Kwa wanaume tu njoo tutete

Kwa wanaume tu njoo tutete

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
14,563
Reaction score
22,839
Habari wanajamvi letu pendwa natumaini muwazima wa afya njema kwa ambaye mambo hayako poa pole sana,turudi kwenye maada
-----------
Jamani wanaume wenzangu tuongee kiume,humu ndani kumetokea wimbi la wanaume kutafuta mchumba au mke..huwa najiuliza inakuaje hii inamaana mtaka kusema kutongoza linataka kuwa janga la kitaifa? wanawake hawa wa humu ndani ndo hao tunaopishana nao huko nje sasa unashindwa kumtongoza akiwa huko unategemea akukubalie humu ndani kweli?

Binafsi ninaamini unaweza kupata mke kupitia mtandao maana ndo hawa hawa tunaishi nao nachukulia mtandao kama sehemu ya mawasiliano sasa inakuaje mtu anaacha namba ya simu mwanaume mzima ukitegemea mwanamke atakupigia sijui aanze vipi kujieleza eti "samahani nimeikuta namba yako kwenye mtandao ukihitaji mke mimi niko tayari" mmh jamani hata changudoa hawezi kukupigia atajua huna hela maana ungekuwa na hela ungeenda kwenye ofisi zao upate huduma..

Jamani humu kuna ladies wengi status zao wako single kama umezimika na mmoja wapo kuna PM nenda kule kajieleze,mwanzoni nilijua ni namna ya kulitendea haki jukwaa lakini nikagundua wengine wanakuwa serious maana mtu anaweka bandiko hata mara tatu akihitaj mke,Najiuliza tu ukishindwa kumtongoza mwanamke hivi kweli utaweza kuomba papuchi kwa wale wenye misimamo na ukapewa kweli? Hata mwanamke anajisika raha anapotongozwa na anajiamini zaidi kwamba katika 100 umemfuata yeye anajiona anathamani,kwa mtazamo wangu tunajiabisha wenyewe..
Naomba tubadilike basi,ukienda love connect mwanamke akitangaza kuhitaji mchumba hata wakumpa moyo na kumfariji wanakuwa wengi kuliko kwa mwanaume jiulize ni kwa nini mpaka kuna memba mmoja akalalamika eti Wanawake mtufanyie fair,fair gani wakati mnaacha namba tu ambazo hata wanawke hawaweki hizo namba

Samahani nimeongea kwa kirefu mniwie radhi tu,Baba paroko Eiyer,Babu Asprin,njooni mje mtoe msaada huku
 
Suala la kutafuta mke lina mambo mengi kidogo

Inawezekana kabisa ikawa sahihi kutafuta mke mtandaoni na ukapata anaefaa
Lakini uangalifu ni wa muhimu sana

Kutongoza ni sanaa lakini unaposema unahitaji mke na ukapigiwa simu wewe utakuwa wa kwanza kupeleka ombi kwa mhusika na utakuwa wewe umemuanza

Binafsi sioni kama kuna tatizo hapa ila nasisitiza tena umakini unahitajika sana
Hata hao wa mitaani nako umakini unahitajika pia!
 
waendelee tu kutafuta mtandaoni kuna matapeli kuna aina ya kila majitu wawe makini sanakuna mengine kama haya image.jpg images.jpg
 
Suala la kutafuta mke lina mambo mengi kidogo

Inawezekana kabisa ikawa sahihi kutafuta mke mtandaoni na ukapata anaefaa
Lakini uangalifu ni wa muhimu sana

Kutongoza ni sanaa lakini unaposema unahitaji mke na ukapigiwa simu wewe utakuwa wa kwanza kupeleka ombi kwa mhusika na utakuwa wewe umemuanza

Binafsi sioni kama kuna tatizo hapa ila nasisitiza tena umakini unahitajika sana
Hata hao wa mitaani nako umakini unahitajika pia!
Vipi hili suala la kuweka namba ya simu ili huo mchumba akutafute? mwingine kaweka namba halafu anatoa maelezo kwamba unapotuma msg anza na neno mchumba na hilo likoje Baba paroko
 
Hilo nalo neno!!! Kuna jamaa alikuwa anatafuta mupenzi mda mrefu kweli hadi juzi kaanzisha siredi nyingine!
Mwingine ametoa namba eti unapotuma msg Anza na neno mchumba kwanini asiende PM kwa dada anyemvutia ajieleze kuwa anahitaji mke nadhani atapata kirahisi kuliko kusubiri wampigie simu
 
