Kwa wauzaji wa nguo za kiume

Kwa wauzaji wa nguo za kiume

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,099
Reaction score
12,928
Habari.

Wapi tunaweza kupata suti za kiume kwa ajili ya harusi kwa hapa Dar na bei zake zinakuwaje???
 
Mh, umetoka Katavi leo? Nenda posta Brandy House utapata suite maridadi kabisa...hapo ulipo ulizia gari za kwenda posta ni zipi na ushuke mwisho wa kituo.
 
Mh, umetoka Katavi leo? Nenda posta Brandy House utapata suite maridadi kabisa...hapo ulipo ulizia gari za kwenda posta ni zipi na ushuke mwisho wa kituo.
Ha ha ha haaah,,,,,,,ni mwenyeji kiasi. Nashukuru sana.
 
Nenda kwa sheria ngowi wetu. Suti bei reasonable kabisa, haizidi tzs milioni tatu.
#blame it on escrow
 
Unataka asiweke appointment apange foleni. Ukiingia hapo lazma akusomeshe hadi uelewe unatoaje toaje hiyo hela wakati kariakoo kwa 50,000 unapata mchina wa maana? Mteja mfalme pale lazma na kahawa ikuhusu na lecture ya sijui kitambaa kimefumwa na nzi wa chooni.


Watu wengine bora hela za escrow hazitupitii. Pata picha mie na Nyani Ngabu na rafiki yetu le mutu kubwa tungeziona zile hela? Tungetia mbwembwe aisee
Hahah...

Na hapo lazima aweke appointment kwanza...
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha haaah,,,,,,,ni mwenyeji kiasi. Nashukuru sana.

Mkuu pia Mwenge karibu na flats za jeshi kuna duka linaitwa Wedding Bells jaribu hapo...

Posta Mpya ground floor ya IT Plaza pia kuna duka kubwa tu la suti...

Kama mshiko hauruhusu basi hamia K'koo ukatafute 'Armani' za Guangzhou na Instabul...
 
Nenda kwa sheria ngowi wetu. Suti bei reasonable kabisa, haizidi tzs milioni tatu.
#blame it on escrow
Hiyo ndio bajeti ya harusi yote bibie, kuiweka katika suti yote hiyo ni kutojitendea haki.
 
Mkuu pia Mwenge karibu na flats za jeshi kuna duka linaitwa Wedding Bells jaribu hapo...

Posta Mpya ground floor ya IT Plaza pia kuna duka kubwa tu la suti...

Kama mshiko hauruhusu basi hamia K'koo ukatafute 'Armani' za Guangzhou na Instabul...

Nashukuru sana watu8, nitatembelea pande zote hizo.
 
Last edited by a moderator:
Hamna tembo huko katavi ukaongezea ongezea? Mwanaume mzima dili za escrow zinakupita kama umesimama? Hebu acha aibu, hela ya kachumbari hiyo baba
Hiyo ndio bajeti ya harusi yote bibie, kuiweka katika suti yote hiyo ni kutojitendea haki.
 
Hamna tembo huko katavi ukaongezea ongezea? Mwanaume mzima dili za escrow zinakupita kama umesimama? Hebu acha aibu, hela ya kachumbari hiyo baba
Tatizo wamebana kila njia, kama haupo mtandaoni katika madili hayo ya tembo basi utaozea jela......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom