Kwa yoyote yule aliyekuwa nayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa yoyote yule aliyekuwa nayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Black Jesus, May 21, 2009.

 1. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba kama kuna mtu yeyote yule amabe anayo au anaweza kunambia wapi naweza kuipata ile hutuba ya Dr mwaykembe aliyohutubia na kuwambia viongozi wa ZANZIBAR kuwa hawana ADABU.
   
 2. Mpandafarasi

  Mpandafarasi Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndugu WanaJF,

  Kama mdau alivyoomba naomba kuwasilisha mtundiko wangu nikiambatanisha speech ya Mheshimiwa Mwakyembe. Kwa kifupi Mheshimiwa Mwakyembe alikuwa akichangia katika BUNGE LA TANZANIA ndani ya MAJADILIANO YA BUNGE pale kwenye MKUTANO WA KUMI NA MBILI ndani ya Kikao cha Arobaini na Tano – Tarehe 14 Agosti, 2008. (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi).

  Mheshimiwa Mwakyembe aliwasilisha hoja zake kama hivi:


  MHE. DR. HARRISON G. MWAKYEMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kukubali nichangie leo asubuhi, hivyo kuniwezesha kushiriki kikamilifu kwenye kikao muhimu kilichofanyika jana cha Nishati na Madini.


  Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Katiba na
  Sheria, Mheshimiwa Mathias Chikawe kwa kuwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa ufasaha mkubwa. Vile vile nampongeza kwa kututhibitishia wote hapa kwamba pamoja
  na kutokuwa na Naibu Waziri, anaweza akafanya kazi barabara na kwa ufanisi mkubwa.
  (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, nimefarijika sana na taarifa iliyoko ukurasa 35 wa taarifa ya Mheshimiwa Waziri inayoelezea utekelezaji wa hatua ya kutenganisha shughuli za upelelezi na shughuli za uendeshaji mashitaka, shughuli ambazo kwa muda mrefu sana zimekuwa zikiendeshwa na Polisi. Polisi huyo huyo anakamata, Polisi huyo huyo anapeleleza, Polisi huyo huyo anahoji kwa maana ya interrogation, Polisi huyo huyo anaamua nimpeleke huyu Mahakamani, nisimpeleke na Polisi huyo huyo anaendesha mashitaka. Kwa kweli hiyo hali haikuwa nzuri sana na haijawa nzuri mpaka leo kwa sababu madaraka yote hayo kuwa kwenye mikono ya chombo kimoja ni hatari kwa utawala wa sheria na utoaji wa haki. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, lakini tumechelewa sana kuanza utekelezaji wa zoezi hili hasa ikizingatiwa kwamba pendekezo la kutenganisha shughuli hizi lilitolewa kwa Serikali tarehe 12 Agosti, 1977 (miaka 31 iliyopita) na Tume ya Kupitia Mfumo wa Utoaji Haki (The Judicial System Review Commission) iliyokuwa inaongozwa na Mheshimiwa Pius Msekwa, wakati huo akiwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Mheshimiwa Spika, nasema tu kwamba hali hii ya kukalia mapendekezo ya msingi kama haya kwa miaka 31 haipendezi. Ni muhimu kwa Serikali kutekeleza bila kuchelewa sana mapendekezo ya Tume ambazo Serikali yenyewe inaziunda Tume zinatumia muda mwingi na pesa ya walipa kodi.

  Mheshimiwa Spika, lakini yaliyopita si ndwele, tugange na yaliyopo na yajayo. Ninachosema tu ni kwamba ili zoezi hili la Civilianization of Prosecution liweze kufanikiwa vizuri, basi kuna umuhimu kuboresha mazingira ya kazi ya Mawakili wa Serikali. Kwa kweli hali yao siyo nzuri sana na naweza kudiriki kusema Wizara ya Katiba na Sheria ni moja ya Wizara ambazo kwa kweli wataalam wake wanakimbia kwa urahisi sana kutokana na mazingira ambayo siyo mazuri. Na siyo kosa la Mheshimiwa Waziri au Katibu Mkuu, ni kosa letu sisi wote kwamba kwa kweli tuna-provide hela kidogo sana kwa Wizara hii.

