Kwa wapinga Nyerere tu

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Nimeona nianzishe thread hii kwa ajili ya wapinzani wa siasa za Nyerere hasa baada ya kuona wanajipenyeza kwenye threads zisizohusiana. kwa thread hii, mwageni lawama zote kwa hoja ila si kutukana.
 
Nimeona nianzishe thread hii kwa ajili ya wapinzani wa siasa za Nyerere hasa baada ya kuona wanajipenyeza kwenye threads zisizohusiana. kwa thread hii, mwageni lawama zote kwa hoja ila si kutukana.
Tueleze kwanza wewe upo upande gani?
 
Wengi wa wapinzani wake ni majeruhi kutokana na kukosa yale waliyoyategemea. Kwangu mimi mpinzani wa kweli wa Nyerere ni Marehemu Kambona maana baada ya kutokubaliana naye aliamua kukaa pembeni. Hawa wenzangu na mimi wameeenda naye weee halafu baada ya kuona ndoto zao hazitimii ndio wanakuja na story ambazo nyingi hazina hoja za kweli.

Leo hii watu tunasahau ili kwamba yule mzee alijenga nafasi yake kwa kutokubali kuwa opportunist na alikuwa very ethical. Uchumi hakuweza kuujenga na naamini kama angelifungua macho kidogo na kujifunza hii chinese model ambayo sasa hivi Ethiopia wanajaribu kwa nguvu zote ku implement, mambo yangekuwa tofauti sana.

Sasa ndugu zangu hawa ambao ili kugombea uraisi wanapelekewa hela zilizochangishwa jamatini kwenye makapu( Inaaminika hazikuweza kufikishwa Dodoma maana wajanja waliziwahi Morogoro) wangeliweza vipi kuongoza Taifa bila kupendelea?? Wakiwa JF wanasema hivi, wakiwa wanaomba kura wanasema vile,mmmmhhhh! Mi binafsi sioni kama wana hoja zaidi ya chuki binafsi kwa kukosa kitumbua ambacho wengine wanakifaidi kweli kweli.
 
The late Nyerere was a true statesman, he was a president who took time 2 read extensively, he was also a leader who can command authority, he never lived a lavish life, he also believed on homegrown solutions to our economic challenges rather than seeking foreign solutions. He was also a true disciple of corrupt free nation. AM YET TO SEE ANOTHER LEADER WITH THESE QUALITIES...
 
Mtafute W.J Malecela ndio kaanza kuonyesha upinzani na nyerere baada ya baba yake kubaniwa kugombea Urais kupitia CCM Tokea juzi anakuja na vithread vyake venye tittle za ajabu ili asionyeshe ana chuki anamuonea wivu Ridhwani kwasababu ungekuta ni yeye ana hela za ufisadi kama Ridhwani kwi! kwi! kwi! kwi!
 
Nyerere alikuwa ni kiongozi bora sana japokuwa kutakuwa na mapungufu aliyokuwanayo lakini nayo hayaondoi U-good boy wa Nyerere kwani Nyerere ni public figure wa dunia kwani alikuwa ni mtu wa haki na usawa may be kwa leo hii JK nyerere naweza kumfanisha kwa kiasi fulani na GODBLESS LEMA kwa kuwa na kiu ya haki paisipo uoga..
 
Nimeona nianzishe thread hii kwa ajili ya wapinzani wa siasa za Nyerere hasa baada ya kuona wanajipenyeza kwenye threads zisizohusiana. kwa thread hii, mwageni lawama zote kwa hoja ila si kutukana.

"...pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, na sio wao wenyewe" (TUJISAHIHISHE-Mwl JK Nyerere, Dar-es-salaam, Mei, 1992)

"Hakuna jibu moja ambalo linaweza kutumika nyakati zote na mahali pote" (JK Nyerere tarehe 4.5.1965)

Ni ukweli kabisa hoja na mitazamo ya Mwalimu ilikuwa imejaa utajiri wa fikra, busara na mitazamo pevu katika kukabili matatizo ya Watanzania, lakini ni ukweli usiopingika (undeniable truth) kwamba baadhi ya mitazamo yake ilikuwa too ideological. Mwalimu alifaulu kwa kiwango kikubwa katika kujenga umoja na mshikamano katika taifa letu lakini kwa kutazama sera za kiuchumi bado zipo hoja zinazohitaji mjadala mpana.

Binafsi napingana na baadhi ya Mitazamo ya Nyerere na wala sipingani na Nyerere, ieleweke kwamba tunapaswa kutumikia fikra zetu za akili kufuatana na ujuzi halisi wa mambo na hali ya mazingira yetu ya sasa.

Jambo la muhimu tunalopaswa kutambua ni kwamba, kila binadamu anafanya makosa lakini hatupaswi kujiridhisha na makosa yetu bila kutumia fikra zetu kutafuta ufumbuzi mkubwa kusahihisha makosa yetu.


Be wise, Act Wise!
 
Back
Top Bottom