Hahahahahahaaaaaa! Mkuu umenikumbusha mbali sana
Hivi hivi vikao vya usuluhishi!
Familia moja tukawasuluhisha sanaaaaa lakni mwanaume kakazana na wazazi wawepo kwenye usuluhishi!
Mwanamke akamsihi sana kwa kupiga na magoti, mwanaume akasema nitakusamehe endapo utaomba msamaha mbele ya wazazi tena wapande zote mbili, basi binti akasema hamna shida waite.
Wazazi wakaitwa, washenga, akaenda mbali zaid kawaita hadi wachungaji (utadhani kamfuma mkewe na mwanaume kitandan)
Mwanaume akajieleza weeeeeeeee! Na mambo ambayo ni ya kawaida tu sio ya vikao akayaweka hapo (ki ukweli kama mzazi hasa mama aliona ni kama yeye ndo anavuliwa nguo, alilia sana yule mama wa binti)
Basi mpira ukarudi kwa binti, (naona ndani ya akili yake alisema liwalo na liwe ) binti wa watu akaanza kwa busara kabisa, akamwomba msamaha mmewe, kwa magoti akamfuata mchungaji kampigia magoti,
Vivo hivo kwa wazazi wote, tena huku analia sana hasa alimpomfika mamake ( ilikuwa kama msiba)
Akasema kabla hamjaondoka naombamtusaidie mambo kadhaa,
Binti alitiririka,
Kuanzia mambo ya jikoni, sebleni hadi chumbani!
Akasema hapa mnapo niona mme wangu ili anitimizie haja zangu chumbani natakiwa nimuingizie kidole mku****i ndo mzee anastuka na akinipanda hata jogoo anatumia mda mwingi kwa tetea wake hata sielewegi hizi mimba sijui ni mtakatifu kama bikira maria, maana sijawahi kuusikia uanaume wake! Ila nipo hapa maana najua nilifanyika mwanamke kwaajili yake ili nichukuliane naye!
Na mengine lundooooo! kiufupi binti alivoona mwanaume kamwaga mboga, yeye aliamua kumwaga ugali, mahindi yaliyokuwepo ndani akayatia sumu msisage, ya shambani kaenda kuyafyeka na shamba kauza! Hahahahahahaaaaaa
Kibao kikamgeukia mwanaume, wazazi wa binti maskin hawakuongea chochote mtoto wao alivyomaliza kuongea wakaomba kuaga, wakambelelezwa lakin wakaondoka! Ngoma ilibaki uku nyuma,
Lakn tunamshukuru Mungu wanaishi ila mwanaume hana raha kabisaaaa hasa wanapokuwepo ndugu wa mwanamke!
Jaman kunapokuwa na misunderstanding hebu kaeni malizeni wenyewe achaneni na vikao vikao!
Ukiuliza kosa!
MWANAUME ALIKUTA SMS ZA STAFF MWENZIE NA BI DADA ZA MITONGOZO, (hapo ni mtongozo sio wamekubaliana) MWANAMKE AKASEMA NI KWELI HUYO STAFF ANAFANYA HIVO LAKIN YEYE ALISHAMKATALIA,
SASA MUME KAKOMAA KAMA NDO IVO ACHA KAZI, BINTI AKASEMA NAACHAJE KAZI KWAAJILI YA MPUUZI AMBAYE MIMI SIKO INTERESTED NAYE, KIKUBWA NI MSIMAMO WANGU KWANI HUKO NYUMBANI AU KWENYE BIASHARA NDO SITATONGOZWAA (mume kakomaa vikao) hayaaaa shauri yenu
(Mnisamehe nimewachosha) mweeeee