Kwa wenye uzoefu na powertiller, msaada please

Tarakilishi

JF-Expert Member
May 19, 2013
2,181
2,446
Nimeamua kujikita kwenye ujasiriamali wa kilimo, hivi sasa nimeshalima mpunga kwa mara ya kwanza. Katika kujiandaa vzuri na kilimo nina lengo la kununua powertiller, Hivyo ninaomba msaada wa mawazo kwa wenye uzoefu na powertiller, ni aina ipi nzuri, horsepower ngapi, Bei zake zina-range kiasi gani, zinapatikana wapi, Ufanisi(hapa nataka kujua kama zinafaa kweli kwa kilimo maana nimekuwa nikipata tetesi za mara ooh haziwezi ardhi ya tz n.k. Natanguliza shukrani zangu, mawazo tofauti yanakaribishwa
 
Kubota pekee
 
Naleta mrejesho kuwa kilimo changu cha mpunga nilifeli 100% kwasababu ya udhaifu wa usimamizi. Katika kufeli kwangu nimejifunza jambo moja kubwa sana nalo nil "Kilimo ni usimamizi". Ukifeli kwenye usimamizi jiandae kupata hasara tu, hamna namna. Mi nilikuwa nalima kwa simu mwisho wa siku nikavuna mabua shamba zima.
Sasa hivi nipo kwenye ujasiriamali mwingine ambao naweza kuusimamia na maendeleo ni mazuri. Siku nikiacha kazi ndio nitarejea kwenye kilimo maana nitakuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya usimamizi.
 
Powertiller ni Kubota tu ndio bora na bei yake inarange m8_10 hapo inakuwa full kuanzia mashine yenyewe, tela, majembe yote, matairi yote ya kawaida na ya chuma
 
Kwa kilimo cha mpunga powertiller inafaa hasa wakati wa kuchakata udongo, nakushauri ununue Kubota haya ya kichina niliyanunua mawili lakini injini yake haidumu na pia zina tatizo kwenye gearbox . Cha kuzingatia ni kwamba Powertiller ni kwa ajili ya kilimo kidogo cha shamba dogo kwa baadhi ya ardhi kukatua ni shida kubwa kwani ulimaji unategemea nguvu za mlimaji ila kwa kuchakata powertiller ni mkombozi
 
Kwel kabisa mkuu, zinabeba na mizigo pia ukishavuna, kwa huku kwetu kipind cha kiangazi zinabeba hadi matofali na mchanga
 
Back
Top Bottom