Moja kati ya technique kubwa ya EL ni kununua watu kwa makundi pamoja na media ambazo zitasaidia kupeleka ujumbe tena uliowekwa chumvi kwa wananchi kwamba yeye ni kipenzi cha Watz.
Tulianza kushuhudia hili tangu alipokua bado ana sare za kijani, makundi yaliyoghiribiwa yanafika kwa EL pasipo taarifa lakini cha kushangaza utakuta media tayari zipo eneo la tukio kabla hata haya makundi kufika zikiwa tayari zimejipanga kurusha matangazo. Tunaongopewa eti vijana wa bodaboda wemetoka Simiyu wakiendesha pikipiki kuja nyumbani kwa EL Dodoma kumuomba awanie urais, hii ni ishara kwamba hiki ni kiini macho.
Sote ni mashahidi, mkutano wa kwanza wa arusha EL alisafirisha watu kutoka kila kona ya TZ kwa gharama kubwa, mfano wapo waliokatiwa tiketi za ndege ili tu kutengeneza kiini macho kwamba yeye ni kipenzi cha watu.
Nina rafiki yangu yeye kwa mara ya kwanza kupanda ndege ilikua ni mkutano wa Arusha kwa hisani ya Mmasai. Asilimia kubwa ya mabasi yalikodiwa na EL kuelekea Arusha ili kutengeneza umati kutengeneza hiki kiini macho.
Leo tunashuhudia usafiri wowote ukikubali kuwa kwenye maandamano ya mapokezi yake mafuta ni bure, hii iwe ni bodaboda au magari.
Kweli pesa zilizopatika pasipo jasho lolote hutumika hovyo, leo tunafurahi ila hizi ni pesa zetu wenyewe zinatumika kutuzubaisha.
Kweli wanaomshabika EL aidha hufuata mkumbo au kutafuna hizi pesa zake ila swali la kwanza la kujiuliza ni wapi hizi pesa zimepatikana?
Hizo ngonjera wengi wamezichoka lililoke mbele yetu ni 2015.10.25 hivi hizo pesa anazogawa EDO je serikali imebakI na hela KWELI maana tunaambiwa deni la taifa kila mtanzania aliyeko hai anadaiwa 600,000/ + je TRA wanapata kodi stahiki kwenye mgao huo sidhani kama kuna mwananchi ataelewa hizo mbwembwe za kuwa watu wanagawiwa pesa jamani kumben Ndiomaana babu wa loliondo alikumbwa na mafuriko ya wanya kikombe Tunataka MAGEUZI ilitupate fursa ya kufanya MABADILIKO chama cha zamani hakiwezi kazi hiyo EDO kama alivyo ANATOSHA