Kwa Watanzania mnaoendelea kughiribiwa na Lowassa

Kwa Watanzania mnaoendelea kughiribiwa na Lowassa

Ndio maana Watanzania wanataka kukiondoa chama hiki cha kijani kilicholea ufisadi wa kutisha nchini kiasi cha kuruhusu huyu mgombea anayedaiwa kununua watu ili waende kwenye mikutano yake.

Chama hiki twawala kimefanya nini kumzuia huyu mtu na wengine asiendelee kufanya hivyo? Chama kilichukua hatua gani kumzuia Kinana na Nape kukusanya watu kwa malori kuhudhuria mikutano yao kipindi kile wanazunguka nchi nzima?
 
Wewe umewahi kupokea Tsh. Ngapi kutoka kwa Lowasa?
Maana tusiwaaminishe wananchi matakwa yetu tuwe wawazi jamani.
Penye ukweli tuwe wakweli huwezi kusema anatoa pesa wakati haujawahi kupokea.

Rudia na usome vizur andiko langu majibu yapo humo
 
muhindo

yani kwakumkabidhi EL bendera ya UKWA hii hoja ya kupingana na ufasadi haina mashiko kamwe kwani mliomtuhumu fisadi huku Dr Sl.aa akijinasibu kwamba anaushahidi leo ndio raisi wenu,tafuta hoja nyingine hii yakupambana na ufisadi mmeshaizika wenyewe kwa mroho wa mtonyo wa mwenyekiti
 
Last edited by a moderator:
mimi nimeshawaelewa wa Tanzania...inavyoonekana hata leo hii Magufuli akihamia UKAWA tunampa nchi...yaonekana hatuna shida na record ya mgombea binafsi....wengi wanataka tu CCM itoke....Magufuli ni mgombea sahihi kabisa kosa lake kubwa ni kwamba anatokea CCM.
...so tatizo sio Lowassa ..tatizo ni CCM kama chama ndo watu hawakitaki

kweli kabisa
 
Wananunuliwa mafuta wajaze kwenye bodaboda zao nchi nzima
 
Ndio maana Watanzania wanataka kukiondoa chama hiki cha kijani kilicholea ufisadi wa kutisha nchini kiasi cha kuruhusu huyu mgombea anayedaiwa kununua watu ili waende kwenye mikutano yake.

Chama hiki twawala kimefanya nini kumzuia huyu mtu na wengine asiendelee kufanya hivyo? Chama kilichukua hatua gani kumzuia Kinana na Nape kukusanya watu kwa malori kuhudhuria mikutano yao kipindi kile wanazunguka nchi nzima?
 
Kishaelaza mara nyingi, pesa inatoka kwa rafiki zake wenye huruma sana kwa mtanzania.
Watanzania tulivyo waajabu kauli zake hizo wala hutuzishtukii!! Hakuna anaye hoji hizo fedha atazirudisha kutoka wapi na kwa njia gani?

Tangu lini wafanya biashara na mafisadi papa wakawa na huruma kwa walala hoi? Hao ma King maker shida yao nikutaka kumuweka madarakani mtu ambaye watakuwa wanamuendesha puta kwa wakitumia remote hatujiulizi kwa nini Rais Nyerere alikuwa mbali nao!

Sina hakika kama Mh.Lowassa hajui kwamba kundi hilo linamchota akili tu ili mwisho siku atumike kama daraja la kusaidia kuvamia vitalu vyote vya gesi ,mafuta na migodi ya madini, watajimilikisha kila kitu mpaka mbuga za wanyama,mswahili wa kawaida atatia pua yake pale.

Watanzania tuwe makini na Viongozi wanaotegemea wafanya biashara kugharimia ndoto zao za kwenda IKULU tusikubali Taifa letu kurudishwa back to STONE AGE.
 
mimi nimeshawaelewa wa Tanzania...inavyoonekana hata leo hii Magufuli akihamia UKAWA tunampa nchi...yaonekana hatuna shida na record ya mgombea binafsi....wengi wanataka tu CCM itoke....Magufuli ni mgombea sahihi kabisa kosa lake kubwa ni kwamba anatokea CCM....so tatizo sio Lowassa ..tatizo ni CCM kama chama ndo watu hawakitaki

Umemaliza kila kitu ndg!
 
Moja kati ya technique kubwa ya EL ni kununua watu kwa makundi pamoja na media ambazo zitasaidia kupeleka ujumbe tena uliowekwa chumvi kwa wananchi kwamba yeye ni kipenzi cha Watz.

Tulianza kushuhudia hili tangu alipokua bado ana sare za kijani, makundi yaliyoghiribiwa yanafika kwa EL pasipo taarifa lakini cha kushangaza utakuta media tayari zipo eneo la tukio kabla hata haya makundi kufika zikiwa tayari zimejipanga kurusha matangazo. Tunaongopewa eti vijana wa bodaboda wemetoka Simiyu wakiendesha pikipiki kuja nyumbani kwa EL Dodoma kumuomba awanie urais, hii ni ishara kwamba hiki ni kiini macho.

Sote ni mashahidi, mkutano wa kwanza wa arusha EL alisafirisha watu kutoka kila kona ya TZ kwa gharama kubwa, mfano wapo waliokatiwa tiketi za ndege ili tu kutengeneza kiini macho kwamba yeye ni kipenzi cha watu.

Nina rafiki yangu yeye kwa mara ya kwanza kupanda ndege ilikua ni mkutano wa Arusha kwa hisani ya Mmasai. Asilimia kubwa ya mabasi yalikodiwa na EL kuelekea Arusha ili kutengeneza umati kutengeneza hiki kiini macho.

Leo tunashuhudia usafiri wowote ukikubali kuwa kwenye maandamano ya mapokezi yake mafuta ni bure, hii iwe ni bodaboda au magari.

Kweli pesa zilizopatika pasipo jasho lolote hutumika hovyo, leo tunafurahi ila hizi ni pesa zetu wenyewe zinatumika kutuzubaisha.

Kweli wanaomshabika EL aidha hufuata mkumbo au kutafuna hizi pesa zake ila swali la kwanza la kujiuliza ni wapi hizi pesa zimepatikana?

akili za mbwa jike akiwa kwenye heat
 
Jamani tuwe wakweli, Next Level angewezaje kununu wat maelfu waliojitokeza kumpokea Dar na Mbeya na Arusha leo? Kama NL anaweza akawajaza mapesa watanzania mamilioni tulio na nia ya dhati ya kumpigia kura, hakika yeye ndio anayetufaa kuwa Raisi wetu. CCM wabinafsi mnakula nchi wenyewe.

Tusaidiane kushangaa mkuu. Ila trip hii wataisoma no. Wamewaamsha wenyewe wananchi hasa huko vijijini kwakuwapandishia nishati yao mafuta ya taa bei kisa waliogopa kuwakamata wachakachuaji ambao nimaswahiba zao. Wasitafue mchawi, niwao weeeenyewe.
 
ccm ndio iliyozalisha rushwa na ufisadi, ni jiko linalopika na kuandaa ufisadi. kisha leo plepole anataka kuhadaa watanzania eti ccm na magufuli hawana ufisadi anajipotezea mate na energy. watanzania tunafahamu kila kitu. tulimtaja jk ktk list of shame na bado polepole hakuzungumza, ccm hiyoyo ituambie rizwn amepata wapi huo ubilionea wakati naye ana degree moja kama watoto wa walala hoi,aliajiliwa wapi penye mshahara wa basic salary bilion 1. kama sio mfumo uleule wa ccm umemtajilisha mtoto wa jk. polepole anatafuta madalaka kama aliyopewa yule bwana aliyemrukia na kumpa kichapo mze warioba leo tunaona ni mkuu wa wilaya. kwahiyo hata polepole hawezi achana na mfumo ccm sababu anauchu na kuwa bilionea

Haswaaaaa mkuu!! Watwambie Ikuru imefanyika biashara gani mpk hawa maskini wenzetu kina Jk nawatoto wake leo nimatajiri wakutisha????.

Vilevile huyo magufuli, hizo bilioni 254 alizoiba na CAG akagundua, anazirudisha lini?! Aturudishie hela zetu jamani! MAGUFULI RUDISHA HELA ZETU HATUKUBALIIII!!

