A
Anonymous
Guest
Katika usimamizi wa Mitihani ya Taifa Kidato cha Pili na Nne kumekuwa na tofauti ya muundo wa ulipwaji wa fedha za usimamizi baina ya Halmashauri moja na nyingine.
Mfano, hapa Manispaa ya Morogoro wasimamizi wa mikondo wamelipwa pesa pungufu ukilinganisha na maeneo kama Tanga Jiji, Mbinga nk.
Kituo kina siku 13
Baadhi yenu kuna mtu atalipwa siku 10, mwingine 6 na mwingine 12 inategemea na siku atakazosimamia lakini huko Tanga Jiji watu wote wamelipwa kwa idadi ya siku husika kwenye kituo husika cha mtihani.
Kama mpo wasimamizi wasaidizi 6 wote mnalipwa kabla ya kazi kiasi sawa bila kulingana na ratiba ya mtihani katika kituo husika.
Manispaa ya Morogoro kumekuwa na wizi, wanawaondoa watu kabla ya mtihani kuisha na hatujui fedha hizo huwa zinaenda wapi. Kuna maofisa hapa wamezoea kudhulumu wasimamizi wasaidizi na wanaamini hakuna namna jambo hili linaweza kufika katika mamlaka za juu.