bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,360
Jamani mimi sijui kama ni ushamba wangu ama ni ugeni wa mambo lakini kwa vyovyote vile naomba nitakapokosea nikosolewe na nitakapoteleza nisahihishwe bila jaziba na matusi. Leo naongelea wanawake na wanaume waliopo makazini kwenye ofisi mbalimbali za serikali na za private. Mimi kwanza nitoe angalizo nimekuwa nikifanya kazi sehemu ambazo wanawake ni wa kuhesabiwa sana kutokana na kada yangu.Kwa hiyo wanawake kwa kuwa ni wachache na pia sehemu yenyewe ipo busy ni salamu tu basi na jioni ni kwaheri tutaonana kesho.
Sasa kuna sehemu mpya nimeajiriwa nina miezi mitatu kamili, lakini yanayotendeka kwenye ofisi hii yananitia kinyaa ile mbaya. Yaani utakuta mtu ni mume wa mtu kabisa mnapanda gari amempakata mke wa mtu na huyo mke wa mtu ametulia kimya kwenye mapaja ya bwana huyo na sio kusema eti siti zimeisha wapi siti kwenye gari la staff ni za kutosha. Sasa yanayofanyika kwenye maofisi ndo utachoka kabisa utakutana na mama tena mwenye heshima zake anapapaswa na kushikwa ma--ko na baba mwenye tena pete ya ndoa eti wanakoroga chai kwenye chumba cha tea room yaani nashangaa sana. Wengine hata wanadiriki kuitana sweetie wakati hawawezi kuwaita wake zao wala waume zao sweetie.
Halafu na wasichana ambao hawajaolewa mtulie kwenye maofisi sio kujirahisisha tu, hivi unajua kuwa muoaji serious atataka kupata feedback kutoka kwenye ofisi yenu how you behave sasa kama ni wa kushikwashikwa kila mara na kujichekesha chekesha labda akutane na mwingine ndo ataremba akikutana na mimi namwambia ukweli kuwa hapa hakuna kitu ni jamvi la wageni. Maana wewe ushaona mtu ana pete ya ndoa umo tu unategemea nini kama si kuliwa na kuachwa hapo. Na nyie wavulana acheni kuharibu ndoa za watu eti kwa kujifanya damu inachemka
Hata kama ni kuzoeana lakini sio hivyo nduguzanguni lazima tuheshimu ndoa zetu na tuwe na mipaka maana socialization nayo ikizidi itakuwa shida sasa. Mi nawaza na kuwazua hivi hawa wanaoshikanashikana na wengine kukaliana kwenye magari siku wakiambiwa kuwa waende semina nje ya Dar si watafanya kweli. Tuheshimu ndoa zetu na tuwe na mipaka kwa kila jambo maana ibilisi yupo kazini