johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 718
- 703
Kwa muda sasa, nimekuwa nikijaribu kuitazama jumuiya ya afrika mashariki kwa lengo la kutafuta manufaa yake hususan kwa watu maskini kabisa wanaoishi kwenye vijiji vya nchi hizo, lakini lakini kwa bahati mbaya nimekosa kuyaona hayo manufaa.
Jumuiya hizi za kikanda na nyingine zinazofanana na hizo hususan katika bara la afrika ni sawa na klabu za kuwakutanisha viongozi wakuu wa nchi wanachma ili kupiga soga huku wakitumia mamilioni ya fedha za walalahoi w amataifa hayo kwa ajili ya kujiburudisha.
Kinachoendelea Burundi ni kielezo ya fikra hizo kuwa jumuiya hizi hususan EAC ni vitengo vya kikanda vyenye lengo la kuwakutanisha na kuwanufaisha watu wachache huku mamilioni wengine wakiachwa wasijue haswa kinachoendelea.
Ni aibu kusikia wiki moja baada ya baada ya kuanza kwa machafuko yanayopeleka vifo na maelfu wengine kuishi ukimbizini, ndio sasa Jumuiya ya EAC inaanza kuchukua hatua kwa kinachoendelea nchini Burundi.
Sasa EAC ndio imetuma Ujumbe Burundi kwenda "kufahamu" nini kinaendelea wakati nchi za mbali na hata jumuiya nyingine kama UN zikiwa zimeanza mapema kuchukua hatua dhidi ya mgogoro wa Burundi. Baada ya tume kurejea na kuandaa ripoti ndio viongozi ( akiwemo na mwanzilishi wa dhahama hii, Nkurunziza) wa chi wanachama watakutana ili kubaini hatua za kufanya.
Najiuliza tu, Jumuiya hii iliyoko katika ncjhi za ukanda wenye historiaya machafuko ya mara kwa mara, inacho chombo ambacho kinaheshimiwa kwamba kikitoa maamuzi ya haraka na yatatekelezwa?