulipo.

Ewe Faru John huko ulikokwenda ukibahatika kukutana na Mwalimu, mwambie bado tuna mkumbuka Sana, tunakumbuka busara zake, ujasiri wake na maono yake kuhusu hii klabu yetu.

Mwambie lile Gari alilo liacha hapa klabuni sio salama tena kusafiria. Madereva makondacta na wapiga debe wamekuwa jeuri kweli kwa abiria.

Ukibishana nao tuu hawakushushi kituoni kwako, watasafiri na wewe umbali mrefu kisha utashushwa eneo usilo lijua na kupotezwa huko na kuwa mwisho wako wa uhai au wakutese vikali sana .

Mwambie sio tuu binadamu wanao fanyiwa ufilauni huo hata wanyama pia nao sasa wanafanyiwa hivyo hivyo. Mpe Ukweli jinsi wewe ulivyo potea na jinsi tunavyo kutafuta mpaka sasa bila mafanikio.

Ukiwa ndani ya gari abiria hatutakiwi kuongea, kukosoa au kutoa maoni yetu juu ya mwendo kasi wa gari hili na usalama wetu. Ukimwambia dereva spidi mbona Kali hapo mbele kuna kona dereva anajibu jeuri yeye kafuzu na hajaribiwi.

Gari tunaliona linarudishwa nyuma kwa spidi kali ukiuliza kwa nini utaambiwa gari linaenda mbele kama hutaki kusafiri shuka na mizigo yako hupewi na hata nauli hurudishiwi.

Mwambie mwalimu hapa ninapo ongea nimejificha chini ya buti la gari ili wasinione nikiongea hawa wapiga debe wakanipoteza. Gari lipo spidi kali abiria wamechoka njaa Kali lakini dereva hataki kusimama tule na hatujui anaenda wapi.

Najua itamsikitisha Sana mwalimu kusikia habari hii juu ya Gari alilo tuachia linavyo tumika vibaya. Ila msisitizie asinitaje kuwa ni mimi nimempa taarifa. Madereva wenyewe hawa hatuwaamini wengi wanatumia vilevi wanaweza kukugonga na gari kwa makusudi.
 
Hali ikiendelea hivi inabidi kila zahanati ya kijiji iwe na kitengo cha magonjwa ya mfadhaiko! Watu wengi wanaugua stress kwa ushahidi wa thread zinazoletwa hapa!
 
Kwa jinsi ulivyoliongelea hilo gari inaonekana ni pickup maana wanyama wamepanda humo humo,lkn pickup haipakizi abiria wengi,basi itakuwa ni zile chai maharage za zenji,hivi zile chai maharage wanyama uliowataja watakaa wapi? Au tumepakizwa kwenye fuso? Labda lori nusu wanya wanya nusu tumepangwa cc abiria...
sawa ilimradi gari
 
rhinoculled.jpg
 
Kwanini Faru amekua maarufu kiasi hichi tunashangaza sana kwani Faru si wapo wengi tu kwenye Mbuga zetu huyu Faru John yeye ana kipi kikubwa kwani km kutafuta kiki za Kumalizia mwaka aanzishe mjadala wa kudai mabaki ya DINOSOSI yaliowekwa kule Ujerumani yaletwe kwetu tutamuona kafanya jambo kubwa sana ktk sekta hii ya Utaliii
 
Labda sababu ya jina lake la John
 
Hali ikiendelea hivi inabidi kila zahanati ya kijiji iwe na kitengo cha magonjwa ya mfadhaiko! Watu wengi wanaugua stress kwa ushahidi wa thread zinazoletwa hapa!
nyani hawezi kuuona mkunduwe, hivi wewe si ndo utakuwa mteja wa kwanza endapo hizo zahanati zitafunguliwa? Maana kama huoni kuwa tumepanda gari bovu basi ww ndo una matatizo
 
Kwanini Faru amekua maarufu kiasi hichi tunashangaza sana kwani Faru si wapo wengi tu kwenye Mbuga zetu huyu Faru John yeye ana kipi kikubwa kwani km kutafuta kiki za Kumalizia mwaka aanzishe mjadala wa kudai mabaki ya DINOSOSI yaliowekwa kule Ujerumani yaletwe kwetu tutamuona kafanya jambo kubwa sana ktk sekta hii ya Utaliii

Faru John mbali na sifa nyingine alikuwa na umaarufu wa kupiga game mwanzo mwisho!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hakika tutakumbuka daima Faru John, kwani umetutoka kimazingara na wakati bado tunakuhitaji hapa Duniani. Ni vigumu kuamini kama umetutoka basi salamu zetu zikufikie popote pale ulipo.

Ewe Faru John huko ulikokwenda ukibahatika kukutana na Mwalimu, mwambie bado tuna mkumbuka Sana, tunakumbuka busara zake, ujasiri wake na maono yake kuhusu hii klabu yetu.

Mwambie lile Gari alilo liacha hapa klabuni sio salama tena kusafiria. Madereva makondacta na wapiga debe wamekuwa jeuri kweli kwa abiria.

Ukibishana nao tuu hawakushushi kituoni kwako, watasafiri na wewe umbali mrefu kisha utashushwa eneo usilo lijua na kupotezwa huko na kuwa mwisho wako wa uhai au wakutese vikali sana .

Mwambie sio tuu binadamu wanao fanyiwa ufilauni huo hata wanyama pia nao sasa wanafanyiwa hivyo hivyo. Mpe Ukweli jinsi wewe ulivyo potea na jinsi tunavyo kutafuta mpaka sasa bila mafanikio.

Ukiwa ndani ya gari abiria hatutakiwi kuongea, kukosoa au kutoa maoni yetu juu ya mwendo kasi wa gari hili na usalama wetu. Ukimwambia dereva spidi mbona Kali hapo mbele kuna kona dereva anajibu jeuri yeye kafuzu na hajaribiwi.

Gari tunaliona linarudishwa nyuma kwa spidi kali ukiuliza kwa nini utaambiwa gari linaenda mbele kama hutaki kusafiri shuka na mizigo yako hupewi na hata nauli hurudishiwi.

Mwambie mwalimu hapa ninapo ongea nimejificha chini ya buti la gari ili wasinione nikiongea hawa wapiga debe wakanipoteza. Gari lipo spidi kali abiria wamechoka njaa Kali lakini dereva hataki kusimama tule na hatujui anaenda wapi.

Najua itamsikitisha Sana mwalimu kusikia habari hii juu ya Gari alilo tuachia linavyo tumika vibaya. Ila msisitizie asinitaje kuwa ni mimi nimempa taarifa. Madereva wenyewe hawa hatuwaamini wengi wanatumia vilevi wanaweza kukugonga na gari kwa makusudi.

Ni mengi likiwemo hili ambayo yamenidhihirishia kwamba kumbe kweli "kufa kufaana na wala si kufanana".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom