Kwa watu wa mkoa wa Mara

[/COLOR]

Nimewasoma. Yote ni heri ila hilo hapo juu la katiba ya ubaguzi wa kuwabagua wasio vijana halitatuvusha! Liangalie upya wewe mwenye katiba yako.
Hayo ni mawazo yako,yaani una maana kuwa na umoja wa vijana ni kubagua wazee?kuna mtu kawakataza kuwa na umoja?kuna uvccm na bavicha, mbona wazee wa ccm na cdm hawajalalamika.Au ulimaanisha nini? au unashauri nini?
 
Nitafute tata kwenye 0782 577 006 tuongee mustakabari wa mkoa wetu.
 
jamani naona tatizo siyo ukabila ila ni uzalendo kwa hawa viongozi wetu Hebu fikirieni wakati wa PM msuya, Mr mgonja, kwa ufupi waliyowafanyia wachaga wenzao msuya kapeleka Lami hadi marangu cheki Mgonja alivyoiboresha Rombo sie tulikuwa na majenerali wangapi tumewahi kuwa na PM sasa hivi tunao viongozi wangapi wa ngazi za juu ambao wanaushawishi kabisa wawa kuweza kufanya mambo kila m2 akakubali tunae waziri na katibu mkuu wa nishati na madini lakini mkoa wa Mara umeme vijijini ni tatizo tujifunze kwa ngeleja alivyowapatia wana Sengerema umeme vijijini nafikiri Mkoa wa Jimbo maskini kuliko yote ni Jimbo langu la M mwibara jimbo hili jimbo linabahati ya kuwa karibu na mwambao wa ziwa na wakazi wake wakubwa ni wavuvi lakini tatizo ni ubinafsi wa viongozi wetu mikopo itolewayo haina tija kwa wao lakini kungekuwepo uwezekano mabeenki yakawakopesha hawa watu mashine za uvuvi kama wanavyokopeshwa wakulima hizi power tila nafikiri mvuvi angejikomboa lakini wao hilo hawalioni na kuna uwezekano mkubwa sana mabenki kuleta vitu kama hivyo serikali ikaweka mkono wake wavuvi wakapewa hizo mashine lakini tatizo linabaki pale la UBINAFSI wala siyo ukabila kama wengine wanavyoaminiy
 
Post yako nimeisoma na nimeilelewa lakini siyo katika ufahamu ule ambao nilkihitaji kuelewa Napata shida kidogo katika post yako naona kama imeegemea upande wa kisiasa zaidi kwangu mimi naoana kama ni post inayofanana na zile za wanasiasa ambao huzitumia katika kuomba ridhaa ya kuongoza wananchi katika nyanja fulani Sina maana ya kuwa wewe ni mwanasiasa la hasha ila ukweli unaujua wewe binafsi Mimi mwenyewe napata shida kubwa kabisa kuelewa ni kwa nini mkao wetu kila kukicha ndo unazidi kurudi nyuma nilikuwepo mwaka huu baada ya miaka kadhaa kuwa nje ya mkoa lakini yale niliyoyaacha hayapo tena na hakuna dalili ya kurejea tena Hapa suala siyo kumtegemea kongozi ajaye sisi wenyewe ni viongozi hebu fikiria kama kweli mtu unakata miti kwa kuchoma mkaa je hapa kiongozi wa nini na kati anajua ni nini madhara yake hapo baadaye Haya ni maoni yangu tu
 
Mm sio mwana Mara ila nawashauri kitu kimoja, msikubali kuwa Chagga_body guards. Sifa za kijinga zimewatawala.
 

Jambo lolote linalohusu mustakabari wa watu,huwezi kuliepusha na siasa,au labda hujui maana ya siasa.Siasa ni maisha ya kila siku ya mwanadamu(MAISHA YOTE YAMETAWALIWA NA SIASA),Siasa kama field nyingine ambayo ni ya kweli inafanywa kisayansi.Sikiliza hii stori,wakati nilipokuwa mdogo,kuna bwana mmoja jirani yetu aliitwa Gregory,huyu bwana alikuwa na sifa ya urafi(kupenda kula kupita kiasi),watu wengi wakamchukia sana,akapoteza heshima mbele za watu na watu wote wanaomfahamu wameshindwa kuwapa watoto wao wanobatizwa jina la Gregory,je unafikiri ni kwa sababu ya jina baya au tabia ya mwenye jina?vivyo hivyo kwa siasa,wanasiasa ndo wabovu.Na ndio maana nimekwambia kuwa wanasiasa wametufikisha hapo tulipo na sio siasa.Lakini pia kama jambo hili nitalifanya bila kujali maneno kama yako.Siwezi kuacha nia yangu njema eti kwa sababu tu umesema nimeongea kama wanasiasa.Naomba uniunge mkono tuijenge MARA yetu.
 
ni kweli tata makao makuu yanatakiwa kuwa mugumu . by all standards mie sio mbaguzi na Mungu apishie mbali nisiwe mbaguzi lakini kiukweli roho huwa inaniuma sana ninapoona wanaofaidika na mbuga ya serengeti sio wazawa wa serengeti na mkoa wa mara kwa ujumla! anyway the end is near, I can not see the change, but I can smell it!
 
Aksante sana mleta hoja.
Dhamira ya dhati pamoja na kusimamia na kutekeleza dhamira yenyewe ndiyo msingi wa mabaliko.
Vijana wa Mara wanaweza kuleta mabadiliko sana kama wakiamua.
Jambo la kwanza la kuanzia ni kuachana na mambo ya ukabila na ushabiki wake then wafocus kwenye vitu vya maendeleo. Coz hata kwenye huu uzi naona baadhi ya watu wameanza kutiririka kwa kiluga utadhani Mkoa wote wa mara ni wa Kabila moja.
Narudia kusema, Kama mleta hoja na wachangiaji wenye interest na mkoa wa mara wanataka mabadiliko ya kweli
inabidi elements zote za kikabila na kikoo zisiruhusiwe kabisa. then watu waangalie kinachowaunganisha zaidi ndiyo kipewa kipaumbele.
 
Asante bwana ka-rabbit,tupo pamoja sana,kwa mabadiliko tuwasiliane kwa namba 0782577006
 
Tata hiyo umenena kabisa
 
Mkuu naona huu uzi ni WA Muda kidogo lakini bado uko hai. Kweli Mkuu SAGANKA naunga hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…