Binafsi naona mwanaume ukishindwa kujiamini kwa kumface mwanamke na kumueleza haja ya moyo wako na kuishia kulalamika, nina mashaka hata ukipata mke bado utakuwa mtu wa kulaumu na kumtegemea mke kwa kila kitu. Mwisho wa siku kuna hatari ya kuwa na mume asiyejua majukumu yake wala uwezo wa kutunza na kuilinda hiyo familia. Ni vyema kujiamini. Kuface mdada na kumshawishi kuwa mke kunamuongezea mkaka uwezo mkubwa wa kujiamini na kuwa na uwezo wa kulinda na kutunza familia.
 
Vipi hili suala la kuweka namba ya simu ili huo mchumba akutafute? mwingine kaweka namba halafu anatoa maelezo kwamba unapotuma msg anza na neno mchumba na hilo likoje Baba paroko

Mkuu haya mambo mengine naona kama ni binafsi zaidi

Kuna watu wana namba kwaajili ya hii kitu na sio zile wanazotumia kikazi au kuzoeleka zaidi

Akipata na kuridhika nae anaitupa namba

Naona mambo ya utandawazi haya ..!!!!
 
Binafsi naona mwanaume ukishindwa kujiamini kwa kumface mwanamke na kumueleza haja ya moyo wako na kuishia kulalamika, nina mashaka hata ukipata mke bado utakuwa mtu wa kulaumu na kumtegemea mke kwa kila kitu. Mwisho wa siku kuna hatari ya kuwa na mume asiyejua majukumu yake wala uwezo wa kutunza na kuilinda hiyo familia. Ni vyema kujiamini. Kuface mdada na kumshawishi kuwa mke kunamuongezea mkaka uwezo mkubwa wa kujiamini na kuwa na uwezo wa kulinda na kutunza familia.
Exactly ndo maana nikauliza umeshindwa kumtongoza kuomba game utaweza au ndo hawa wanalalamika wanahudumia lakini game hajapewa kumbae hajaomba anategemea mwanamke amletee asime haya ingiza!
 
Kila Mtu Kaka Ana Utashi Wake,na Pia Mbona Kwasasa Hata Wanawake Wenyewe Wapo Wazi Kuelezea Hisia Zake.
 
utaalamu wa kutongoza haukupi mke bora
Hapa kinachoongelewa siyo utalaamu wa kutongoza maada imejikita kwenye kujiamini kwa mwanaume,ukiweka namba eti mwenye shida na ww akupigie maan yake hujiamini,kama unajiamini itafute namba ww ya huyo mwanamke umpigie na umueleze shida yako,sasa siku hizi hii inapungua wengi wanataka kuacha namba ili wapigiwe maana yake ni kutojiamini
 
Mkuu Daudi1 ahsante kwa mwaliko.

Wavulana wa siku hizi kuna tatizo sehemu. Wamerahisishiwa mambo na teknolojia lakini inashangaza wanashindwa kuitumia ipasavyo.

Najaribu kutafakari enzi zetu tukitongoza kwa kupitia SLP na kama vipi kukatana mitama vichochoroni, hawa vijana si wangeishia kupiga punyeto?

Vijana wanapaswa kutoa uso wa aibu kwa wadada. Mwanamke ukimtokea kijasiri yeye ndo anakuwa na aibu. Na unapoonyesha ujasiri ndo mwanamke anapokukubali zaidi.

Vinginevyo hivi vibinti virembo vitaendelea kuangukia kwenye mikono yetu wakongwe kwa kuwa wavulana wameshindwa kazi.

Acheni kulialia mitandaoni wavulana, mabinti wanawacheka.

Ngoja nikazimue kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Hili jambo naona Lina 2 sides, moja ni wanaume wasiojiamini au waliojikatia tamaa ktk swala la mahusiano aidha kutokana na kujeruhiwa kimapenzi au mfumo mbaya wa maisha walionao na kufikiri vibaya.

Pili kuna watu ambao mazingira yanayowazumguka au tuseme aina ya shughuli wanazozifanya vinasababisha washidwe kua katika nafasi nzuri ya kukutana na aina ya mwanamke wanayempenda hivyo wanajikuta wanajaribu kutumia mitandao kama nyenzo ya kuwasaidia.

Hayo ni mawazo yangu kuhusiana na mada husika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom