Kwa wataalam wa solar power msaada tafadhar.

alet

Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
81
Reaction score
62
Wasalaam wana Jf..
solar charger inaonyesha iki chaji betri hata usiku wa manane.
nimejaribu kufungua nyaya za kutoka kwenye solar panel hadi kwenye solar charger haijabadilisha kitu.
nini tatizo hapo wataalamu?
 
Check charge controller kabla ya mambo yote.

Ninashukuru, ndugu yangu kwani charger controller na solar charger si ni hiyo hiyo moja au ni vitu viwili tofauti? samahani mimi sio mtaalam wa solar.
 
ninashukuru, ndugu yangu kwani charger controller na solar charger si ni hiyo hiyo moja au ni vitu viwili tofauti? Samahani mimi sio mtaalam wa solar.

mkuu tatizo ni nini hasa?fafanua nikusaidie maana natumia umeme jua
 
ni hivi mkuu ile indicator inayoonyesha solar charger ikichaji siku hizi inakua on muda wote hata usiku tofauti na kipindi cha mwanzo ambapo usiku ilikua ikizima.
 
Imekufa hiyo, badili kabla ya kuua betri kwani kinachofanyika hapo charge inahama kwenye Betri kwenda kwenye solar pannel.
 
Wakati wa kufunga charger controller hakikisha inalingana na nguvu ya solar.usije weka yenye ampier ndogo wakati solar ina watt kubwa.kwahiyo hainisha una solar ya watt ngap tukusaidie
 
panel ina 175W na solar controller ina 20A. vipi mkuu hapo kuna kosa lilifanyika?
 
Wati 120/Voti 12 utapata ampia 10. Hivyo chaja kontrola yako ya ampia 20 shwari kabisa. Hata nashauri ungepata chaja kontrola ya hali ya juu kidogo aina ya MPPT.
 
hiyo MPPT nina ipata wap mkuu?
 
Wati 120/Voti 12 utapata ampia 10. Hivyo chaja kontrola yako ya ampia 20 shwari kabisa. Hata nashauri ungepata chaja kontrola ya hali ya juu kidogo aina ya MPPT.

pannel ina 175W 24V hapo hiyo MPPT inafaa?
 
175w/24v utapata ampia toka kwenye vioo vyako. Maelezo ya MPPT ni magumu kidogo kwa kiswahili chetu lakini kifupi ni kwamba kwa kontrola za kawaida tunapoteza karibu asilimia 30 hivi ya kiasi Cha umeme unaozalishwa na vioo. Uko wapi kimkoa?
 
nipo Makambako mkoani Njombe.
 
Dar zaweza kupatikana, lakini nafikiri si busara unapotajiwa kitu basi Mara hiyo utake kukinunua. Ni vizuri ufanye utafiti wa kina, ujue utendaji kazi wake, gharama, faida na hasara nk na ndipo uamue kununua au kutonunua. Kesho nitakuwA Rujewa, kama utakuwa na nafasi tupange tukutane Igawa. Nirushie namba yako ya simu.
 
aisee! kesho ninasafari ya kuja Rujewa kuanzia saa 8 hivi nitakuwepo hapo.
 
Back
Top Bottom