Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,789
- 2,704
Habari zenu.
Leo nimeona niwashirikishe yale yaliyomo katika nafsi yangu.
Nitaandika kwa mtindo mgeuzo, yaani sio wa maji kufuata mkondo.
Mtunzi yoyote anaweza kuendeleza.
Shuka nayo--
Njia ilikuwa nyembamba, kila nilipojikaza kutaka kujipenyeza nilishindwa. Sasa niliona ule mlango wa kutoka nje ukianza kunibana, nilipumua mithili ya Kobe mzee, pumzi ilianza kuwa ndogo.
Nilijiuliza kwa nini ninaenda, nani aliyeniita. Hakuna aliyejitokeza kuniuliza maswali yangu.
Kulikuwa na giza zito mule ndani, giza lililoshahibizwa na joto, Mara kwa Mara hewa kutoka katika ule mlango ilikuwa ikiingia kuja kule niliko, kiukweli nilitamani kutoka nje.
Nilijilazimisha kutoka lakini Mara zote niliishia kutoa kichwa mlangoni kisha kurudi ndani, kichwa kilipulizwa na hewa ya nje ambapo muda wote nilitamani kutoka.
Hapo hapo nikapoteza fahamu.
******************
Harakati ziliendelea nyumbani kwa Mzee Donald, harakati za kuhakikisha Mke wa Mzee Donald anajifungua Salama.
Mzee Donald muda wote alikuwa akizunguka zunguka kama beberu liliofungiwa lisiingie ndani kwa majike. Alikuwa anawasiwasi ya mke wake kipenzi Neema, Mwanamke aliyempenda kuliko kitu chochote.
Jasho lilimtoka kwa wasiwasi uliokunja vishikizo vya moyo wake, Mara kwa Mara alisikika akisema " Eee Mungu Msaidie Mke Wang"
Wamama wawili waliovalia kanga nyeusi walitoka wakiwa wenye nyuso za kukata tamaa hali iliyozidisha hofu kwa mzee Donald.
" Vipi amekufa?"
Mzee Donald aliuliza huku akitweta.
"Hapana Mzee Donald, wala usihofu mke wako atajifungua salama, Ila kuna tatizo..."
"Tatizo..!! tatizo gani tena Mungu wangu?"
Mzee Donald alikuwa kama mtu aliyepagawa.
"Mkeo hata jifungua salama"
"Hata Jifungua salam.."
" Mtoto anahitaji Ngoma ya Lugwadu"
Bibi kikongwe aliyekuwa anatoka kutoka ndani alimkatisha Mzee Donald na sauti yake ya kukwaruza.
Ngoma ya Lugwadu hupigwa kwa wamama ambao watoto wamekataa kutoka. Katika kijiji hichi huamini kuwa watoto waliokataa kutoka kipindi cha kujifungua hutaka shughuli maalumu ya kiutamaduni ambayo ni Ngoma ya Lugwadu.
Kwa haraka wapiga ngoma ya lugwadu waliwasili, majungu ya pombe na chungu kidogo chenye damu ya Bundi kilikuwa kimebebwa na yule bibi kizee.
Damu ya bundi hutumika katika kusafisha kitovu cha mtoto atakayezaliwa, pia huwekewa katika utosi mpaka mtoto atakapofikisha siku thelasini na sita.
Ngoma zikaanza kupigwa kwa ustadi mkubwa, watu wakicheza kama wapunga pepo.
Chumbani Mke wa Mzee Donald uchungu ulizidi kumpata, Mara mtoto akazaliwa.
Alikuwa mtoto wa Kiume, Mke wa mzee Donald alikuwa amechoka kikamilifu, hakuweza kufanya lolote zaidi ya kupitiwa na Usingizi.
Mtoto aliyezaliwa alikuwa kimya saana hali iliyoleta wasiwasi kwa wakunga.
Wakamuandaa vizuri kwa kumpaka ile damu kwenye kitovu. Kisha yule Bibi kikongwe akaoongea;
" Shiri siki kiri firi"
Mara mtoto ghafla akapiga Chafya. Muda Wote huko nje Ngoma ya Lugwadu ilikuwa ikichezwa.
Mtoto akatolewa nje kwenye ngoma kama mila yao itakavyo.
************
Kelele za ngoma ndizo zilizorejesha fahamu zangu, vumbi la eneo lile lilinifanya nipige Chafya.
Mtunzi no.01
Yoyote anaweza kuiendeleza.