Kwa wenye matatizo ya Moyo.. huduma bure Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wenye matatizo ya Moyo.. huduma bure Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 17, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Mgonjwa wa moyo wahi THI, upasuaji wa bure...

  2008-10-17 10:32:36
  Na Richard Makore

  Muungano wa nchi za Falme za Kiarabu kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchi mbalimbali duniani leo wanaanza kutoa huduma ya upasuaji wa moyo bure nchini.

  Huduma hiyo ya maradhi ya moyo itatolewa katika Taasisi ya Moyo Tanzania (THI) iliyopo jijini Dar es Salaam.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Falme hizo hapa nchini, Mallalla Mubarak, alipozungumza na waandishi wa habari.

  Mubarak alisema nchi yake imetoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo hivyo matibabu yatatolewa bure THI kuanzia leo.
  Alisema Watanzania wote, watoto kwa wakubwa wanakaribishwa katika hospitali hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Aliongeza kuwa wananchi wengi wanaokabiliwa na maradhi ya moyo wanakufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu nje ya nchi.

  Balozi Mubarak alisema wananchi wote wenye matatizo ya moyo wanatakiwa kufika hospitalini hapo ambapo watawakuta madaktari bingwa wakiwasubiri.

  Aidha, alisema leo watafanya kazi ya kuwachunguza wagonjwa wote watakaofika hapo na wiki ijayo ndiyo kazi ya upasuaji itaanza.

  Alifafanua kuwa madaktari bingwa watakaoshiriki katika upasuaji wanatoka Uingereza, Misri, Ufaransa, India na wengine kutoka hapa nchini.

  Aliongeza kuwa utafiti uliofanywa na nchi yake hapa nchini umebaini kuwa watu wengi wana matatizo ya moyo.

  Alisema baada ya kumaliza uchunguzi wa awali unaoanza leo, wiki ijayo wataanza kutibu wagonjwa watakaobainika kusumbuliwa na moyo.

  Balozi huyo alisema, licha ya mgonjwa kufanyiwa matibabu ya moyo pia atapatiwa dawa zingine bure.
  Alisema zoezi hilo pia litafanyika visiwani Zanzibar na Pemba.

  Nchi zilizofaidika na ufadhili wa matibabu hayo hadi sasa ni Kenya, Sudan, Ethiopia, Syria na Morocco.

  Mkurugenzi wa THI, Dk. Ferdinand Masau, alisema zoezi hilo litachukua wiki mbili na kipindi hicho kila mtu anayesumbuliwa na moyo afike kwa ajili ya kupata matibabu bure.

  Dk. Masau alisema watakuwa wanatoa huduma hiyo kwa watu 15 kwa siku wakiwemo watoto na watu wazima.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Oct 17, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hii nayo ni siasa au matangazo
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Namuombea Dr Massau na Watanzania wote Afya njema. Hapa US tunabahati ya kupata huduma ya juu sana na nina imani kwamba kwa mfano wa Dr Massau Watanzania wengi wananufaika. Tanzania tunataka vifaa zaidi vya screening vya kisasa hasa vya kansa na moyo, serikali inatakiwa kufanya utaratibu kupata hivi vifaa. Ukweli ni kwamba kama tuta screen watu wengi na kuzuia magojwa kabla hayaja tokea serikali itapunguza garama za kuhudumia wagojwa wa kansa na moyo.
   
 4. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #4
  Oct 17, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jitihada za THI chini ya Dr.Massau zinaoneka wazi kabisa na ninawashukuru pia hawa wakuu wa nchi za kiarabu kwa kutoa huo msaada. Nadhani watanzania wengi tutanufaika kwa njia moja au nyingine na huduma hii. Tuwahimize tu wenye matatizo waende wakachekiwe........hope ile foleni ya kwenda india itapungua.

  Asante.
   
 5. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Isije ikawa ni yaleyale ya medical students/interns wako kwenye clinical training
  anyway,hongera Masau na watoa msaada.
   
 6. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ..Shy acha kuturudisha mwaka 47 we unaelewa kabisa jinsi baadhi ya watanzania wenzetu wanavyoteseka na matatizo ya moyo kwa kukosa pesa za matibabu au kwa kuwa wewe hayajakukuta ndio maana unaona ni siasa???

  Bravo THI na wote waliofadhili zoezi hilo................
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Waswahili hatuna jema. Kama wewe unaweza kuwatafuta intern duniani wakaenda kijijini kwangu kuwasaidia wale wagonjwa nitashukuru sana, kwani hata hao intern wa muhimbili kule hawafiki. wapo R.M.A na M.A ndio medical officer. Unaongea hivyo kwani hujawahi kuumwa kijijini utawatamani sana manesi wa red cross na hutawaona.
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hizi huduma za moyo bado zinzhitajika sana kwani maradhi ya magonjwa ya moyo yanazidi kushika kasi miongoni mwa Watanzania wengi kwa ngazi zote za umri. Dr. Masau please endeleza jambo hili. Pia tunamkumbusha Bwana Reginald Mengi kuhusu ile taasisi yake ya moyo ambayo ataipa jina la kijana wake Marehemu Rodney. Pia tunawapongeza wale wengine wote wanaojitolea kutoa msaada kwa Watanzania wasiojiweza kwenda India na kwingineko duniani. Mungu awabariki
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Shy hajakosea,nadhani alikuwa anamaanisha hii thread ingewekwa kwenye JF Dokta na sio jukwaa la siasa!
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  This is quite old kuifukua, haitusaidii.....ilishapitwa na wakati......just confusing people.....I just wanted to phone someone I know who has heart problems....kumbe issue ya 2008.......!

  Sipo ungeanzisha thread mpya...uweke maoni yako ukitolea mfano hiki kilichofanywa last year, kuliko kuifukua thread yote....inachanganya watu!
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa wenye matatizo ya Moyo.. huduma bure Dar
  Mzee Mwanakijiji[​IMG][​IMG] [​IMG] 17th October 2008, 04:03 PM

  Kaazi kwelix2
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Mods,iondolewe hii,inapotosha watu tu maana ni habari ya mwaka jana yawekwa leo hapa kwa ajili ya nini kama si kuchanganya watu.Kitakachotokea ni watu kukurupuka na kuanza kuwataarifu watu/ndugu/marafiki zao wenye matatizo ya Moyo na kuwataka waende THI kwa ajili ya huo uchunguzi wa BURE,watu watakimbilia THI na kuonekana hamnazo,baadae itaonekana source ya habari ni JF(What a shame)!!!!
   
Loading...