UPENYO
Member
- Nov 18, 2013
- 44
- 25
Je Unapenda Kumiliki Shamba au Kiwanja katika Wilaya ya Kisarawe?
Nimekuwa nikiulizwa sana na jamaa zangu kuhusu upatikanaji wa mashamba katika wilaya ya Kisarawe. Kwa kuwa mimi ni mzoefu wa wilaya hii kutokana na kufanya kazi katika wilaya hii kwa miaka kadhaa na pia ninamiliki maeneo kadhaa (viwanja na mashamba) katika wilaya hii nimeona nianzishe thread hii ili kusaidia watu wengine pia. Nimekuwa nikiulizwa na jamaa zangu wanaofahamu kuwa kwa sasa niko huku na pia ninajua wako watu wengi wanaopenda kumiliki japo eka moja lakini wanashindwa waanzie wapi, wengine wanaogopa kutapeliwa au wanaelekezwa maeneo mengine penye bei kubwa.
Wilaya ya Kisarawe inapakana kwa sehemu kubwa na wilaya ya Ilala (ktk wilaya za DSM). Kwenda Kisarawe mjini kutokea DAR ni rahisi kwa kuwa ni barabara ya lami - yaani barabara ya Mwl Nyerere, Gongolamboto, Pugu Kajiungeni kisha unaendelea moja kwa moja kupanda milima hadi Kisarawe mjini (Makao makuu ya Wilaya). Kumbuka kuwa Pugu Kajiungeni kuna makutano ya barabara 3 yaani hiyo inayotoka Dsm, inayoendelea kwenda Kisarawe na inayookata kushoto kwenda Chanika. Umbali wa kutoka DSM posta - Askari Monument hadi Kisarawe Mjini ni km 26. Ukifika Kisarawe mjini barabara inaendelea kwenda Chole na Mzenga ingawa lami inaishia sehemu palipo na Kiwanda cha Cement (Kisarawe Cement Company) na ni km 5 toka Kisarawe mjini.
Mahala hapo lami inapoishia ndipo palipo na makutano (junction) ya kwenda Kibaha na panaitwa Mpuyani (kwa jina la wenyeji). Hapa sijui kama watu wengi wanajua (hasa wanaokaa maeneo ya Uwanja wa ndege, Ukonga, Gongolamboto Pugu n.k.) kuwa ni shortcurt ya kwenda Kibaha kupitia Kisarawe. Kutoka Kisarawe hadi Kibaha Maili moja ni km 26. Ukiachia km 5 za lami toka Kisarawe mjini hadi Mpuyani/Kiwanda cha Cement umbali mwingine wote ni wa vumbi ingawa barabara hiyo huwa ni nzuri majira yote ya mwaka kwa kuwa inafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara. Barabara hii iko chini ya TANROADS.
Mashamba au maeneo ninayozungumzia yana ukubwa tofauti kuanzia eka moja na kuendelea na yako sehemu tofauti. Mashamba hayo hayana hati isipokuwa unaponunua uongozi wa serikali ya kijiji ndio unaosimamia mauzo/manunuzi hayo na wanatoa hati za mauzo/manunuzi. Unanunua toka kwa wenyeji au mtu yoyote mwenye eneo. Pia unaweza kuomba toka serikali ya kijiji na ukapata ingawa kwa sasa imekuwa ngumu kidogo si kama zamani. Hii inatokana na ukweli kuwa miaka michache iliyopita kulikuwa na wimbi kubwa la watu toka mjini (Dar) walioitumia nafasi hiyo kujipatia maeneo makubwa kinyume na utaratibu kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa vijiji. Kumbuka kwamba Serikali ya Kijiji imeruhusiwa kisheria kutoa ardhi isiyozidi ekari 50.
Kwa ujumla mashamba yapo katika kata zote. Mengine yapo kando kando ya barabara kubwa ya Kisarawe Chole (hadi Selous), Kazimzumbwi Mzenga hadi Gwata na mengine yapo mbali zaidi kutoka barabarani. Bei inategemea umbali toka Kisarawe mjini na pia umbali toka barabara kuu.
Kwa kufuata barabara kuna vijiji vifuatavyo na umbali ufuatao toka Kisarawe mjini: Kazimzumbwi (10km),.Kisanga (15km), Sungwi (20km), Masaki (26km) na kuendelea. Nimeamua kuishia Masaki tu. Kwa kweli ukianzia Kazimzumbwi na kwenda Chole na Mzenga ardhi ni nzuri. Wenyeji wanalima sana muhogo na pia mahindi na mazao mengine yanakubali pia.
Ukweli ni kuwa sehemu inayoitwa Masaki ni strategic area kwa kuwa ni centre ya siku nyingi (zamani wahindi walikuwa wakiishi hapa) na junction ya barabara inayotoka Chanika kwenda Chole na barabara ya Kisarawe Chole. Kibiashara pana future nzuri ingawa bado ni kijijini. Hata bei za maeneo yake ni kubwa kulinganisha na maeneo mengine.
Kwa ujumla maeneo hayo ni mazuri kwa kilimo hata kwa kuishi. Shida kubwa kwa kuishi ni ukosefu wa maji ya kutosha. Kuna mradi wa umeme uko katika hatua za mwisho wa kuweka umeme katika vijiji toka Kisarawe mjini hadi Msanga (kama km 70) kupitia Maneromango. Nguzo na nyaya tayari vimewekwa. Nadhani umeme unatarajiwa kuwaka kabla ya mwezi Machi, 2014.
Huwa napenda kuwashauri hasa vijana wanaochipukia kuwa wakati ni huu na ardhi ni rasilimali kubwa ambayo mtu anahitajika kuwa nayo kwani mahitaji ya ardhi yanaongezeka kila siku. Kumbuka kuwa miaka 10 tu iliyopita Kimara, Kivule, Pugu, Boko na Bunju na sehemu kubwa ya Kigamboni na maeneo mengine vilikuwa ni mbali sana na Kariakoo na vilikuwa ni mapori. Siku zote kumbuka: uamuzi wa kunua eneo leo ni uamuzi sahihi siku zote...
Baada ya kutoa jiografia hiyo nawaachia wadau watafakari wenyewe. Napenda kuwajulisha kuwa mimi sio dalali na wala sio mfanyabiashara wa mashamba isipokuwa nimeona nisaidie wenzangu japo kidogo. Naamini hii inaweza kuwa msaada kwa wengi wanaohitaji kununua mashamba katika Wilaya ya Kisarawe.
Kama kuna maswali karibuni nitajitahidi kujibu.