KERO NRFA lipeni wakulima wa mahindi kwa wakati mwaka 2024/2025. Haya ni mateso na uonevu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

boyzia

Member
Aug 23, 2024
5
1
Habari, imekuwa tatizo, kero, usumbufu kwa wakulima wa mahindi nchini linapokuja suala la kuuza mahindi kwa wakala wa chakula NRFA kulipa fedha kwa wakati.

Waziri wa kilimo katika ziara ya Mh. Rais Samia kule Sumbawanga aliahidi kuwa kupitia wakala wa chakula NRFA watanunua mahindi kwa bei ya 700 kwa kilo na kulipa ndani ya wiki mbili.

Hali imekuwa tofauti hadi wakati huu mimi mdau na mkulima mdogo nimewauzia mahindi hapa kakozi Songwe sasa ni mwezi SIJALIPWA.

Ombi kwa waziri na wahusika nrfa, FUATILIENI NA LIPENI WAKULIMA KWA WAKATI HASA WALE WALIOTANGULIA.
 
Back
Top Bottom