KWA WENYE KIU YA KUOLEWA

KWA WENYE KIU YA KUOLEWA

Abdul mrope

Member
Joined
Jul 6, 2017
Posts
37
Reaction score
79
KWA WENYE KIU YA KUOLEWA

Nikusaidie tu bure labda itakuponya kama wewe sio sikio la kufa. Kamwe usijitegeshe au kujinasisha mimba ili kumshika au kumlazimisha au kumkamata mwanaume unayemtaka akuoe. Mimba inakaa tumboni lakini penzi linakaa moyoni, kama hajakupenda tokea moyoni usidhani kilichokukaa tumboni kinaweza kumfanya akupende. Usijifariji kama akilazimika na kukubali kukaa na wewe sababu ya mtoto, kumbuka ipo tofauti ya kukaa na mtu na kuishi na mtu. Kawaulize wenzako waliojinasisha hivyo hivyo, leo wanalea watoto pekeyao, na wengine wako kama wanandoa vile ila wanajua fika moyoni mwao kuwa kinachowaunganisha ni mtoto tu. Kama mimba imejeuka kuwa mtego basi huyo jamaa atakuwa ni panya.
 
Back
Top Bottom