Vilevile zilenyumba zetu walizogawiana nakutusababishia hasara kibwa, watumishi wengi leo wanaishi mahotelini nasisi watanzania ndotunabeba msalaba wakuwalipia hayo mabilioni kisa Magufuli kauza nyumba zetu. MAGUFULI RUDISHA NYUMBA ZETUUU!! HATUKUBALI MWAKA HUU, HATUKUBALIIII!!
 
hatuna tatizo na fedha zake muache agawe ,si zake we kinakuuma nini,tafuta za kwako gawa,na ukiambiwa toa ushaidi hauna,zaid ya maneno ya kusikia,tutampiigia kura kumwezesha kwenda ikulu kuliko kukiipa ccm kimeshindwa miaka 38,tunahitaji mabadiliko
 
mkuu ukawa wangeweka hata kinyesi tungechagua kinyesi.huu ni mwaka wahasira za watz na si mwaka wa uchaguzi.maana tumechoka na watu kumwagiwa tundikali kuondolewa meno na macho.nknknk
 
Moja kati ya technique kubwa ya EL ni kununua watu kwa makundi pamoja na media ambazo zitasaidia kupeleka ujumbe tena uliowekwa chumvi kwa wananchi kwamba yeye ni kipenzi cha Watz.

Tulianza kushuhudia hili tangu alipokua bado ana sare za kijani, makundi yaliyoghiribiwa yanafika kwa EL pasipo taarifa lakini cha kushangaza utakuta media tayari zipo eneo la tukio kabla hata haya makundi kufika zikiwa tayari zimejipanga kurusha matangazo. Tunaongopewa eti vijana wa bodaboda wemetoka Simiyu wakiendesha pikipiki kuja nyumbani kwa EL Dodoma kumuomba awanie urais, hii ni ishara kwamba hiki ni kiini macho.

Sote ni mashahidi, mkutano wa kwanza wa arusha EL alisafirisha watu kutoka kila kona ya TZ kwa gharama kubwa, mfano wapo waliokatiwa tiketi za ndege ili tu kutengeneza kiini macho kwamba yeye ni kipenzi cha watu.

Nina rafiki yangu yeye kwa mara ya kwanza kupanda ndege ilikua ni mkutano wa Arusha kwa hisani ya Mmasai. Asilimia kubwa ya mabasi yalikodiwa na EL kuelekea Arusha ili kutengeneza umati kutengeneza hiki kiini macho.

Leo tunashuhudia usafiri wowote ukikubali kuwa kwenye maandamano ya mapokezi yake mafuta ni bure, hii iwe ni bodaboda au magari.

Kweli pesa zilizopatika pasipo jasho lolote hutumika hovyo, leo tunafurahi ila hizi ni pesa zetu wenyewe zinatumika kutuzubaisha.

Kweli wanaomshabika EL aidha hufuata mkumbo au kutafuna hizi pesa zake ila swali la kwanza la kujiuliza ni wapi hizi pesa zimepatikana?

Ni pesa za Tembo wa nchi hii. Ni pesa za Epa na Kagoda. Ni pesa za Lumbesa toka Stanbic. Ni pesa za ubadhirifu toka wizara ya Magufuli. Ni pesa za Meremeta na Deep Green. Lakini giliba ya ccm kwa miaka 50 ndio mbaya zaidi. Mwisho wenu haukwepeki. Mtaondoka kwa aibu!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
magufuli anafarijika ICU akiona kumbe bado anavijana wanampigania
 
CCM wanalia sana sasa hivi kwa sababu Lowasa anafanya kile walichokua wanafanya wao.Nyie sasa kinawauma nini si tuaubiri tarehe 25 october ili tuone.Kwa nini sasa kila thread ni Lowasa anzisheni za.magufuli basi mnampa promo Lowasa bila kujijua
 
HEBU FIKIRIA MARA MBILI HAYA YAFUATAYO
1.Katiba bora kabisa ilikwamishwa na nani?? kumbuka iliandaliwa na wana CCM mahiri kina Warioba,
2.Mipesa(350BILIONI)nani waliokuwa wanawatetea wezi na majambazi waliobeba fedha kwenye VIROBA
3.Kivuko cha kwenda BAGAMOYO inakuwaje dude lile chakavu linakuwa na bei kubwa kuliko boti ya kisasa
kabisa ya AZAM????Nani aliyesimamia hii kitu na kuiteteta bungeni
4.EPA,GREENFINANCE,Upotevu wa mabilioni wizara ya Ujenzi(rejea ripoti ya CAG) etc

Wananchi wangepata maendeleo kiasi gani kama watetezi pale bungeni wangejali maslahi ya wanchi kuliko hili dude linalokumbatia majambazi??? NO!!! NO!!! VOTE FOR UKAWAni mwendawazimu pekee anayeweza kuirudisha rangi ya kijani pale ikulu
Binafsi nimekataa kufuata mkumbo, naiandaa kura yangu kumkwamisha fisadi el asikanyage magogoni.
 
Back
Top Bottom