Kwa wanaotafuta wachumba wa kweli wa kuoana

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Siku ya Kwanza nitoke Vipi?

Fikiria wewe ni kijana wa kiume umepanga kukutana na binti ambaye unategemea awe mchumba wako, unawaza je, itakuwaje? Je, atanikubali kweli? Ataridhika jinsi nilivyo kweli? kiroho kinakudunda kweli maana hujazoea haya mambo!
Huhitaji kuwaza au kufanya mambo makubwa just relax fuata hizi tips bila shaka lazima utamvutia kiasi cha yeye kutaka kukutana na wewe tena na tena.

HAKIKISHA IDARA YA USAFI UMEKAMILIKA
Umeoga vizuri, umevaa nguo safi, unaweza kuvaa nguo za gharama na bado zikawa chafu so vaa nguo safi, piga mswaki na kuwa na meno safi.
Wapo akina dada akishajisikia unanuka basi bye bye, au akiona meno ni machafu na mboga za tangu juzi zimo kwenye meno anakata tamaa kabisa, au mdomo unaonuka.
Pia angalia kucha zako zipoje, kama ni chafu una balaa wewe!
JALI MUDA
Jitahidi kuwepo mahali mlikubaliana katika muda muafaka, kama ni mara ya kwanza na umemuweka dada wa watu akusubiri zaidi ya saa nzima huwa haipendezi pia ni dalili kwamba hupo makini. Hata kama umechelewa kuna dhalula karibu kumpigia simu na kumueleza sababu na utafika muda gani. Siyo kwenda kujieleza baada ya kufika huku umechelewa.

USIWE MTU WA KUJISIFIA NA KUONGEA TU
Usitumie muda wako wote kuongea habari zako mwenyewe na wewe kuongea tu bila yeye kumpa nafasi kuongea. Ni vizuri sana ukawa na hekima kuuliza maswali huku ukimpa nafasi kubwa yeye kuongea huku wewe unamsikiliza. Pia be fun, hakikisha anfurahi ila usizidishe maana inabidi usome saikolojia zake kujua ni dada wa aina gani.
Pia hata kama lugha yako ina maneno ya ajabu ajabu uwe makini kwani kuna akina dada wengi hujiuliza hivi kama anatukana, au analalamika, au analaani hivi leo siku ya kwanza je, tukioana?
Pia achana na habari za kuanza kuongelea mahusiano yako ya nyuma au habari za wanawake wengine unless either ni mama yako mzazi.
TABASAMU.
Kutabasamu ni ufunguo wa moyo wako ulivyo ndani, isijetokea dada aka smile na wewe ukawa umeweka tu ndita usoni na kuzima mdomo kama uso wa mtu anayekunywa gongo. Mwanamke anayehitaji mwanaume friendly, aliyetulia na uwe wewe kama ulivyo bila kujifanya ni mtu Fulani hivi.

TEMBEA NA PESA
Inatokana na sehemu ambayo umepanga kukutania na kama mwanaume ni vizuri kutembea na pesa ingawa kweli unaweza kuwa na dada ambaye ana pesa na anataka kulipa ni vizuri hiyo bill lipa wewe kwa mara ya kwanza kwani itaonesha huna uchungu na ngawira zako. Pia ukishapewa bill usiulize sana maswali yanayoonesha upo very concerned na hizo pesa just pay it tight away.
Siyo unaenda bila pesa na bill ikija unaanza kung’aa macho na kujihurumia.

ANGALIA TABIA ZAKO
Jitahidi kuwa gentle, fungua mlango kwa ajili yake, unapoongea mwangalie usoni siyo kifuani. Jiamini hata unapoongea ongea kama mwanaume ambaye ni source of woman’s happiness. Unaweza kumgusa wakati unaongea ila uwe makini kumsoma kama kweli anafurahia kwani this is your first time, kuna wanawake wanapenda kuwa touched.
Pia uwe makini usiwe mtu wa ku-force mambo kwa maana kwamba unataka kila kitu siku hiyo hiyo kieleweke.
Hapa unafungua mlango tu wa kukutania mara kwa mara na kufahamiana kwani akipendezwa na wewe leo basi kesho atataka mkutane tena na ndipo unaweza kuanza kuingiza topic zako maana sasa mmeanza kuzoeana.

AMEN...............!!!!
 
ANGALIA TABIA ZAKO
Jitahidi kuwa gentle, fungua mlango kwa ajili yake..........

AMEN...............!!!![/QUOTE]

tatizo langu mi ni hapa tu.dont play MR. nice guy kama siyo tabia yako and you cant keep doin baadae kama mambo yenu yatakaa vizuri!wacha maigizo,be yourself na mwache achague mwenyewe!mara nyingi tunajifanya kuwa kama watu wa kwenye hadithi za kufikirika na matokeo yake mabinti nao wanaingia kwenye mahusiano na sisi wakiwa hivyo hivyo kimtazamo halafu tunawalalamikia!
 
