Kwa washauri wa JK tu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa washauri wa JK tu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kombati, Apr 6, 2012.

 1. kombati

  kombati Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tangu nimeanza kuijua na kuifuatilia siasa ya Tanzania na tangu nimemjua japo kidogo JAKAYA KIKWETE,haya ni baadhi ya maswali ambayo ningependa ayajibu kiukweli na kiuhalisia wala sio kisiasa. Ayajibu kama binadamu anayetambua kuwa kuna binadamu wengine wanaotaabika sababu ya tabasamu lake na ukimya wake katika mengi ya mambo ambayo yanahitaji maamuzi yake

  1. kuna nini kipo nyuma ya pazia katika kesi yaNguza Viking na mwanae Papii Kocha?..katika hali ya kawaida sio rahisi baba na mwanae kuwabaka kwa zamu watoto kama walivyotuhumiwa na hatimaye kuhukumiwa.
  2. Unaijua kampuni ya Dalbit?
  3. jengo la ghorofa linalojengwa mkabala na ofisi za manispaa ya Iringa mmiliki wake ni nani? Ridhiwani?
  4. Ni nini kilichokuporomosha toka 82% mwaka 2005 mpaka 61% 2010 ikiwa umetekeleza ilani na ahadi za chama chako?
  5. Unajua ni kwanini Mwalimu Nyerere aliwakataa wewe pamoja na Lowasa katika uchaguzi wa mwaka 1995?
  6. Mkurugenzi wa wilaya ya Mufindi na mkuu wa wilaya umewateua wafanye kazi au wasimamie maslahi yako ya biashara za mbao?
  7. Ni wapi wewe na Lowasa mmekutana?
  8. Nini maana ya Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya?
  9. Wapi ulitoa kaulimbiu ya Ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi?
  10. Hivi huwa unasoma vitabu kweli?, unakifahamu kitabu cha Uongozi wetu na hatma ya Tanzania kilichoandiwa na Mwalimu Nyerere?
  11. Kodi ya mmachinga na Geita Gold Mining ipi ina umuhimu kwa ustawi wa taifa letu?
  12. Majaribio ya uchimabaji wa mafuta Mtwara yanaendeleaje?. Nasikia wanatoa pipa 300 kwa siku.
  13. TPDC wameanza kazi?..vp wameingia kwenye ushindani wa soko huria?
  14. Nazikumbuka ajira 1,000,000 ulizoahidi 2005,wewe bado unazikumbuka?
  15. KAGODA, TANGOLD, MEREMETA, tumeshaanza kunufaika nao?
  16. Maisha bora kwa kila mtanzania ulishayakamilisha? Maana kauli mbiu hii sikuisikia 2010
  17. Hivi kiwanda cha mgololo hakikuumi kumilikiwa na wageni?. Mimi nimefika pale na nilitoa machozi kukililia kama kristo alivyoililia Yerusalem.
  18. Umewahi kusikia kuwa kuna utata kuhusu minara pacha ya Benki Kuu?
  19. Nimekumbuka wezi wetu wa EPA, vipi walirudisha fedha zote?.nimesikia kule TIB zimechakachuliwa tena.
  20. Unamuenzi vipi baba wa taifa katika maisha yako?
  21. Wewe ni mmoja kati ya waumini wa sera na falsafa za TANU?
  22. Unamjua ASAS?
  23. Nani ni waziri mkuu wako, Lowasa, Sitta au Pinda?
  24. Anne Makinda ni spika wa kuteuliwa au wa kuchaguliwa?
  25. William Shelukindo Vs January Makamba, kunani?
  26. Unaamini kuwa ulishinda uchaguzi wa mwaka 2010?
  27. Antony Diallo, Deodorus Kamala, Batilda Buriani, Philp Marmo, Mwantum Mahiza, Joel Bendera, Mulongo Magesa, wanastahili kuwepo ulipowaweka?
  28. Lake Oil, unaijua?
  29. Amiri jeshi mkuu wa majeshi vipi ndege ya Qatar imebeba wanyama wetu na upo kimya?
  30. DOWANS na Rostam Aziz na wewe mna uhusiano gain?
  31. Unajua maana ya kustaafu?
  32. Unajua maana ya mafao?
  33. Unaiona Tanzania gani miaka 50 ijayo?
  34. Nini ni hatma ya kigamboni?
  35. Ziara na misaada ya George Bush inawanufaisha vipi watanzania?
  36. Elimu ya juu kwako ina umuhimu wowote, na ni nini sera yako juu ya elimu hii?
  37. Ulizomewa UDSM wakati wa maadhiisho ya miaka 50 ya chuo, unakumbuka?
  38. Ziara yako moja nje ya nchi inaigharimu nchi kiasi gain cha fedha?
  39. KIBUBU unachotembeza kuomba huko USA hakijajaa mpaka leo?
  40. Profesa Maji marefu anasafiri na wewe kama nani na ni nini umuhimu wake katika safari zako?
  41. Walimu, walimu unawadharau, unawajali, unawasikiliza au huwasikilizi?
  42. Uwekezaji bila unyonyaji inawezekana?
  43. Tanzania bila uwekezaji inawezekana?
  44. Tanzania bila ukimwi inawezekana?
  45. Tanzania bila malaria inawezekana?
  46. Tnzania bila misaada inawezekana?
  47. Tanzania bila ufisadi inawezkana?
  48. Tanzania bila CCM inawezekana?
  49. Uchaguzi bila kuiba kura inawezekana?
  50. Haki bila maandamano inawezekana?
  51. Elimu ya juu bure bila mikopo inawezekana?
  52. Mawaziri bila mashangingi inawezekana?
  53. Hospitali bila vifaa na dawa inawezekana?
  54. Shule bila vitabu na walimu inawezekana?
  55. Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana?
  56. Ajira bila rushwa inawezekana?
  57. Ubalozi bila watoto wa vigogo inawezekana?
  58. Maendeleo bila uhuru wa habari na kujieleza inawezekana?
  59. UDOM bila Mlacha inawezekana?
  60. Katiba mpya yenye kujali haki na usawa kwa watu wote bila maandamano je?
  61. Elimu ya juu bila migomo na maandamano inawezekana?
  62. Uongozi bila hekima na busara inawezekana?
  63. Tanzania bila TAKUKURU inawezekana?
  64. Baraza la maadili la viongozi wa umma unazijua kazi zao?
  65. Unayajua maradhi halisi yaliyomuondoa AMINA CHIFUPA?
  66. Daudi Balali alizikwa USA, Trindad na Tobaggo au New Jersey?
  67. Vipi uliletewa picha za mazishi ya Balali?
  68. Utata ajali ya Chacha Wangwe umepata majibu yake?
  69. Profesa Juan Mwaikusa wauaji wake vipi?
  70. Regia Mtema na wewe umeambiwa ndiye aliyekuwa anaendesha gari wakati anapata ajali?
  71. Vipi ya Nungwi yameishia wapi?
  72. Ripoti ya Mv Bukoba vipi?
  73. Ajali ya treni Dodoma vipi umejipanga isijirudie au unaamini mwendokasi?
  74. Wa mbagala na gongo la mboto vipi wamerudia maisha yao ya zamani?
  75. Ajali za barabarani vipi madereva tuwachukulie hatua gani?
  76. Maadhimio ya Bunge kuhusu ripoti ya RICHMOND vipi?
  77. Maadhimio ya Bunge kuhusu Luhanjo, Jairo, Ngeleja n Malima vipi?
  78. kutawala bila kuhofia Mwanahalisi, Tanzania Daima, Raia Mwena na Jamii Forums unaweza?
  79. Kutoa hotuba bila vijembe, kejeli na vitisho unaweza?
  80. Kuomba omba ndio sera na falsafa ya serikali unayoiongoza? Mbona kwenye ilani yenu haikuwemo?
  81. Unaweza kutuandikia vitabu kuhusu misingi, tabia, manufaa na matokeo ya sera ya kuomba omba?
  82. Ulipigwa mawe Mbeya vijijini unakumbuka?. Ulijiuliza ni kwanini?
  83. Umeme ulikatika mwezi mzima Mbeya baada ya kupigwa mawe unakumbuka?
  84. Umeshaanza kujenga Machinga complex zingine ngapi DSM?
  85. Vipi machinga complex mikoani tukungoje mpaka lini?
  86. Manyoni Tabora kupitia Itigi au Manyoni Tabora kupitia Singida Mjini, njia ipi unaipenda?
  87. Kijijini kwetu hawajui maana ya REA, vipi kwenu umewaelimisha wameshaijua?
  88. Pius Msekwa, Anne Makinda, Kingunge Ngombalemwiru, vipi kasi zao, ari zao na nguvu zao bado mpya au ni zaidi?
  89. Katika noti hizi mbili ipi wewe inakuvutia kuitumia?. Mimi naipenda sana unayotaka kuifuta.
  90. Huwa nasikia umesoma uchumi, vipi mabilioni yako yameleta tija kwenye uchumi wetu?
  91. Raisi wa awamu ya tatu na wa awamu ya tano wanatoka jimbo hilo hilo?
  92. Mahakama ya Kadhi unaijua wewe? Kuwa makini inaweza kukuhukumu.
  93. Unazikumbuka zile enzi ulipokuwa waziri wa fedha, vipi uchumi ulikuwaje?
  94. Natamani nijue ni lini mtera ikijaa maji mashine zake hazitaelemewa, vipi unajua?
  95. Hivi KIWILA kunachimbwa madini gani na yana tija gani kwa taifa?
  96. Kale ka utaratibu ka kuulizwa maswali TBC1 vipi kanaendeleaje?, sijaangalia muda mrefu kidogo.
  97. Dhahabu ikiisha, migodi ikifungwa yale mashimo yakijaa maji utaanzisha kilimo cha umwagiliaji au tutafua umeme kupunguza huu mgao?
  98. Vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua vipi?
  99. LOLIONDO ulienda?
  100.KWANINI USIJIUZULU?
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa si ungeituma kwenye email ya Ikulu kabisa, humu kwani kuna washauri wa jk?
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ndo ukamwambie akawadanganye wale wa Diamond Jubilee lakini sio kizazi cha mabadiliko
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  duh . . . .
   
 5. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mh...network problem.
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Tusaidie kucopy afu uifoward huko ikulu.
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Maswali na hoja za kimajungu!
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwani wewe ndie JK?
   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  mhuuu! Kujiulu...
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  ndo maana huku napigwaga sana bun, heading inasemaje? Yeye amesema kwa washauri wa jk tu, mimi nikamwambia si awatume kwenye email ya ikulu? Wewe ni mshauri wa jk?
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jf ni kubwa sana na ina watu mchanganyiko , tunaingia na majina feki je una hakika gani hawapo huku?
   
 12. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  low battery....
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  101. Je anajua kuwa mwanae ndio kinara wa kuingiza madawa ya kulevya, kupitia importation of sugar?
   
 14. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hii kali,....haya nani ajibu hapo magogoni, nyosheni vidole basi... na ukianza kujibu moja ujue yote utajibu, kudadadeki
   
 15. c

  collezione JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mhh... Bravo kaka. Haya maneno mazito. Ila sijui kama mwenyewe nayasikia
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Anajua ndio mana ile list alosema anayo kaichunia mpaka wa leo.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  One of the nonsense thread; useless information; majungu ukichanganya na ujinga

  Mkuu hii inafaa sana kuwa ajenda yenu kwenye kikao cha jumuiya kesho au siyo?
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ngumu kumeza. Jitahidi.
   
 19. c

  collezione JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ndugu umeongea vitu vinavyo_touch vibaya... Hii akiipata mkwe.re lazima atatafakari mwaka mzima. Ajui kuwa waTanzania tumeamka sasa"

  Na kiongozi makini lazima kichwa kitamuuma.
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Solution yake ni kuila sura ya JK kwani imenona sana.
   
Loading...