  Mheshimiwa Spika, mimi sisemi Wakili wa Serikali alipwe kama Wakili wa Kujitegemea, hapana. Ninachosema ni kwamba, tumeshindwa kuwapa vijana wetu mahitaji ya msingi kabisa kuweza kutekeleza kazi zao. Wakili wa Serikali ambaye tunambebesha mafaili ya kesi za ujambazi, kesi za ufisadi, kesi za aina mbali mbali, hatujui analala wapi. Tunachojua tu sisi ni kumpa Sh. 70,000/= kwa mwezi akatafute chumba. Siku hizi tumeongezea eti 100,000/=. Hata kwa Dodoma hapa, hupati nyumba kwa 100,000/= na Dar es Salaam ndio shida. Kwa hiyo, vijana wetu wametawanyika hovyo kwa Mfuga Mbwa, sijui Gongolamboto Dar es Salaam na kadhalika. Tunawaweka kwenye vishawishi vikubwa mno!

  Mheshimiwa Spika, kwenye nchi za jirani, wenzetu tu hapa hapa, State Attorneys wanakaa kwenye Quarters za Serikali ambazo ni more secure kiusalama. Hapa, siku hizi inakuwa sherehe kwa mwenye nyumba akiona Wakili wa Serikali anakaa nyumbani kwake kwa maana kila asubuhi anakuja kugonga mlango “kijana wangu, hebu nisaidie mtoto wangu wa jirani pale kakamatwa na bangi, kamtoe.” Basi ndio kazi hiyo vijana wetu wanafanya. Tunawapeleka huko.

  Wakili wa Serikali hana usafiri. Yeye na daladala, daladala na yeye. Mvua inyeshe, jua kali, akiwa na mafaili ya Serikali. Wakili wa Serikali tunamtegemea awe smart; suti nyeusi, kiatu cheusi, soksi nyeusi, shati jeupe na haliwezi kuwa moja tu, litaleta utando wa kutisha, kwa hiyo, mashati ya kutosha meupe, tai nyesi na tai maalum nyeupe. Lakini pesa tunayompa Wakili wa Serikali kununulia vitu hivyo, haitoshi hata kununulia robo ya vitu hivyo. Nafikiri kuna umuhimu sasa hivi kuongeza bajeti ya Wizara hii.

  Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri na uongozi mzima wa Wizara akiwepo rafiki yangu Salula - Katibu Mkuu mwenye uwezo mkubwa sana, walipiganie suala hili ili mwaka ujao wa fedha tuone mabadiliko ya package ya State Attorneys. Mimi nimefurahia kidogo kusikia kuhusu habari ya Mahakama. Taarifa ya Mheshimiwa Waziri iko ukurasa wa 50 wa kitabu chake inasema kuwa kimsingi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekubali kuanzishwa kwa Mfuko wa Fedha wa Mahakama (Judiciary Fund). Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri, kwa sababu Rais alikubali mwezi wa Tano, mwezi Oktoba tuone Muswada wa Sheria hiyo hapa, tusichelewe chelewe. Mahakama iko katika hali mbaya, wanahitaji an Independent Fund.
  (Makofi)
  Mheshimiwa Spika, naomba niongelee suala moja dogo lingine. Jana jioni nilishitushwa na joto lililokuwepo humu ndani kuhusu Mahakama ya Kadhi. Nikapata wasiwasi kidogo kwamba pengine sikusoma vizuri hotuba ya Waziri wa Katiba, kwa hiyo, ikabidi niisome tena ukurasa wa tano mpaka ukurasa wa saba. Lakini ujumbe niliyoupata pale ni mzuri tu. Taarifa inasema, Tume ya Kurekebisha Sheria imekamilisha utafiti wake na taarifa yake imewasilishwa Serikalini na Serikali sasa hivi inatafakari taarifa hiyo na uamuzi wa Serikali utaletwa Bungeni. Sasa hili joto linatoka wapi? Why
  are we jumping the gun?

  Mheshimiwa Spika, utadhani kwamba sasa tumepewa Muswada wa Mahakama ya Kadhi uko mbele yetu, sasa tunabishana! Hapana! Mheshimiwa Waziri ameleta habari njema sana kwetu. Baadhi yetu, tunadhani hili suala ni jepesi sana. Wengine wanasema, hivi mnachelewesha nini? Tungeanza hata jana! Hapana! Wengine walifikia hatua jana, nimesikitika kusema eti wengine haliwahusu! Eeh, hii hatari! (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, nadhani hii sio sahihi, wote tunahusika, Mahakama hii ikianza wote sisi Waislam na wasio Waislam, tutachangia uendeshaji wake kupitia kodi zetu. Kwa hiyo, wote tunahusika! (Makofi)


