Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Status
Not open for further replies.
Je unajua kwa nini watu wanampenda Magufuli ni kwa sababu ya utendaji wake na hii ni tofauti na JK alivyoingia kwani mimi binafsi sikujua utendaji wa JK akiwa kama waziri zaidi ya kusaidiwa na promise ya baba wa taifa, kwa mtoa mada anachokisema ni mapungufu ambayo yapo kwa walio wengi na kwa uzoefu wangu kwenye majimbo ya kagera kuna fitna za chinichini nyingi sana na ukimshinda mtu ugonvi hauishi mpaka unazikwa si kwa Magufuli tu uliza bukoba mjini na kwingineko, mtafute Lwakatare akuambia yanayojili huko, hayo ndio mapungufu ya kagera ila tunahitaji kuyatafutia ufumbuzi
 
Lowassa, Rostam, Karamagi,Kikwete,Chenge hawa woote hawafai na ndio wameifikisha nchi kwenye umasikini kama huu na wote ni mabingwa wa visasi, we acha hizo bana.Magufuli anafaa namshauri ajiunge cdm kwa wapiganaji
 
Tuhuma zaweza kuwa kweli au chuki binafsi. Lakini mkubwa ulikuwa wapi muda wote huo,au ndio njama za kumwangusha huyu jasiri na mtendaji ktk chama chenye tuhuma ya kuwa na fisadi wengi?

Habari yako imeegemea upande wa udhaif u tu nadhani una hisi uzuri wa pombe unafahamika, ingekuwa vema ukaeleza na uzuri wake ili wana jf tuweze kupima pande zake zote mbili kikamilifu.
 
sawa mkuu tunakupongeza kwa jitihada zako za kutupa ukweli unaoujua kuhusu Dr Magufuli,siwezi udharau huu ujumbe wako hata kama umeutoa mapema kabla bwana magufuli hajasema kuwa anampango wa kugombea Urais.
Pia unuzuii mimi kufikiria zaidi ya hapo ulipo fikia,huu utabaki kuwa ufahamu wako wewe na hao walio nyuma yako.Asante mungu akujalie afya tele.
 
Wakati wa uchaguzi mdogo wa Biharamulo, vihoteli vya Bi'mulo vyote vilikuwa vimejaa, tukalazimika kulala Chato kwenye bonge la hoteli la multi millions!, guess ni la nani?.

kwanini tu 'guess' Pasco si tutakuwa tunaendeleza majungu kwa nini usimtaje kama unataarifa sahihi
 
Yes uchambuzi huu umejaaa hoja.

Moja ya kitu kinachokera ni serikali kuwadanyana wanachi kuwa kugawanya majimbo au wilaya na hata mikoa ni njia ya kuwaletea maendeleo kumbe ukweli Kuongeza idadi ya majimbo wilaya au mikoa ni kuwaneemesha watu wachache tu.

Magufuli ni kiongozi mzuri lakini mangufuli ana mapungufu yake. na ukubwa na tatizo lamapungufu yake haliwezi kuwa na dawa ndani ya CCM. Tatizo ni CCM wote wanajua Sanaa zao hatawale wenye nafuu nao wanazidi kwenda kushoto.

TUmsbiri na Anna Tibaijuka naye wa huko kagera. naye anapikwa. 5 years to come tutasikia kaiva kwenye kufanya madudu.

Wao wanasema collective responsibility

 
Usiwe unafata upepo tu! Usitake aminisha umma kuwa CCM wote hawafai! Kuna wachache walau wanaweza ! Magufuli ni mmoja wapo

mimi sifuati upepo! Kama Magufuli anafaa kuwa raisi hata Lowassa anafaa kuwa raisi kwa mtazamo wako. Mtu anayetaka simpathy ya wananchi kupitia media ndo unamuona bora? Magufuli hafai kuongoza nchi huu ndio ukweli!
 
Mkuu Buzwagi haipo Biharamuro, au mi nimepoteza kumbukumbu! lakini hapana nimefanya interview hapo mara mbili najua iko kahama. hayo mengine yawezekana yapo na siyo kwa Dr Magufuli ila ni mtindo wa CCM wengi niseme karibu 90% ya wabunge wanafanya hizo mbinu. Maoni yangu, CCM hawatakiwi Tanzania bara.

hajasema Buzwagi mkuu amesema Tulawaka.
 
Kama hayo yanayosemwa hapo against huyu Bwana Magufuli ni kweli basi it is quite obvious kuwa huyu bwana ni mtu hatari sana! Hafai hata kuwa Waziri! CCM itatakiwa kuwa makini sana mwaka 2015 kuzuia watu kama hawa kufikiriwa kuwa possible candidates wa Urais.
 
Mbona sisi watu wa bara tunapenda sana kujiona tunafaa zaidi kuwa marais wa jamhuri ya muungano wa tz. Ningependa jf ijikite na kuiangalia znz na +contenders.......
 
Wewe ndiyo mleta porojo hapo usizuie watu kupata taarifa acha watu wapate taarifa fanyia kazi habari hizo ndiyo useme maneno yako otherwise utakuwa hauna maana yeyote mimi sileti habari hizi kishabiki kama ulivyo nenda biharamulo kauliza haya fuatilia hayo halafu ndiyo uje unasema ni porojo mtu mwenye hekima hakurupuki asikiapo jambo hufanyia kazi jifunze hilo utaheshimika

kaka unachanganya habari, hebu reply with quote tujue unamjibu nani
 
Haya ni madai ya muda mrefu na yamekuwa yakitolewa na watu wa Biharamulo dhidi ya Magufuli, huenda kuna ukweli. Lakini licha ya mapungufu yote hayo, jamaa bado anaweza tukilinganisha na wengine waliopo katika chama chao..
 
Kwanza nshakupa Thanks kwa kuwakilisha, in short hakuna mtu anayeijua ccm kama ccm wenyewe, sasa Sophia Simba alishasema wote wameoza Magufuli included, lakini Mr Pombe ni angalau kuliko wengine wote, unaona anateuliwa mtu kama pinda unasema huyu atakuwa afadhali kuliko hawa wengine kumbe hana manufaa yeyote ni msanii tuu, tunataka kiongozi anayetenda na ukimuona unajua anamaanisha anachokisema. Wote hawafai ila yeye ana unafuu, hebu angalia inafikia stage watu wanamkumbuka lowassa kwa utendaji kazi wake wanasahau kitu muhimu kwamba yeye ni fisadi wa kutupwa! Bora Magufuli kazi anafanya na inaonekana ingawa my take angefaa zaidi kuwa waziri mkuu kuliko kuwa Rais.
 
Mbona sisi watu wa bara tunapenda sana kujiona tunafaa zaidi kuwa marais wa jamhuri ya muungano wa tz. Ningependa jf ijikite na kuiangalia znz na +contenders.......
Ni akina nani wa Zanzibar ambao wanategemewa kugombea urais?? Anzisha hiyo mijadala na wengine watachangia.
 
Magufuli siyo malaika. Kama binadamu lazima atakuwa na mapungufu na mazuri yake pia. Mtoa mada ameonyesha mapungufu ya Magufuli kama kiongozi. Ingekuwa vema zaidi kama kuna anayeyajua mazuri ya Mheshimiwa huyu ayamwage hapa ili tuweze kumweka vizuri kwenye mizani.
 
Mkuu kuna mengine umesahau amelitia hasara kubwa sana taifa kwa maamuzi yake ya jazba na yaubaguzi warangi,mfano hai nipale mwanza alivunja kituochamafuta cha mfanyabiashara wakihindi eti ni open area,jamaa akafungua mashtaka akashinda kesi akatakiwa alipwe bil.5 sasa wamempa eneokaribu lote laviwanja vya 7saba kumpoza,pia kazuia boti ziendazokasi mwanza to bukoba za lake express kwa chuki tu,watu mpk leo wanasumbuka usafiri kwa ubinafci wa magufuli hafai hata kwa udiwani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom