Safari hii hatudanganyiki siku zote tangu tumeanza kuwachagua CCM hawajawahi kutuambia hata siku moja kuwa mchagueni mgombea wetu kwa kuwa ni mwizi na mnyang'anyi.
Siku zote CCM wamekuwa wakituhadaa kwa kutuambia kuwa mchagueni mgombea wetu kwa kuwa ni mtu safi mpole,ni mtu wa watu,mchapa kazi,ana penda watu,muadilifu na sifa nyingi nzurinzuri na hawajawahi kusema hata siku moja kuwa mgombea wao ni mwizi.
Wananchi tunapozikubali hadaa hizo za CCM na kumchagua mgombea wao walietuaminisha kwa sifa nyingi nzuri matokeo yake tunaibiwa na hata tunapopiga kelele hakuna anayetusaidia.
Safari hii ni bora tumchague mtuhumiwa mwenye sifa mbaya ambaye wizi wake na ufisadi wake haujathibitishwa,kwa kuwa tunajua kuwa iko siku moja kama ni kweli alikuwa fisadi na kama hajaacha ufisadi wake na wizi wake atakuja kubadilika na kuacha ufisadi na wizi wake.
Kuliko kumchagua mtu ambaye tumeaminishwa kuwa ni mtu safi,ni muadilifu,mcha mungu,siyo mwizi,siyo fisadi na mchapa kazi,akienda msalani ana toa dhahabu tupu tofauti na binadamu wenzake.
Tukisha mchagua ana badilika na kuwa tofauti kabisa na jinsi tulivyoaminishwa,ana kuwa mwizi na fisadi hata kumzidi kibaka wa kila siku na hata tukipiga kelele kuwa tunaibiwa hakuna anaye tusikiliza wala kutusaidia wanasubiri uchaguzi mwingine uje waje na hadaa zingine tena.Safar hii hatudanganyiki.