  Mheshimiwa Spika, siku ya siku tutalazimika kurudi tena hapa, kubadilisha Ibara
  ya 19(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayosema: “Serikali haitajihusisha na uendeshaji wa vyombo vya dini.” Itabidi tuibadilishe na kuibadilisha hiyo haitahitaji Waislam peke yao, itahitaji wote hapa. Ibara ya 98 ya Katiba inasema, unahitaji theluthi mbili ya Wabunge wote kuweza kupitisha hilo suala. Kwa hiyo, wote tunahusika! Mimi naomba tuiachie Serikali ifanye kazi yake kwa uangalifu, hili si suala jepesi kama ambavyo wengine wanasema. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, wengine wanasema, aah, unajua Zanzibar mbona hakuna matatizo. Jamani, Zanzibar ni tofauti. kwani zaidi ya asilimia 99 ya wananchi wake ni Waislam. Kwa hiyo, siyo kitu cha kulinganisha. Ni sawa na Ujerumani. Mimi nimeishi Ujerumani. Ujerumani ukilipwa mshahara, unalipia kitu kinaitwa Kirchensteur ambayo
  ni kodi ya Kanisa, mpaka unajiuliza hivi hawa watu wana akili timamu! Unaambiwa eeh, hapa watu zaidi ya asilimia 90 ni Wakristo. Kwa hiyo, tusitoe mifano ambayo hailingani.
  (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, kumetolewa mifano ya Uganda. Mimi nimefanya kazi Uganda. Uganda, Mahakama ya Kadhi iko kwenye Katiba, lakini mpaka leo haijaanza kufanya kazi. Kwa hiyo, Serikali ambayo ni prudent, lazima iangalie kwa makini kabla
  ya kuanzisha. Tuipe Serikali muda, tusii-rush. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, Kadhi Mkuu kwa mfano, inapendekezwa sehemu nyingi na hata hapa itapendekezwa kwamba ateuliwe na Rais. Kwa hiyo, lazima Serikali ianze kuangalia. Je, what if Rais anakuwa Mkristo, nani atakubali kwa mfano Kadhi Mkuu ateuliwe na Kafir? Kwa hiyo, ni mambo ya kuangalia hayo, tusii-rush Serikali kwenye hayo.

  Mheshimiwa Spika, mtu ambaye anaona anacheleweshwa, Katiba haimzuii wala Sheria haizuii kuanzisha utaratibu wa dini wa dispute settlement. Tuna mifano mizuri tu. Wakatoriki wanayo a very elaborated system of dispute settlement ambayo wanaigharamia wao wenyewe. Utakuta wana Tribunal of First Instance kwenye Jimbo, appeal zinakwenda kwenye Tribunal of Second Instance ambayo ni kwenye Taifa na Majaji pale ni Maaskofu yaani Baraza la Maaskofu na lazima hawa wote wawe wamesoma Canon Law. Appeal zinakwenda Rome na kule wanakaa Majaji watano. Sasa pale ikifika, ndio mwisho. Panaitwa Signatura Apostolica, ndio mwisho. Ndio Supreme Court hiyo. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, nilikuwa nasema yote haya kusisitiza tu kwamba jamani, hebu tusi-rush suala hili , tusiweke joto lisilo na maana, Serikali imepokea, Waziri amesema. Ametoa tamko zuri, kuwa watalileta Bungeni. Leo tunaongea utadhani kuna hoja hapa ya kadhi. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, naomba niongelee hoja ya Msemaji wa Upinzani jana kwamba suala la Zanzibar ni nchi au sio nchi ni mgogoro wa kikatiba. Mimi siuoni mgogoro wa Kikatiba hapa, ila ninachokiona zaidi hapa ni utovu wa nidhamu kwa baadhi
  ya viongozi. Nitaeleza. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, kikatiba uwajibikaji wangu, mimi kama Mbunge ni tofauti na uwajibikaji wa Waziri. Mimi nawajibika kwa vitu vitatu; nawajibika kwa Jimbo langu
  (wananchi walionipigia kura), nawajibika kwa chama changu na nawajibika kwa dhamira yangu kama Mtanzania, kama mzalendo. Lakini Waziri anafungwa na kanuni ya kikatiba
  ya kwamba yeye lazima awe na msimamo wa pamoja na Serikali nzima wanapokuwa hapa Bungeni. Inaitwa Collective Ministerial Responsibility. Wanafungwa na hicho. Sitaki kusoma Ibara ya 53(2) inayosema; Mawaziri wote chini ya Waziri Mkuu, wanawajibika kwa pamoja kwa Bunge hili. (Makofi)
  Mheshimiwa Spika, nasema yote haya kueleza tu kwamba linaloamuliwa na Serikali, Mawaziri hawana choice, lazima kuunga mkono. Waziri Mkuu akinyoosha mkono wa kulia, wote lazima wanyooshe kulia. Wasiponyosha kulia watadondoka kwa sababu Waziri Mkuu akiamua tu kujiuzulu, mnajua Cabinet yote inakwenda. Waziri Mkuu akikohoa, wote homa hawa! Kwa hiyo, ninachosema tu hapa ni kwamba, kama Waziri au Naibu Waziri hakubaliani na msimamo wowote wa Serikali, hawezi kupinga hadharani. Wana vyombo vyao vya siri vya kuyamaliza humo ndani! Akitaka kuongea kama Mwakyembe au kama Mama Anne Kilango Malecela au Selelii au Ole Sendeka, basi ajiuzulu kwanza, huo ndio utaratibu wa Westminster System.

