Ahead
JF-Expert Member
- Jan 11, 2013
- 2,258
- 2,521
Kwa niaba ya wakulima wenzangu tulio wilaya sumbawanga vijijini,naomba kuleta malalamiko yetu juu ya unyanyasaji wa kodi ya mazao i.e mpunga,mwaka jana tulilipa gunia la debe kumi sh 2000,ndani ya mwaka huohuo tukaambiwa tunatakiwa kulipa gunia la debe saba 2000 leo hii tar 11/06/2017 tukaambiwa gunia la debe sita 2000,na ikiwa ni siku mbili tu toka bajeti ya serikali imesomwa naomba sana utusaidie kuhusu swala hili hasa ukizingatia sisi ni wakulima ambao tunakumbana na changamoto nyingi ikiwemo tabia nchi na bei kubwa ya pembejeo,tumezuiliwa hapa Sumbawanga kwenye geti la myangalua na mtoza ushuru anaeitwa Bitu Sadi,najua nimefikisha kilio cha wanyonge mahali sahihi