TEMBEA NA PESA
...Pia ukishapewa bill usiulize sana maswali yanayoonesha upo very concerned na hizo pesa just pay it tight away.Siyo unaenda bila pesa na bill ikija unaanza kung'aa macho na kujihurumia.

ANGALIA TABIA ZAKO
Jitahidi kuwa gentle, fungua mlango kwa ajili yake, unapoongea mwangalie usoni siyo kifuani.

Ndio maana nilikuwa nakosa sana wachumba enzi zangu..
Manake bill ije nisiulize maswali..lol
Halaf eti nikuangalie tu usoni bila kushuka chini kidogo..huh!
Otherwise zinasaidia sana hizi tips zako..welldone Kimbweka
 
Last edited by a moderator:
Hicho kipengele cha ' USIWE MTU WA KUJISIFIA'...ujue sometimes hayo mambo yanakuwa ya kurithi,utakuta mtu hata hajijui kama anajisifia kila dakika ila ndio hivyo..anajisifia..! Kuna makabila yana hiyo sifa.. Usipime,ukimkuta anatongoza lazima atoe advertise za furniture ghali aliyonunua week iliyopita au gharama ya gari alilonalo..nyumba anayoishi ama Masters yake alivyoisomea huko Stanford...yaan balaaa! Na ndo yuko hivyo,haibadiliki.. Tunamfanyaje huyu??
 
Kwa mambo kama haya ndio maana migogoro ndani ya ndoa haitaisha. Eti jitahidi kuwa msafi, kwa hiyo unamaanisha mtu awe msafi siku moja tu then wakioana je?
Kuongoka ni hiari ila kutubu ni lazima ili usamehewe dhambi zako.
 
Kimbweka, Kiss on the first date is it allowed....especially mmepoteza muda mrefu over the phone then you decide to have proper outing.
 
Last edited by a moderator:
Kimbweka, Kiss on the first date is it allowed....especially mmepoteza muda mrefu over the phone then you decide to have proper outing.

Hahahaha...naona unapenda hii kitu.....!!!
Unapiga la mbali mbali siyo la kung'ang'ania utafikiri umeshakubaliwa......!!!!
 
Mnakutana mara ya kwanza yaani mlikuwa hamfahamiani kabisa au kukutana mara ya kwanza kwa ajili ya kutongozana? Kama mlikuwa mnafahamiana tangu awali ukiwa tofauti na vile ulivyo hata huyo binti ataona unapretend tu.
 
Mnakutana mara ya kwanza yaani mlikuwa hamfahamiani kabisa au kukutana mara ya kwanza kwa ajili ya kutongozana? Kama mlikuwa mnafahamiana tangu awali ukiwa tofauti na vile ulivyo hata huyo binti ataona unapretend tu.

Umeonaaaaaaaaa,inatakiwa mtu uwe real(Comfortable) ya nini uende kutungua vinyago kwa date ya kwanza,je hizo nyingine si bankwa hela yote itakata?
 
Mnakutana mara ya kwanza yaani mlikuwa hamfahamiani kabisa au kukutana mara ya kwanza kwa ajili ya kutongozana? Kama mlikuwa mnafahamiana tangu awali ukiwa tofauti na vile ulivyo hata huyo binti ataona unapretend tu.

Siyo kukutana barabarani........!!
Kukutana kwa maongezi rasmi inaweza kuwa hotelini, sehemu yeyote ya starehe ili kumpa dukuduku lililopo moyoni....!!
 
Umeonaaaaaaaaa,inatakiwa mtu uwe real(Comfortable) ya nini uende kutungua vinyago kwa date ya kwanza,je hizo nyingine si bankwa hela yote itakata?

Lazima utoke smart ukishakubaliwa......mambo mengine mbele kwa mbele.....!!
 
These things sometimz zinakuja automatically! inaweza tokea mkapendana bila hata kuzingatia hivyo vigezo ulivyo vitaja! hujawahi kuona couple ukiiwaangalia hawaendani kabisa...iwe kifedha, kimawazo...personality..n.k ila ndo wanapendana balaa
 
Kbiko yao ni HAMA/RANGE RVR!! Mi first time alinktaa ila nilipomwambia kuwa nina nyumba,gari mbili HAMA&RANG thn nimetoka juz UINGRZA kumalizia mstrs yng na kwa sasa ni boss ktk kampn fulan hapa BONGO ndo akawa amelainka fasta na cku hiyo nikampigia cm mgdo wang anaish MRKN ili anitumie cm aina ya blcbry kma zawd ya mchmba wang .
 
Back
Top Bottom