  Mheshimiwa Spika, nasema haya kwa sababu kilichotokea hivi karibuni, mimi nasema ni fedheha kubwa kwa Serikali yetu. Mimi nasema as a Constitutional Lawyer. Waziri Mkuu ametoa tamko hapa Bungeni, tamko sahihi kabisa kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar sio nchi in the sense of a Soveregn State. Akasema Wanasheria Wakuu kaeni chini, muangalie kama kuna dosari, basi muishauri Serikali. Kichekesho kinakuja. Mimi siwalaumu Wabunge, siwalaumu wananchi maana wananchi wana uhuru kujadili chochote. Lakini Mawaziri na sijali wa Zanzibar au wa hapa, kusimama kumkosoa Waziri Mkuu na kumkejeli, huko ni kutoka nje ya Collective Ministerial Responsibility ya Mawaziri. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, wengine wanafikia mpaka hatua ya kusema, aah, hata hela yetu iko BOT! Jamani, mimi nimekuwa najiuliza, Serikali iko wapi? Usiri na heshima ya Serikali yetu umekwenda wapi? Vyombo vya majadiliano ya Serikali nani amevipeleka likizo? Waziri wa Zanzibar anapomkejeli na kumkosoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; anajua constituonal implications zake? Anaelewa? Sema tu muda hamna, lakini ningependa sana kulielezea kwa nini nasema kwamba lina serious constituonal implications. (Makofi)

  Mheshimiwa Spika, nimalize tu kwa kusema, sipendi kupigiwa kengele. Kilichotokea kuhusu suala la Zanzibar ni nchi au si nchi na conduct ya Mawaziri hasa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni fedheha kubwa kwa Serikali. Hapa siuoni mgogoro wa kikatiba, ninachokiona hapa ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa baadhi ya viongozi ndani ya Serikali, utovu ambao lazima uadhibiwe. Ukiacha kutoadhibiwa, mimi sitaona ajabu siku moja Rais akinyoshewa vidole usoni. Naunga mkono hoja! (Makofi)

  Nawasilisha.

  NB: Msisitizo ni wangu binafsi. Kwa full hansard ya siku hiyo tembelea tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Angalia kurasa za 22 hadi 26
  http://www.parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-12-45-2008.pdf
   

  Attached Files:

 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hotuba hii - Baabu kubwa ktk kipengele husika..
   
 4. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Harrison Mwakyembe ana dharau ya ajabu kwa watu wa chini. Eti wanasheria wa serikali wasiishi Manzese kwa Mfuga Mbwa na Gongolamboto, kuna vishawishi. Anaona wote wa huko ni waovu wachafu. So uppity uppity.

  Halafu anadai, I am not making this up, Mwakyembe anadai Rais akiwa Mkristo waislam wote humwona Kafiri:

   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wewe nae kalale sasa.......
   
 6. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 857
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mimi ningeomba hotuma ya aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Mtwara Bwana Luwigo (Sina uhakika kama nimekumbuka jina lake vizuri) aliyoitoa kwa Mkapa akilalamikia kubinafsishwa kwa kitengo cha makontena. Kimsingi yeye alitakiwa kumkaribisha Mkapa lakini akatumia fursa ile kutoa hotuba. Rai waliichapishaga.

  Sehemu moja wapo ya hotuba alisema kuwa "najuwa Mh. Rais mara nitakapomaliza kutoa hotuba hii utanifukuza kazi kwa hivyo nimeshajiandaa na kufungasha mizigo yangu...."
   
Loading...