Kwa yeyote atakaye guswa

oruguyo

Senior Member
Jul 28, 2012
132
37
Ndugu naomba tusaidiane kuwaeleza wahusika kuhusu walimu ambao hawajalipwa fedha zao za kusimamia mtihani Wa kidato cha NNE mwaka Jana 2015. Ndugu kunawilaya ambazo hadi sasa walimu hawajalipwa fedha za usimamizi Wa mitihani ya kidato cha nne .kutokana na jambo hili kufanyika kwa mdamrefu, chama cha walimu kimeshindwa kushughulikia jambo hili. Tunaomba tusaidiane kufikisha taarifa hii kwa wahusika kwani hakuna dalili na mtuwakuwasemea walimu Wa Mbogwe geita jambo hili.aksante.
 
Daah walimu wanateswa, umenikumbusha wale waliochapwa kule sijui wapi na bwana Albert, wengine wanataka kushushwa vyeo na maafisa wasipopeleka wilayani fedha za kuendesha michezo, na magumu mengine mengi. Sasa sijui nikushauri uvumilie tu.... sina uhakika.
 
Sihitaji ushauri nahtaji tusaidiane kufikisha ujumbe kwa mamlaka za juu zinazohusika.
 
Nyie ndio mnafanya walimu kudharauliwa,na kwanini tatizo lipo baadhi ya wilaya tu,wanajua mbulula tu na mapoyoyo
 
Kazi tayari ilikwisha dharauliwa tunachofanya nikuwaonyesha wahusika nikwanamna gani dharau zao zinavyozidi kujidhihilisha katika jamii.
 
Samahani mkuu kabla ya kuchangia, ningependa kujuzwa mambo kadhaa

Wahusika wa malipo kuanzia ngazi kitaifa, kimkoa,na kiwilaya

Pili ni kwanin wilaya zingine walilipwa na hizo zingine bado?

Baada ya hapo nitachangia
 
Mwalimu anasimamia paper muda wote halipwi hata mia, then ikiundwa kamati ya kumpoza ili vijana wajilie chabo akigundulika anaadhibiwa kuliko fisadi.
 
Walimu wa Geita mjitathimini yawezekana mna kasoro. Juzi juzi tu kuna taarifa ilirushwa na ITV kuwa walimu mnashukuru mahakama za kijadi kufutwa na Mkuu wa MKOA. Kwamba mlikuwa mkipewa kichapo cha mbwa Mwizi na mahakama hizo mlipo jaribu kuzigomea. Mmoja wenu akatoa ushuhuda kuwa kapata ulemavu wa mguu kutokana na kichapo.
Sasa na wewe unakuja na hili swala hapa jamiiforum. Hivi umeshindwa kutoa malalamiko yako kwenye ngazi zote husika? Kama umetoa wamekujibu nn? Tangu nwaka jana hadi leo hujapata haki yako, umechukua hatua gani? Unadhani jf ni mahala sahihi pa wewe kumwaga dukuduku lako na likapatiwa ufumbuzi?
Niwaombe walimu wa Geita mtumie taaluma zenu kukabiliana na changamoto mlizo nazo. Hivi mnaposomea ualimu mnasomea na kozi ya kutii maonevu? Mbona jukwaa hili limejaa taarifa zenu tu za hakuna hiki kwa walimu, hakuna kile kwa walimu? Daaah!
 
Ungekuwa wewe ungefanya nini ? Mambo haya simepesi kama tunavyo dhani ndomaana tunalazimika kutumia mitandao yakijamii kuuonyesha umma dhuruma inayo fanyika dhidi ya watumishi Wa umma.
 
Soma tena ulichoandika
Unataka nibadilishe ukweli.
Walimu wa kanda ya ziwa ni shida wana matukio mengi sana yanayoonyesha kuwa ni mapoyoyo.
Haya matukio yote ya kupigwa na kukopwa kwa ajili ya kazi maalumu umewahi kusikia yametokea huku Dar es Salaam
 
Walimu wa Geita mjitathimini yawezekana mna kasoro. Juzi juzi tu kuna taarifa ilirushwa na ITV kuwa walimu mnashukuru mahakama za kijadi kufutwa na Mkuu wa MKOA. Kwamba mlikuwa mkipewa kichapo cha mbwa Mwizi na mahakama hizo mlipo jaribu kuzigomea. Mmoja wenu akatoa ushuhuda kuwa kapata ulemavu wa mguu kutokana na kichapo.
Sasa na wewe unakuja na hili swala hapa jamiiforum. Hivi umeshindwa kutoa malalamiko yako kwenye ngazi zote husika? Kama umetoa wamekujibu nn? Tangu nwaka jana hadi leo hujapata haki yako, umechukua hatua gani? Unadhani jf ni mahala sahihi pa wewe kumwaga dukuduku lako na likapatiwa ufumbuzi?
Niwaombe walimu wa Geita mtumie taaluma zenu kukabiliana na changamoto mlizo nazo. Hivi mnaposomea ualimu mnasomea na kozi ya kutii maonevu? Mbona jukwaa hili limejaa taarifa zenu tu za hakuna hiki kwa walimu, hakuna kile kwa walimu? Daaah!
Yeye kashindwa na ndio maana kaamua kupiga kelele, kama wewe unajua pakuanzia ni wakati sahihi wa kumuelimisha.

Kumsema bila kumpa mbinu ya kufanya hujamsaidia. Mpe mbinu akishindwa ndio umseme,

Binadam tunatofautiana katika kukabiliana na changamoto, sasa kama wewe unajua namna ya kufanya msaidie nq sio kumsema pekee
 
Back
Top Bottom