Kwa yanayoendelea, Jeshi la Polisi lisajiliwe kama Chama cha Siasa

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Haina maana yoyote watanzania kuendelea kuwa wanafiki, kwa mujibu wa katiba jeshi ni chombo cha kulinda raia na mali zao, na linapotokea jambo kama uchaguzi polisi inatakiwa iwe kama refree wa ngumi, kuachanisha inapobidi lakini wakiachiana unaacha watwangane ngumi kwa mujibu wa sheria.
Kinyume chake jana jeshi la polisi lilionekana limebeba wafuasi wa ccm ndani ya magari yao na wao kama washereheshaji. Hii siyo tu inatia kinyaa bali inaridhalilisha jeshi la polisi na viongozi wake, inaonekana Tanzania tumeamua kuporomosha taasisi kwa kasi Kubwa, nchi inaendeshwa kwa kauli na vitisho, watoto wadogo kama Gambo na Makonda wanatembea na motorcade utafikiri nchi ina marais watatu.

Jana wasimamizi wa vyama wametolewa nje nchi nzima alafu wanasema wameshinda! umeshinda ulikuwa unashindana na nani? Watu kadhaa wamepigwa mapanga polisi wanaangalia kwa kuwa wametumwa kuwaonea raia wasifanya jambo ambalo katiba imeruhusu!

Najua polisi na viongozi wake akina Sirro wao ni binadamu na nafsi yao inawaambia kwamba wanafanya jambo ambalo silo, lakini kwa kuwa wametumwa kufanya maonevu na watu wanaoitwa wakuu wa wilaya na mikoa wamegeuka kuwa adui wa raia.

nataka niwaase polisi najua nyie ni bindamu na mnafanya kazi chini ya shinikizo kubwa kwa kuwa nchi inaongozwa na mtu licha ya kuwa na roho mbaya ya kuzaliwa nayo lakini pia hana common sense mnachotakiwa kufanya akina Sirro mtakapopewa maagizo yanayoendana na ukandamaizaji wa haki za raia mkatae it won’t be the end of the world, msipofanya hivyo mnachochea hasira za raia. Nyie hamko mitaani sisi tuko huku hasira juu yenu ni kubwa kupita maelezo.

Kama hamtaweza kufanya hayo kujitenga na siasa ni bora ijulikane tubadilishe katiba jeshi la polisi lisajiliwe kama chama cha siasa ili vyama pinzania vijue nyie ni washindani halali wa kisiasa ili na wao mtakapowapiga virungu na wao wawe na vikosi vyao vya ulinzi wawe na haki ya kujibu mapigo.


Nawakilisha
 
Ni wakati wa kutafakari kwa kina na kutumia akili kuwa nini kifanyike kuondoa utawala huu usiojali haki za raia wake ila unajali kukusanya kodi wajinufaishe
 
Ni wakati wa kutafakari kwa kina na kutumia akili kuwa nini kifanyike kuondoa utawala huu usiojali haki za raia wake ila unajali kukusanya kodi wajinufaishe

Mkuu tafakari inabidi ifanyike kwa haraka, mimi nimekutana na baadhi ya wana ccm unawaona wamevaa magwanda lakini nafsi zao unaona jinsi ambavyo zinasikitika kwa udhalimu unaozidi wa makaburu wa South Africa enzi hizo.
 
Back
Top Bottom