Kwa wanaume wanaotarajia kupata watoto

Wanaume wenzangu naomba mtambue kwamba kama kuna kipindi ambacho unatakiwa kuonyesha mapenzi ya kiwango cha SGR / mapenzi ya hali ya juu ya kujali sana ni pale mkeo anapokuwa mjamzito.

Kipindi hiki mke huwa na mambo mengi sana na mpaka mengine unajiuliza hivi hii mimba inavyompelekesha ni yeye tu au wanawake wote wanakuwa hivi pia?

Kuambiwa umletee chakula fulani hlf baada ya kukileta akakitaa ni kawaida tu, kuambiwa usiku wa manane anahitaji soda ya baridi ni kawaida tu na viusumbufu vingi ambavyo havina kichwa wala miguu.

Huu ni wakati ambao mwanamke anapitia changamoto nyingi sana kihisia na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini mwake,kwahiyo anakuwa katika hali ambayo sio ya kawaida, wengine wanakuwa hawana mambo mengi nawengine wanakuwa na mambo mengi.

Huu si wakati wa kushinda bar na kurudi nyumbani late bali ni wakati ambao uwepo wako ni muhimu sana kwa mwenza wako ili apate kufarijika

Si wakati wa kumpa stress na michepuko yako, ni wakati ambao anahitaji amani ya moyo wake sana,,ni wakati wa kujitoa mazima kwake na kumfanya awe malkia wako.

Kwasisi ambao kwa namna moja au nyingine kwa kipindi fulani tulizua taharuki katika kipindi hiki tuliona pale baby mama anapokuwa na stress mpaka kiumbe tumboni unakisikia kinavyo hangaika kana kwamba kinataka kitoke kimsaidie mama yake ,hii sio nzuri hata kidogo huwa sometime natamani ningerudisha siku nyuma na kuondoa makosa niliyofanya wakati baby mama alipokuwa mjamzito,,sitaki nawe ufanye makosa hayo.

Huu ni wakati wa kuwa mpole na laini sana kwa mkeo,,kwa kifupi jifanye fala sana kwa lengo la kufanya mkeo awe na wakati mzuri katika kipindi hiki,,hapa jishushe sana na uwe mwema sana kwake na uvumilie usumbufu wowote ambao utaupata kutoka kwake,,tambua sio yeye huyo bali ni ujauzito ambao anao ndio umebadilisha kila kitu katika maisha yake.

Onyesha upendo mkubwa sana kwa mkeo na hakikisha hatoi chozi katika kipindi hiki kigumu sana

Kuwa mwanaume na mume bora kabisa kupata kutokea hapa duniani.

Ni hayo tu!
Mnafanyiwa na kuletewa drama tu. Mbona waliotelekekezwa na kubeba mimba huwa hawafanyi hivyo? Mbona wanafunzi na madhouse girl waliobebeshwa mimba haziwapelekeshi hivyo?

Mimi ni Mme na Baba wa watoto 4, katika mimba zote mke wangu hajawahi kuwa na hizo drama. Mkubwa yupo form 5 anaingia Six na binti yetu wa mwisho yupo Class Six ila sijawahi experience hayo mambo. Poleni kwa kupelekeshwa vijana wa leo.
 
Wanaume wenzangu naomba mtambue kwamba kama kuna kipindi ambacho unatakiwa kuonyesha mapenzi ya kiwango cha SGR / mapenzi ya hali ya juu ya kujali sana ni pale mkeo anapokuwa mjamzito.

Kipindi hiki mke huwa na mambo mengi sana na mpaka mengine unajiuliza hivi hii mimba inavyompelekesha ni yeye tu au wanawake wote wanakuwa hivi pia?

Kuambiwa umletee chakula fulani hlf baada ya kukileta akakitaa ni kawaida tu, kuambiwa usiku wa manane anahitaji soda ya baridi ni kawaida tu na viusumbufu vingi ambavyo havina kichwa wala miguu.

Huu ni wakati ambao mwanamke anapitia changamoto nyingi sana kihisia na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini mwake,kwahiyo anakuwa katika hali ambayo sio ya kawaida, wengine wanakuwa hawana mambo mengi nawengine wanakuwa na mambo mengi.

Huu si wakati wa kushinda bar na kurudi nyumbani late bali ni wakati ambao uwepo wako ni muhimu sana kwa mwenza wako ili apate kufarijika

Si wakati wa kumpa stress na michepuko yako, ni wakati ambao anahitaji amani ya moyo wake sana,,ni wakati wa kujitoa mazima kwake na kumfanya awe malkia wako.

Kwasisi ambao kwa namna moja au nyingine kwa kipindi fulani tulizua taharuki katika kipindi hiki tuliona pale baby mama anapokuwa na stress mpaka kiumbe tumboni unakisikia kinavyo hangaika kana kwamba kinataka kitoke kimsaidie mama yake ,hii sio nzuri hata kidogo huwa sometime natamani ningerudisha siku nyuma na kuondoa makosa niliyofanya wakati baby mama alipokuwa mjamzito,,sitaki nawe ufanye makosa hayo.

Huu ni wakati wa kuwa mpole na laini sana kwa mkeo,,kwa kifupi jifanye fala sana kwa lengo la kufanya mkeo awe na wakati mzuri katika kipindi hiki,,hapa jishushe sana na uwe mwema sana kwake na uvumilie usumbufu wowote ambao utaupata kutoka kwake,,tambua sio yeye huyo bali ni ujauzito ambao anao ndio umebadilisha kila kitu katika maisha yake.

Onyesha upendo mkubwa sana kwa mkeo na hakikisha hatoi chozi katika kipindi hiki kigumu sana

Kuwa mwanaume na mume bora kabisa kupata kutokea hapa duniani.

Ni hayo tu!
Kipindi hiki mamam anakuwa na matumizi mengi mengine useless yanahitaji pesa...sasa ukiwa laini na fala utatafutaje hela?
 
Back
Top Bottom