Wapinga maendeleo waliojificha kwenye demokrasia ya vyama vingi

Nov 6, 2016
52
141
JAMBO AMBALO NAWASHANGAA SANA WAPINZANI, WAPINGA WATU, WAPINGA MAENDELEO NI KUTOJUA KANUNI YA DUNIA (360")

Na Comrade Ally Maftah

Leo nainua juu kalamu yangu na kuishusha kwenye mitandao ya kijamii, kuwakanda wapinga maendeleo wanaojivika kilemba cha wapinzani yaani vyama vya siasa mbadala.

Wanawatukana wana CCM ambao wamejikita katika eneo la kuinua hali ya kimaendeleo na kulitia moyo Taifa na viongozi wetu wanawaita MACHAWA. kumbukeni kwenye bendi kila mtu ana kipaji chake na sauti yake katika tunzi za beti na muundo wa ALA za muziki, kuna wanaokosoa ( kistaarabu ) wapo ndani ya CCM, kuna wanaoshauri, kuna wanaosherehesha,

Dunia inatupa nafasi ya kushughulikia mambo katika nyanja mbalimbali, hatuwezi kujikita kwenye masikitiko, malalamiko, kukebehi, kuudhi wengine.

Comrade Ally Maftah amejikita kwenye kuelimisha jamii na kuipa hali ya ujasiliamali hasa kwa watu wenye vipato vya chini na vijana wanaotoka mashuleni na vyuoni, huwa sijaielekeza akili yangu kwenye kuona upungufu au madhaifu ya mtu, watu, Viongozi, mimi nimejikita kwenye kuona fursa.

RIP OLE MUSHI, UMEUPIGA MWINGI SANA PUMZIKA KWA AMANI, ULIFANYA ULICHOKUWA UNAKIWEZA 100% UKAKIFANYA 100% WEWE NI SHUJAA

Ndimi Comrade Ally Maftah
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es salaam
IMG-20240206-WA0001.jpg
IMG-20240203-WA0019.jpg
 
Ni akili finyu ndiyo ambayo inafikiri CCM hakipaswi kukosolewa ama kupata upinzani kutoka kwa vyama vingine makini vya ushindani. CCM haina hati miliki ya utawala wa nchi hii. Ndiyo maana ilani yake hunadiwa na kushindanishwa na za vyama vingine kila baada ya miaka mitano kwa njia uchaguzi.

Ushindani huu ni sehemu muhimu sana ya mchakato wa kidemokrasia, na pia kupitia matakwa ya kikatiba na kisheria. Sasa mtu anawezaje kutothamini mchango mkubwa wa vyama makini pale vinapoibua na kuhoji madudu yanayofanywa na chama tawala!?

Wananchi wa nchi zilizoendelea huviona vyama vyote ni sawa katika mizani ya ushindani, na huvichukulia kama tu vazi linalotakiwa kubadirishwa mara kwa mara. Wana uzoefu wa kutosha kuhusu uzuri wa kubadilisha utawala chama kimoja kwenda kingine katika vipindi tofauti. Hali ni tofauti sana hapa nchini, watu wengi bado mawazo yao yapo ndani ya kasha la fikra, na wala hawana uwezo ama ujasiri wa kufikiri nje ya kasha, wao huishi tu kwa mazoea ili tu siku zizidi kusonga mbele.

Nchi nyingi zinazokumbatia mfumo wa ujamaa na kujitegemea ndiyo wahanga wakubwa wa utawala wa kidola chini ya mfumo uliopitwa na wakati wa utawala wa chama kikongwe kimoja. Ndiyo! It is a socialism hangover! Kiasi kwamba si ajabu kumkuta mtu mzima amekaririshwa tu mazuri tu ya chama tawala, na kuvichukulia vyama vingine makini vya ushindani kama havina maono wala mchango wowote ule katika maendeleo ya nchi yetu.
 
Kutoa onyo serikali isijenge mradi wa mabilioni pale jangwani ndio kupinga maendeleo.
 
JAMBO AMBALO NAWASHANGAA SANA WAPINZANI, WAPINGA WATU, WAPINGA MAENDELEO NI KUTOJUA KANUNI YA DUNIA (360")

Na Comrade Ally Maftah

Leo nainua juu kalamu yangu na kuishusha kwenye mitandao ya kijamii, kuwakanda wapinga maendeleo wanaojivika kilemba cha wapinzani yaani vyama vya siasa mbadala.

Wanawatukana wana CCM ambao wamejikita katika eneo la kuinua hali ya kimaendeleo na kulitia moyo Taifa na viongozi wetu wanawaita MACHAWA. kumbukeni kwenye bendi kila mtu ana kipaji chake na sauti yake katika tunzi za beti na muundo wa ALA za muziki, kuna wanaokosoa ( kistaarabu ) wapo ndani ya CCM, kuna wanaoshauri, kuna wanaosherehesha,

Dunia inatupa nafasi ya kushughulikia mambo katika nyanja mbalimbali, hatuwezi kujikita kwenye masikitiko, malalamiko, kukebehi, kuudhi wengine.

Comrade Ally Maftah amejikita kwenye kuelimisha jamii na kuipa hali ya ujasiliamali hasa kwa watu wenye vipato vya chini na vijana wanaotoka mashuleni na vyuoni, huwa sijaielekeza akili yangu kwenye kuona upungufu au madhaifu ya mtu, watu, Viongozi, mimi nimejikita kwenye kuona fursa.

RIP OLE MUSHI, UMEUPIGA MWINGI SANA PUMZIKA KWA AMANI, ULIFANYA ULICHOKUWA UNAKIWEZA 100% UKAKIFANYA 100% WEWE NI SHUJAA

Ndimi Comrade Ally Maftah
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es salaam
View attachment 2895703View attachment 2895704View attachment 2895705
Kalamu ya Baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
____________
Nimeumizwa sana na kifo cha ndugu Thadei Ole Mushi. Aliwahi kutetea hadharani haki yangu ya kuishi ilipotaka kudhulumiwa. Sikuwa nakubaliana na hoja zake nyingi isipokuwa moja ambayo ni: haki yake ya kusema na kutoa maoni yake kwa uhuru.

Alikitetea sana chama chake na alikipinga pia kwa hoja. Niliumia mno alipojitokeza hadharani kukanusha tuhuma za mchezo mchafu (kuwekewa sumu) juu ya kuugua kwake. Kama tuhuma hizo zilikua na ukweli hata robo, basi watesi wake walimtumia kujisafisha. Hakuna wa kuwachafua tena kwa sasa.

Kwa msimamo wake wa kutetea uhuru wa maoni, alitengeneza maadui ndani ya chama alichokuwa anakitetea. Chama chake kinawaheshimu na kuwavumilia wanaokikosoa wakiwa nje lakini hakina ubavu wa kuwavumilia wanaokikosoa wakiwa ndani.

Katika ombwe la fikra pevu kwa vijana wanaojihusisha na masuala ya siasa, alikuwa miongoni mwa wachache wenye kuandika na kujadili bila kutukana. Hatunao wengi.

Familia imempoteza mtu muhimu mapema. Chama chake kimempoteza Mwenezi mwenye akili na uwezo wa kujenga hoja kuliko mwenye cheo cha Mwenezi. Wizara ya elimu imempoteza mwalimu hodari aliyeipenda na kuitetea kazi yake.

Kwa heri Ole Mushi. Umeacha nchi gizani, unaenda kaburini penye giza. Yawezekana hakuna ulichopoteza, japo sisi tumepoteza. R.I.P Ole Mushi.!
FB_IMG_1707444191154.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom